....bali kuna mgogoro mkubwa wa kikatiba hapo.
The Court was faced with a similar situation in Seif Sharif Hamad v. SMZ, Criminal Appeal No. 171 of 1992 (unreported). Two of us dealing with this appeal were also in the panel for that appeal. We mused over a number of incongruent provisions of the two constitutions and after that we had this to say on page 18 of the type-written judgment:
Tunapendekeza kuwa mamlaka zinazohusika katika pande zote mbili za Muungano zichukue hatua zipasazo kusawazisha vifungu hivi na vingine nyenye utata ama uwezekano wa kuleta utata baina ya hizi Katiba mbili.
A free translation would be: We recommend to the relevant authorities on both sides of the Union, to take necessary steps to harmonize these conflicting sections and other sections of the two constitutions which are potentially irreconcilable.
It burdens our hearts that such a solemn appeal went unheeded and failed to find purchase like the warning of the Soothsayer to Julius Caesar: Beware the ides of March.
Again, to digress a bit, the earlier version of the 1977 Union Constitution was silent as to which government had authority over Mainland Tanzania for the non-Union Matters. The categorization that such authority was vested in the Union Government existed in the Interim Constitution of the United Republic, 1965, but it was not reproduced in 1977. Professor B.P. Srivastava in his Professorial Inaugural Lecture, The Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 Some Salient Features Some Riddles, delivered on 6th March, 1982, pointed out that omission. He argued that it was unconstitutional for the Government of the United Republic to deal with non-Union Matters for the Mainland Tanzania. Probably that criticism prompted the reinstatement of the 1965 position. We make this observation to underscore the need to be painstaking in writing our Constitution.
yaani hata hii kauli ya kipuuzi iliyotolewa na Kikwete mwanzoni (na niliipinga wakati ule vile vile) watu hawafikirii wanachosema: "NDANI YA TANZANIA ZANZIBAR NI NCHI". Really?
Mkuu Mwanakijiji
Hakuna atakayekusikiliza hapa tumeweka Jambazi sugu pale magogoni unategemea nini? Ameweka group la banyamelenge, Iranians, hata nyang'au naambiwa wameingia kwa mlango wa uani usitegemee kitu kwenye hiki Chama Cha Majambazi.
Sasa hawa wahuni wa Zanzibar wamepata wapi ujasiri wa kuridhia kuligawa taifa na kutengeneza nchi nyingine nje ya hii NCHI moja?!
Hivi hili suala si lilishamalizwa na Mtukufu Rais bungeni
na kukubali kuwa Zanzibar ni nchi katika masuala yasiyo ya muungano?
Je haya mabadiliko yanakingana vipi na mtizamo ule wa serikali ya Tanzania? Ukweli ni kuwa hatua hii haikupaswa kufanywa sasa kwa manufaa ya Wazanzibari wenyewe lakini pia kwa maslahi ya Tanzania. Wazanzibari walipaswa kufocus katika kufanikisha serikali ya pamoja na kuhakikisha kuwa yaliyokusudiwa kama vile kuleta kuaminiana na kushrikiana kati yao kunafanikiwa na sio kuchokonoa kina Mwanakijiji na wazee wa mjini (Mkandara).
Lakini ukiangalia kwa undani wake kilichofanyika hakina athari na muungano labda tu kwa wale ambao tayari wanamitizamo yao kuhusu Zanzibar na wanachongoja ni kupata cha kuhalalisha mitazamo hiyo, na hapa wamepata. [quote[]
Kama wewe huoni haina wengine wote hawaoni; huwezi kuwa na nchi ndani ya nchi nyingine halafu mkabakia kuwa na nchi moja (Ibara ya 1 na ya 2 ya Katiba ya Muungano). Hivi hili linahitaji microscope kuweza kuliona?
Tupunguze munkari nyamani hizi ni nyakati za busara sio kukimbilia conclusions zisizo na mishiko. Huu ni wakati wa uchaguzi tutasikia mengi, sasa kama tutakurupuka kukaa mikao ya kivita kwa kila kinachoibuka ama kinachotengenezwa basi soon tutajikuta kubaya...
omarilyas
sasa ningekuwa mimi wewe ningesema wenye munkari ni hawa jamaa wanaojaribu kulazimisha vitu ambavyo vinatokana na jazba na munkari.. but I guess huwezi kuwakemea hao au kutaka wapunguze munkari.
Kaka muungano hautalindwa kwa kuitana wahuni.....
omarilyas
mzee mwanakijijiForest Gump alisema "stupid is as stupid does".. guess what..mhuni anajulikana kwa uhuni anaofanya. Na hili si tusi naelezea tu kile ninachokiona. Ila waweza kunisahihisha kabisa kwa kuniambia kinachofanyika si uhuni ukinishawishi nitabadili msimamo.
Sasa mmeanza kubweka ee yamekushindeni ya Mafisadi mlibweka hapa wee leo wao ndio wanaokufanyeni Gari la ngombe sukani puwa, nafikiri mwanakijiji unajifanya hayawani kwa makusudi na kujisahaulisha matokeo muhimu ulisahau wakati ule mwakiyembe aliposema ndani ya Bunge eti viongozi wa Zanzibar hawana Adabu na watiwe adabu nafikiri kauli tosha ya Mr Ali juma shamhuna ilitosha kumnyamazisha yeye na wenziwe kama alivyosema Mr shamhuna ni nani mwenye uwezo wa kulitia adabu viongozi wa zanzibar?na kama wewe unahisi Hao wawakilishi watiwe pingu basi na watumwe wakuwatia pingu wafanye hivyo halafu utaona nini kitakuwa kwa tarifa yako wazanzibari hawapo Desperate na pia mabadiliko yamekuja wakati mzuri tunaanza saumuKujaribu kuvunja Jamhuri ya Muungano kwa kisingizio chochote kile cha kisiasa ni uhaini. Mnaweza kutafuta kura na support ya wapiga kura lakini ukweli ni kuwa kuna nchi moja ambayo ni Jamhuri ya Muungano ambayo imetokana na kuungana kwa nchi mbili huru za Tanganyika na Zanzibar.
Jaribio la upande mmoja kuirejesha kinyemela nchi iliyokwisha ungana na nyingine ni kutangaza secession kutoka kwa Muungano na viongozi wote wanaopanga kufanya hivyo ni wa kutiwa pingu.
Sijawahi kufikiria kusema JWTZ liangalia ulinzi wa Katiba lakini wakati huu endapo mabadiliko yanayopendekezwa Zanzibar yatafanyika ni wakati wa kuwaangalia hawa "maadui wa ndani".
Ati wenyewe wamekaa kupitisha mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ili kipengele kimojawapo kisomeke hivi:
Wenyewe wanashangilia!! Lakini wanasahau kabisa waliapa kulinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayosema (msisitizo wangu):
na Magenius wetu hawaoni tatizo hapo: Je hii ni chemsha Bongo? Hivi ukisoma katiba hizo mbili utaelewa kuna nchi "ngapi"? Hivi hata hesabu za seti hawazielewi masikini wa Mungu au somo la mantiki linahitaji kufundishwa kuanzia darasa la kwanza?
Kama a. Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo "LOTE" la Tanzania bara na eneo "LOTE" la TAnzania Zanzibar, sasa Zanzibar ina ENEO GANI ambalo si sehemuya Eneo la Jamhuri ya Muungano? Kama seti moja inahusisha wanyama wote wa mwituni na seti nyingine inauhusisha simba na chui ambao nao ni wanyama wa mwituni, inakuwaje mtu anaanzisha seti nyingine inayosema "wanyama wa mwituni"?
Wanachezea maneno lakini maneno yana maana. Na miye natumia nasema kinachofanyika ni uhaini... (mnaweza kutafuta namna nyingine ya kulikwepa neno hilo). Lakini wataalamu wetu hawa hawa wanasahau Ibara ya 28:3 ya Katiba (waliyoapa kuilinda) inasema nini:
(
Sasa hawa wahuni wa Zanzibar wamepata wapi ujasiri wa kuridhia kuligawa taifa na kutengeneza nchi nyingine nje ya hii NCHI moja? Kuna njia moja tu ya kuunda Nchi ya Zanzibar- KUJITOA kwenye MUUNGANO. Nje ya hapo ni UHAINI!!!
I couldn't be more blunt than that.
Labda nikumbushie sehemu kidogo tu ya hotuba ya Baba wa Taifa kwenye Bunge lililoridhia Muungano Aprili 25, 1964 (msisitizo wangu):
Ooh how prophetic!!!
I'm standing on guard, by CHOICE!
mzee mwanakijiji
naona unapiga kelele lazima znz iwe kwenye muungano ,hebu nipe faida 3 ambazo tanganyika inapata kwenye huu muungano.vile vile naomba unipe hasara 3 ambazo tanganyika itapata ikiwa znz itajitenga .
ikiwa kweli tanganyika ina hamu na muungano why not unite with kenya ,uganda or whatever they speak swahili as well.ikiwa ndoa yako ina matatizo you always have to move on to find another wife or husband .you dont have to force it.
Mwawado, bara wala hatuhitajiki kuulizwa; hili ni suala la Zanzibar..sisi tumelalamika lini kuidai Tanganyika? Kumbuka hata hoja ya G55 ilitokana na Zanzibar na OIC (rejea kitabu cha Mwalimu). Hilii ni suala la Zanzibar TU.