Ni Uovu gani mkubwa zaidi kwenye Maisha ya Mwanadamu?

Ryan Holiday

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,859
3,919
Matendo ya mwanadamu yamegawanyika katika makundi mawili nayo ni matendo ya Nuru (Good Deeds) na matendo ya Giza yani (Evil Deeds).
Evil Deeds - Actions that are intended to harm others and vice versa is true (Good Deeds).

Let's start,
👉By differentiate between Sin, Evil and mistake.

Tofauti Kati ya Dhambi, Uovu na Makosa.

Dhambi - Ni uasi wa sheria ya MUNGU.
Ni matendo yote yaliyo chukizo kwa MUNGU.
1 Yohana 3:4
" Kila mtu afanyaye dhambi, afanya uasi maana dhambi ni uasi."

Maovu/Uovu - Ni dhambi iliyokomaa na kuwa ya kujirudia rudia kwa mhusika.
Isaya 59:2
"Lakini maovu yenu yamewafarakisha ninyi na MUNGU wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia."

Makosa - Ni kutenda mabaya/dhambi kwa kukusudia au kutokukusudia, kwa kujua au kwa kutokujua.
Are You Good Or Evil QUIZ.jpg

Hapo zamani Mwanafilosofia wa Ugiriki Socrates akijulikana Kama "Baba wa Filosofia ya Magharibi" aliulizwa swali?
What is the greatest evil in life? Socrates, reply like this "The Only Good is Knowledge and the only Evil is Ignorance."

Watu wengi walitegemea Greek Philosopher "Socrates" atajibu kwa details zaidi, lakini He make it simple & clear by mentions Four core words.
1.Good - Nzuri
2.Evil - Uovu
3. Knowledge - Maarifa
4.Ignorance - Ujinga

Ni One Good Man opinion, What is yours?
Take it and digest it.
Easy Day
Screenshot_20220404-100600_1.jpg
 
Socrates alitakiwa aseme hilo jibu lake kalitoa kwenye Biblia Takatifu Hosea 4:6.
May be, who knows? Shehullohi

Hosea 4:6​

My people are destroyed from lack of knowledge.
“Because you have rejected knowledge,
I also reject you as my priests;
because you have ignored the law of your God,
I also will ignore your children.

How about you, you stick with the same line or you have some differents perspective.
You are welcome Chum.
👍
 
Ndio katika njia hii ya elimu/maarifa ya kumjua Mungu wa kweli ni yupi. Na baada ya kumjua kumfuata na kuishi sawasawa na Haki yake na Kweli yake. Ili mwisho wa siku nisiwe mtu niliye ishi maisha ya hasara kuu kama huyu wa Muhubiri 5:15-16. Niondoke duniani na Neema ya Wokovu itakayonipa uzima wa milele. Nisije nikaondoka katika ile hali ya kuzaliwa na kufa katika dhambi. To me that will be a very big mistake which is amounting to eternal loss.
 
Ninaweza kujibu katika sehemu mbili
1. Kulingana na kitabu cha 1wakorintho inaonekana uzinifu ndio dhambi kubwa zaidi

1 Wakorintho 6:18-19
[18]Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
[19]Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe.

2. Lakini katika sehemu ya pili kwa maoni yangu naona dhambi iliyokubwa hasa kwa sisi watu wa siku za mwisho ni kutokuamini, maana tulikwisha ahidiwa msamaha wa kila aina ya dhambi na kufuru zote na matukano yote ikiwa utaamini na kutubu, lakini kama huamini huo msamaha utaupataje?, ki ukweli kama huamini hutawaza hata kutubu maana itakuwa ni kama upuuzi kwako.
Angalia hata katika gharika ya nuhu Mungu hakuokoa watakatifu wote ila walioamini kuwa tunaweza okoka tukiingia safinani, hata kisa cha sodoma na gomora hawakuokoka watakatifu wote isipokuwa wale walioamini tukikimbia huu mji bila kugeuka nyuma tutapona bila kujalisha hali yao ya mwanzo.
Lakini pia pigo la mzaliwa wakwanza wa misri, wote walioamini tukipaka damu katika katika miimo ya milango yetu malaika wa kifo akipita tutapona ndio waliookolewa hata literature nyingine zinasema kuna baadhi ya Wamisri waliwaona Waisrael wakifanya hivyo nao kwa Imani wakaiga ingawa haikuwahusu wala hawakuwa sehemu ya mpango lakini kile kitendo cha imani kuiga wale waliowaita watumwa wao, walipona nyumba zao hazikuguswa na malaika wa kifo sio kwa sababu ni watakatifu no, sio kwa sababu ni wenyewe haki no, sio sababu ni ujanja, bali waliamini kile walichokisikia na kukiona kwa watumwa wao wakifanya na hivyo wakapona mifano ni mingi siwezi iandika yote kwa sababu ya muda lakini wasomaji wa maandiko mnaelewa hata habari za Rahabu yule kahaba maarufu mpaka mfalme anamjua.
Na dhambi iliyokubwa ni ile itakayo kunyima uzima wa milele

Kwa hiyo naona dhambi kubwa itakayo ponza wengi siku hizi ni kutokuamini namna ya wokovu ambayo Mungu ameitoa kwa nyakati zetu bila kujalisha hali,lugha,rangi,dini, kabila,taifa lako ambayo ni wokovu tunaopewa kwa neema ila kwa njia ya Imani juu ya damu ya Yesu katika kutakasa dhambi.
Ndugu zangu it's all about faith aaminiye ataokolewa asiyeamini siyo kwamba atahukumiwa la, bali amekwisha kuhukumiwa kwa sababu hakuliamini jina pekee la mwana wa Mungu, Kwa maana hakuna jina jingine walilopewa wanadamu chini ya jua litupasalo sisi kuokolewa kwalo isipokuwa jina la yesu.

Swali la kutafakari:
1 Yohana 5:16
[16]Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.

Dhambi ya mauti ni ipi na isiyo ya mauti ni ipi?
 
Dhambi kubwa kuliko dhambi zote hutokea mwishoni mwa maisha ya kiumbe (Mwanadamu).Katika harakati zote za maisha yako yote jitahidi kabla hujakata ROHO uwe umehusiana na MUUMBA WAKO. Ukifa bila kukiri au Kutubu makosa, maovu au Dhambi zako UTAKUWA UMETENDA DHAMBI KUBWA KUZIDI DHAMBI ZOTE ULIZOZITENDA. Ndiyo maana Mungu anaweza kusamehe dhambi yoyote ile iwe kubwa au ndogo kwakipimo cha Mwanadamu. MUNGU alituweka Duniani akatukabidhi harakati nyingi sana ambazo anajua kabisa kila kiumbe kita gusa hapa na pale, pazuri au pabaya, kwa kujua au kutokujua, kwa kutaka au kwa kulazimishwa. Ila mwisho wa yote ikifika siku yako ya mwisho ukutwe UMEIMBA MSAMAHA. UKIUKOSA MSAMAHA UTAKUWA UMETENDA DHAMBI KUBWA KULIKO.
Nawasilisha
 
Ninaweza kujibu katika sehemu mbili
1. Kulingana na kitabu cha 1wakorintho inaonekana uzinifu ndio dhambi kubwa zaidi

1 Wakorintho 6:18-19
[18]Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
[19]Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe.

2. Lakini katika sehemu ya pili kwa maoni yangu naona dhambi iliyokubwa hasa kwa sisi watu wa siku za mwisho ni kutokuamini, maana tulikwisha ahidiwa msamaha wa kila aina ya dhambi na kufuru zote na matukano yote ikiwa utaamini na kutubu, lakini kama huamini huo msamaha utaupataje?, ki ukweli kama huamini hutawaza hata kutubu maana itakuwa ni kama upuuzi kwako.
Angalia hata katika gharika ya nuhu Mungu hakuokoa watakatifu wote ila walioamini kuwa tunaweza okoka tukiingia safinani, hata kisa cha sodoma na gomora hawakuokoka watakatifu wote isipokuwa wale walioamini tukikimbia huu mji bila kugeuka nyuma tutapona bila kujalisha hali yao ya mwanzo.
Lakini pia pigo la mzaliwa wakwanza wa misri, wote walioamini tukipaka damu katika katika miimo ya milango yetu malaika wa kifo akipita tutapona ndio waliookolewa hata literature nyingine zinasema kuna baadhi ya Wamisri waliwaona Waisrael wakifanya hivyo nao kwa Imani wakaiga ingawa haikuwahusu wala hawakuwa sehemu ya mpango lakini kile kitendo cha imani kuiga wale waliowaita watumwa wao, walipona nyumba zao hazikuguswa na malaika wa kifo sio kwa sababu ni watakatifu no, sio kwa sababu ni wenyewe haki no, sio sababu ni ujanja, bali waliamini kile walichokisikia na kukiona kwa watumwa wao wakifanya na hivyo wakapona mifano ni mingi siwezi iandika yote kwa sababu ya muda lakini wasomaji wa maandiko mnaelewa hata habari za Rahabu yule kahaba maarufu mpaka mfalme anamjua.
Na dhambi iliyokubwa ni ile itakayo kunyima uzima wa milele

Kwa hiyo naona dhambi kubwa itakayo ponza wengi siku hizi ni kutokuamini namna ya wokovu ambayo Mungu ameitoa kwa nyakati zetu bila kujalisha hali,lugha,rangi,dini, kabila,taifa lako ambayo ni wokovu tunaopewa kwa neema ila kwa njia ya Imani juu ya damu ya Yesu katika kutakasa dhambi.
Ndugu zangu it's all about faith aaminiye ataokolewa asiyeamini siyo kwamba atahukumiwa la, bali amekwisha kuhukumiwa kwa sababu hakuliamini jina pekee la mwana wa Mungu, Kwa maana hakuna jina jingine walilopewa wanadamu chini ya jua litupasalo sisi kuokolewa kwalo isipokuwa jina la yesu.

Swali la kutafakari:
1 Yohana 5:16
[16]Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.

Dhambi ya mauti ni ipi na isiyo ya mauti ni ipi?

Dhambi ya mauti ni kumkufuru Roho Mtakatifu/ Roho wa Mungu. Hiyo haina msamaha kwa yeyote yule. Sijui wale walio mfananisha Roho Mtakatifu na nabii flani wataponea wapi kama hawatageuka na kutubu hiyo dhambi.

Mauti iliyo zungumziwa hapo ni ile ya pili ya jehanamu ya moto wa milele yote.
 
Dhambi ya mauti ni kumkufuru Roho Mtakatifu/ Roho wa Mungu. Hiyo haina msamaha kwa yeyote yule. Sijui wale walio mfananisha Roho Mtakatifu na nabii flani wataponea wapi kama hawatageuka na kutubu hiyo dhambi.

Mauti iliyo zungumziwa hapo ni ile ya pili ya jehanamu ya moto na milele yote.
Na dhambi isiyo ya mauti ni ipi?
 
Na dhambi isiyo ya mauti ni ipi?

Dhambi ambayo muhusika hutii dhamiri yake inapomsukuma na inapomsuta pale Roho Mtakatifu anapo msukuma kutubu na akatubu kabla hajafa kifo cha mwili. Niseme hivi kumkufuru Roho Mtakatifu ni kule kutotii kila anapoisukuma dhamira yako kuhusu kutubu dhambi unayoishi. Ukimkaidi na kuacha kumtii na kutubu ukaiacha hiyo dhambi ukafa kifo cha mwili ukiwa nayo ndio ujue umekufa kifo cha umilele kwa kuishia jehanamu ya moto wa milele.

Mfano ni dhambi aliyoitenda Cain ambayo ilisababisha kifo cha mwili cha kwanza kwa kumuua Abel ndugu yake. Mungu alimuasa kuchukua tahadhari lakini dhambi ya uchungu ikamtawala akaishia kuua. Mwanzo 4: 4-8.

Hata wakati wa Bwana Yesu kusalitiwa utaona hii dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ilimkamata Yuda Iskarioti yule msaliti. Alionywa na Bwana Yesu kitajachompata akimsaliti na akakaidi bado akamsaliti. Matthayo 26:24-25.
 
Ni One Good Man opinion, What is yours?
Take it and digest it.
Kwa kuwa tupo duniani kwa lengo la kuendelea kuoneshana upendo na kuishi hivyo basi sawa dhambi ni kulikataa/kuasi lengo hili.

So kumuumiza jirani (kinyume na kumsaidia) ni uasi kukiuka lengo kuu. Na ni dhambi.

Dhambi kubwa ni pale unapomuumiza yule ambaye yeye amekuonesha upendo na kukuamini. Wewe ukafanya kinyume.

Mfano Mungu ametuonesha upendo na kutuamini kwamba anatupa uhai na maamuzi huru ya kuwa tutachagua yaliyo mema na tutamkubali kama Mungu wetu. Kukufuru inakuwa dhambi kubwa. Na kuasi kanuni iliyo kuu ile ya upendo inakuwa dhambi kubwa.

Tafsiri yangu ya dhambi haitegemei kuamini au kutokuamini Mungu(Japo ninaamini). Wacha nitumie baiolojia;
Viungo vyote vya mwili, vimeaminiwa na Mfumo, mind, nafsi na roho na kila mmoja(kila kiungo) kwamba vitatumikiana na kuoneshana upendo. Dhambi kubwa ni pale kiungo kimoja kitawatumia wenzake halafu chenyewe kisitoe upendo na matokeo yake ni kifo. Mfumo mzima utakikataa na kitaondoshwa kikaharibikie huko. Mshahara wa dhambi ni mauti.
 
Thanks Pal'
I appreciate it,
For the nice and astonishing contribution ✌️.
 
Back
Top Bottom