Ni ujinga kuinasibisha hii serikali na uislam

Ni ujinga kuinasibisha hii serikali na uislam

Uislam ni moja kati ya dini zilizojijengea heshima kubwa kutokana na kufuata misingi imara, maadili na itikadi thabiti. Hata hivyo, katika siku za karibuni kumezuka baadhi ya mashehe na waumini wanaoamini kuwa serikali iliyopo madarakani ni ya dini yao, na kwamba changamoto nyingi wanazipata Wakristo pekee.

Mashehe wengine wamefikia kusema kuwa hawataki maandamano kwa sababu Rais wa sasa anatoka katika dini yao. Huu ni mtazamo potofu na hatari. Ukweli ni kwamba serikali haibagui dini, kabila, wala rangi katika changamoto zinazowakumba Watanzania. Yote tunayopitia ni ya pamoja kama taifa moja.

Mifano ya ukweli huu ni hii:

1. Utekaji na mauaji
Wanaotekwa si Wakristo pekee. Waislam pia wapo. Mfano ni Mohamed Kibao, muislam ambaye alitekwa na kuuawa mchana kweupe. Utekaji haubagui dini.

2. Usafiri na miundombinu
Adha ya usafiri inawakumba wote. Hakuna mwendokasi au barabara maalum kwa ajili ya dini fulani.

3. Uuzwaji wa bandari
Waislam pia ni Watanzania. Athari za kuuzwa bandari zinatugusa wote bila kujali dini.

4. Ukosefu wa ajira
Vijana wa dini zote, wakiwemo Waislam, wanakosa ajira kwa sababu ya ubadhirifu na ufisadi wa viongozi wachache. Tukipinga haya, tunapaswa kuungana wote.

5. Tatizo la maji
Shida ya maji haichagui dini. Kama kijiji hakina maji, hakuna atakayepatiwa kwa kuzingatia imani yake.

6. Huduma za afya
Hospitali kukosa dawa ni changamoto ya taifa. Waislam na Wakristo wote wanateseka sawasawa. Kina mama wetu wote wanakosa vifaa vya kujifungulia.

7. Wafugaji wa Kimasai kufukuzwa Ngorongoro
Waislamu pia wamo miongoni mwa walioteseka na kufukuzwa.

8. Uchaguzi usio huru na wa haki
Mfumo mbovu wa uchaguzi umewadhulumu wagombea wa dini zote, wakiwemo Waisla

Tujifunze kutazama matatizo ya taifa kama Watanzania, si kwa kigezo cha dini. Tuwe kitu kimoja kupinga uonevu, ubaguzi na udhalimu.
Tusiwaachie wahuni na wanasiasa wachache nafasi ya kutugawa kwa misingi ya imani zetu.
Tanzania ni yetu sote — Waislam, Wakristo na wasio na dini. Umoja wetu ndiyo silaha yetu.
Mafundisho yanasema hivi
Ndugu wa Muislam ni muislam mwenzako
 
Ninavyojua mimi Masheikh watakuwa wameongelea kwenye hoja ya kuwepo kwa amani na utulivu nchini lakini si kwasababu eti Raisi wa sasa ni Muislamu

Kwa sababu hofu inakuja huenda hata hii amani ndogo tuliyo nayo inaweza kupotea kabisa

Naamini kabisa viongozi wa dini wanaplay part yao kulingania amani

Ingawa tunawalaumu kwa kutokemea huu utekaji unaondelea hapa nchini kwetu
Hoja ya kuandamana haijajengeka kwenye misingi ya Raisi kuwa Muislamu bali msingi wake ni kwamba njia ya maandamano na kutoka dhidi ya mtawala haina asili katika Uislamu na ina madhara makubwa . Mfano uchomaji na uharibifu wa miundombinu, wizi , kuuliwa raia nk.

Hata chanzo cha mgawanyiko wa Umma huu lilianza katika kuandamana na kutoka dhidi ya mtawala, kikundi kilisambaza propaganda kuwa Mtawala Khalifa Uthmaani bin Affan ( Allaah amridhie ) kuwa hatendi haki na ana makosa kadha wa kadha wakaandamana kumtoa mpaka wakamua baada ya hapo ikazalika fitna kubwa na maovu kubwa , maaji na migawanyiko , udhaifu nk katika Umma wa Kiislamu.

Jambo la kukemea utekaji na uovu kwa viongozi wa Dini Kuna njia nyingi za busara kufikisha tena nasaha Bora ni za Siri na hio ndio asili ya nasaha hata wewe hautokuwa ridhaa mtoto wako au Mkeo asambaze uovu wako mitaani na makosa yako na kipaza sauti kuwa hatendi haki.
 
Upo sahihi kabisa Mr. Adriz ,unajua Uislamu ndio amani na ndio maana hata salamu yetu ni amani pia

Inasemwa ni kheri kuwa na kiongozi mdhalimu kuliko sehemu isiwe na mamlaka kabisa

Matokeo yake vitaibuka vimamlaka ambavyo haviwajabiki kwa yoyote na matokeo yake ni machafuko kila sehemu..

Uislamu umeyaona haya kwa mapana makubwa sana,ila kwa mtazamo wa wengine watatafsiri tofauti

Mfano baada ya kuuwawa kwa Gaddafi wote tunajua nini kinachoendelea Libya,nchi haikutawalika

Kuuwawa kwa Sadamu Irak nchi haikutawalika,kuulibuka vimamlaka vingi ambavyo haviwajibiki kwa yoyote yule

Ndio mambo sio mazuri hapa bongo land lkn itafutwe namna nzur ya kubadilisha hali hii
 
Hakika mkuu una mtazamo mzuri
 
Back
Top Bottom