Ni ujinga kuinasibisha hii serikali na uislam

Ni ujinga kuinasibisha hii serikali na uislam

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
15,893
Reaction score
36,391
Uislam ni moja kati ya dini zilizojijengea heshima kubwa kutokana na kufuata misingi imara, maadili na itikadi thabiti. Hata hivyo, katika siku za karibuni kumezuka baadhi ya mashehe na waumini wanaoamini kuwa serikali iliyopo madarakani ni ya dini yao, na kwamba changamoto nyingi wanazipata Wakristo pekee.

Mashehe wengine wamefikia kusema kuwa hawataki maandamano kwa sababu Rais wa sasa anatoka katika dini yao. Huu ni mtazamo potofu na hatari. Ukweli ni kwamba serikali haibagui dini, kabila, wala rangi katika changamoto zinazowakumba Watanzania. Yote tunayopitia ni ya pamoja kama taifa moja.

Mifano ya ukweli huu ni hii:

1. Utekaji na mauaji
Wanaotekwa si Wakristo pekee. Waislam pia wapo. Mfano ni Mohamed Kibao, muislam ambaye alitekwa na kuuawa mchana kweupe. Utekaji haubagui dini.

2. Usafiri na miundombinu
Adha ya usafiri inawakumba wote. Hakuna mwendokasi au barabara maalum kwa ajili ya dini fulani.

3. Uuzwaji wa bandari
Waislam pia ni Watanzania. Athari za kuuzwa bandari zinatugusa wote bila kujali dini.

4. Ukosefu wa ajira
Vijana wa dini zote, wakiwemo Waislam, wanakosa ajira kwa sababu ya ubadhirifu na ufisadi wa viongozi wachache. Tukipinga haya, tunapaswa kuungana wote.

5. Tatizo la maji
Shida ya maji haichagui dini. Kama kijiji hakina maji, hakuna atakayepatiwa kwa kuzingatia imani yake.

6. Huduma za afya
Hospitali kukosa dawa ni changamoto ya taifa. Waislam na Wakristo wote wanateseka sawasawa. Kina mama wetu wote wanakosa vifaa vya kujifungulia.

7. Wafugaji wa Kimasai kufukuzwa Ngorongoro
Waislamu pia wamo miongoni mwa walioteseka na kufukuzwa.

8. Uchaguzi usio huru na wa haki
Mfumo mbovu wa uchaguzi umewadhulumu wagombea wa dini zote, wakiwemo Waisla

Tujifunze kutazama matatizo ya taifa kama Watanzania, si kwa kigezo cha dini. Tuwe kitu kimoja kupinga uonevu, ubaguzi na udhalimu.
Tusiwaachie wahuni na wanasiasa wachache nafasi ya kutugawa kwa misingi ya imani zetu.
Tanzania ni yetu sote — Waislam, Wakristo na wasio na dini. Umoja wetu ndiyo silaha yetu.
 
Dogo acha wenge zimebaki siku 9 tukuone ukiandamana, umeshindwa kuandamana miezi yote 9 iliyopita ndo uje uandamane tarehe 29? Labda uandamane kwa kujaza comments za kupiga mikwara mtandaoni
 
Dogo acha wenge zimebaki siku 9 tukuone ukiandamana, umeshindwa kuandamana miezi yote 9 iliyopita ndo uje uandamane tarehe 29? Labda uandamane kwa kujaza comments za kupiga mikwara mtandaoni
Nitaandamana hapo nyuma kwako.
We utulie tu nitaandamana hapo nyuma kwako
 
Je, unawazungumziaje mashehe wale wanaowambia waamumini wao kuwa hakuna kuandamana ati mambo yote yako safi?
 
Kuna wengine wanasema wao walikuwa mstari wa mbele kupigania uhuru wakati wagalatia mlikuwa mmejificha, sasa ni zamu yenu.
 
Je, unawazungumziaje mashehe wale wanaowambia waamumini wao kuwa hakuna kuandamana ati mambo yote yako safi?
Hao ni wajinga
Basi kama hata watawashauri wasiandamane basi wajitokeze kukemea maovu ya watawala kama ufisadi na utekaji
 
Kuna wengine wanasema wao walikuwa mstari wa mbele kupigania uhuru wakati wagalatia mlikuwa mmejificha, sasa ni zamu yenu.
Lakini Kuna mamia ya mashehe Huwa wanalalamika kuwa walionea na kusingiziwa kuwa ni magaidi na Sasa wapo Ukonga mwaka wa 20 huu
 
Uzuri MaCCM yakitaka kukufanyizia hayahoji wewe ni Mwantumu au John Mwakipesile. Yanakupelekea moto tu, hayacheki na wowote.
 
Ninavyojua mimi Masheikh watakuwa wameongelea kwenye hoja ya kuwepo kwa amani na utulivu nchini lakini si kwasababu eti Raisi wa sasa ni Muislamu

Kwa sababu hofu inakuja huenda hata hii amani ndogo tuliyo nayo inaweza kupotea kabisa

Naamini kabisa viongozi wa dini wanaplay part yao kulingania amani

Ingawa tunawalaumu kwa kutokemea huu utekaji unaondelea hapa nchini kwetu
 
Lakini kumbuka kipindi hiki chote waislam na taasisi zote za kiislam kama bakwata hawajawahi kujitokeza kukemea utakaji na mauaji wala kukemea ufisadi
 
Kobazi hawawezi kemea utekaji wala mauaji yanayoendelea.

Kwasababu bakwata wapo kwenye payroll ya kijani.
 
Back
Top Bottom