Maisha ya mwanadamu ni mafupi

kwisha

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
1,666
4,365
Mhubiri 12:1

Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, kabla hazijaja siku zilizo mbaya, wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.

Maisha ya mwanadamu ni mafupi sana.
Cheza uchezavyo.
Kula upendavyo.
Vaa uvaavyo.
Tambuwa ipo siku.

Utapotea duniani

Ndipo utakumbuka maneno haya.

Al hajj 1:78

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱتَّقُوا۟ رَبَّكُمْ ۚ إِنَّ زَلْزَلَةَ ٱلسَّاعَةِ شَىْءٌ عَظِيمٌۭ
عَظِيمٌۭ ١

Enyi watu! Tahadharini na mateso ya Mwenyezi Mungu, kwa kufuata amri zake na kuepuka makatazo yake, kwani vituko vitakavyotokea pindi kisimamapo Kiyama na mtetemeko mkubwa wa ardhi utakaofanya pambizo zake zipasukepasuke, ni jambo kubwa ambalo hakuna mwenye kulikadiria wala kulifikia vile litakavyokuwa, wala kujua namna yake isipokua Mola wa viumbe wote.

يَوْمَ تَرَوْنَهَا تَذْهَلُ كُلُّ مُرْضِعَةٍ عَمَّآ أَرْضَعَتْ وَتَضَعُ كُلُّ ذَاتِ حَمْلٍ حَمْلَهَا وَتَرَى ٱلنَّاسَ سُكَـٰرَىٰ وَمَا هُم بِسُكَـٰرَىٰ وَلَـٰكِنَّ عَذَابَ ٱللَّهِ شَدِيدٌۭ ٢

Siku mtakapokiona Kiyama kimesima, mama atamsahau mtoto wake mchanga aliyempa titi lake kunyoya kwa shida iliyomshukia, mwenye mimba ataharibu mimba yake kwa babaiko na akili za watu zitapotea watakuwa ni kama walevi kwa tukio hilo kubwa na babaiko na hali wao si walevi wa pombe, lakini ni ukali wa adhabu ndio uliowapoteza akili zao na hisia zao.
 
Tungekua tunaishi hata miaka 300 ingependeza lkn miaka 60 hadi 70 ni michache sana.

Tuijenge dunia kama tutaishi milele na tufanye mema kama tunakufa kesho.

Sent from my SM-G935F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom