Very touchy and heart-moving!Nimelazimika kujiuliza maswali mengi zaidi leo alfajiri baada ya tukio la kusikitisha;usiku wa leo saa tano nikiwa nimelala niliamshwa ili kumkimbiza hsptl bint aliyekunywa betri acid baada ya aliyekuwa boyfriend wake kumuacha huku akidai bado "anampenda" hivyo kuamua kunywa acid hiyo iliyoutoa kikatili uhai wa binti huyo aliyekuwa anatarajiwa kujiunga na chuo,kwani kabla hajakata roho alfajiri ya leo alikuwa anatapika utumbo na vingine vingi,binti huyu alidai upendo ndo ulimpelekea kujitoa uhai kikatili kwani ndivyo alivyokuwa anasema katika masaa machache ya mwisho ya uhai wake na tunamzika leo saa saba,hivi upendo una ukatili huu au ni tafsiri yetu mbovu ya upendo?Hebu tueleze wewe unajua nini kuhusu UPENDO ili utusaidie kupunguza majanga haya au kuyamaliza kabisa,binafsi siamini kama upendo unaweza kumpelekea mtu kushindwa kujithamini na kuwathani wengine pia!Tafadhali naomba maoni au tafsiri yako uwasaidie wengine na tatizo hili!

Very touchy and heart-moving!

Hapo ndo pa kufanyia utafiti kwa interested parties!

Kwa purpose ya LOVE kama sanaa, lazima kuna vitu fulani vya pekee ambavyo huyu kijana alikuwa anamwambia huyu dada enzi wakiwa katika mahusiano mema, vilivyomfanya huyu dada aone kuwa kumkosa huyu kijana haitowezekana kuishi tena..sasa vitu hivyo ndio vinatakiwa kujulikana hadharani!

Huyu kijana akamatwe apelekwe polisi, si kwa nia ya kumfunga, lakini asaidiane na polisi kueleza kwa taratibu alikuwa anamwambia maneno gani huyu binti, then yaandikwe , na itumiwe kama Mwongozo wa kudumu au precedence katika masomo ya mahusiano y kimapenzi!

Binafsi naitazama kesi hii kwa jicho la 3!

Kuna mwana saikolojia mmoja aliwahi kusema, kitendo cha kujiua hua kinajengwa na mawazo ya mtu mwenyewe, yaani kama mtu anapenda kuongelea hili jambo pale tu anapoghafirika au udhiwa na mtu yoyote mfano hupenda kusema " ikitokea hivi mi ntajiua" basi hili hujengeka kwenye akili yake na pale jambo kubwa linampomtokea basi hali ile inamjia na kuchukua uamuzi huo.

Yeye alishauri kwamba mtu yoyte aipende kuwazia hilo tendo la kujiua kama ndo solution yake ya mwisho na unapo sikia kua mwanao au ndugu yako yoyote anapenda kusema hayo maeneo basi fanya kila namna ili aache.