Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 58,968
- 132,599
Pole Mzee Mwanakijiji,Kujaribu kuvunja Jamhuri ya Muungano kwa kisingizio chochote kile cha kisiasa ni uhaini. Mnaweza kutafuta kura na support ya wapiga kura lakini ukweli ni kuwa kuna nchi moja ambayo ni Jamhuri ya Muungano ambayo imetokana na kuungana kwa nchi mbili huru za Tanganyika na Zanzibar.
Jaribio la upande mmoja kuirejesha kinyemela nchi iliyokwisha ungana na nyingine ni kutangaza secession kutoka kwa Muungano na viongozi wote wanaopanga kufanya hivyo ni wa kutiwa pingu.
Sijawahi kufikiria kusema JWTZ liangalia ulinzi wa Katiba lakini wakati huu endapo mabadiliko yanayopendekezwa Zanzibar yatafanyika ni wakati wa kuwaangalia hawa "maadui wa ndani".
Ati wenyewe wamekaa kupitisha mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ili kipengele kimojawapo kisomeke hivi:
Wenyewe wanashangilia!! Lakini wanasahau kabisa waliapa kulinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayosema (msisitizo wangu):
na Magenius wetu hawaoni tatizo hapo: Je hii ni chemsha Bongo? Hivi ukisoma katiba hizo mbili utaelewa kuna nchi "ngapi"? Hivi hata hesabu za seti hawazielewi masikini wa Mungu au somo la mantiki linahitaji kufundishwa kuanzia darasa la kwanza?
Kama a. Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo "LOTE" la Tanzania bara na eneo "LOTE" la TAnzania Zanzibar, sasa Zanzibar ina ENEO GANI ambalo si sehemuya Eneo la Jamhuri ya Muungano? Kama seti moja inahusisha wanyama wote wa mwituni na seti nyingine inauhusisha simba na chui ambao nao ni wanyama wa mwituni, inakuwaje mtu anaanzisha seti nyingine inayosema "wanyama wa mwituni"?
Wanachezea maneno lakini maneno yana maana. Na miye natumia nasema kinachofanyika ni uhaini... (mnaweza kutafuta namna nyingine ya kulikwepa neno hilo). Lakini wataalamu wetu hawa hawa wanasahau Ibara ya 28:3 ya Katiba (waliyoapa kuilinda) inasema nini:
(
Sasa hawa wahuni wa Zanzibar wamepata wapi ujasiri wa kuridhia kuligawa taifa na kutengeneza nchi nyingine nje ya hii NCHI moja? Kuna njia moja tu ya kuunda Nchi ya Zanzibar- KUJITOA kwenye MUUNGANO. Nje ya hapo ni UHAINI!!!
I couldn't be more blunt than that.
Labda nikumbushie sehemu kidogo tu ya hotuba ya Baba wa Taifa kwenye Bunge lililoridhia Muungano Aprili 25, 1964 (msisitizo wangu):
Ooh how prophetic!!!
I'm standing on guard, by CHOICE!
May God help us and our brothers in Zanzibar and Pemba to fulfill this responsibilities.!
Unadhani iwapo jeshi linavamia Zanzibar, wazanzibar tutafunga mikono tukutazameni mnfavyofanya uhuni wenu...kama mlivyowafanyia Uganda...unajidanganya? au unadhani hilo jeshi lenyewe litabaki kama lilivyo baada ya kitendo hicho...kumbuka vijana wetu wazalendo, wapenda na wenye uchungu wa nchi yao ya Zanzibar pia wamo humo humo JWTZ, so unazungumzia CIVIL WAR THEN not military intervention any more...?
Tatizo viongozi wetu wame liachia hili swala mpaka lime kua a controversial issue. Itafika kipindi kudiscuss Muungano ita kuwa kama kudiscuss dini. Mkuu Mwanakijiji maybe this is a wake up call that something should be done now. Tuta fika kipindi tuta kuwa kwenye point of no return. But mambo mengi nalaumu mfumo ulio wekwa kuendesha Muungano na nita rudi baadae kuelezea kwa nini (kwa maoni yangu).
Lakini Watanzania bara hatujafanya lolote kuonesha kuwa haturidhiki na Muungano. Hatujadai Tanganyika kwa namna yoyote ile. Kwa hiyo hili ni suala la Zanzibar tu.
NI asilimia ngapi ya kura za pande mbili zitahesabika kuwa watu wanataka? simple majority au absolute majority?
Ingekuwa rahisi kutengana kila watu wanapotaka Quebec ingekuwa imeshatengana na US ingekuwa imeshatengana. Ninachoona ni woga na kutotaka kugonganisha vichwa watanzania kutetea misingi ya taifa lao. Kuna aibu fulani hivi inawakumba watu kusikia wanatetea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Urusi ilitengana lakini unadhani ndio ulikuwa mwisho wa matatizo kati yao? remember masuala ya Chechyniya na Georgia, au kuvunjika kwa Yugoslavia na mambo ya Montenegro, Sebria, Slovakia na Macedonia, Albania na Kosovo. Kutengana si mwisho wa matatizo ya mahusiano.
Hadi hivi sasa sijaona hoja hasa za "upande mmoja haziutaki" ni viongozi wahuni tu wa CCM na CUF ndio wanafanya hivi. kama waliweza kuwauliza Wazanzibari kuhusu mfumo wa serikali yao kwa kura ya maoni kwanini wasiwaulize kama wanataka au hawataki. Na uamuzi watakaochukua sisi Bara tutauheshimu.
Belgium inatawalika; na Yugoslavia ndio kama nilivyosema hapo juu. Lakini miungano hiyo si sawa na Watanzania. Sisi hatukuunganishwa kwa nguvu. Muungano wetu unafanana sana na wa US kuliko sehemu nyingine.
Thats my point. Mimi sina hofu, lakini pia simuumini wa urahisi rahisi wa kuvunjika kwa jamhuri ati kwa sababu sehemu fulani ya jamhuri "hawataki". Ni kitu gani kitazuia watu wa Kilimanjaro kujitenga wakiamini kuwa kwa kufanya hivyo wanatetea maslahi yao ambayo wanaona hayapatikani ndani ya Muungano? Hapo si tutaweza kutumia mfano wa Sudan na Sudani ya Kusini?
kwa hiyo baada ya kuundwa kwa hii nchi ya Zanzibar kutakuwa na raia wa Zanzibar vile vile au watakuwa bado ni raia wa Tanzania? Hii nchi nyingine ndani ya nchi nyingine itaweza kutoa pasi za kusafiria au kama wakitaka kuna sababu ya wa kuwakatalia kuwa hawawezi?
Hakika mimi si shabiki wa vita and I believe in dialogue, Lakini kwamba Jamhuri ya Watu wa Zanzibar inaweza kupigana na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania NAONA NI KICHEKESHO CHA MWAKA. MAHALI PAKE NI ZE COMEDY!
Bwana wanataka nchi
kula tano ndugu yangu.mkjj namkubali kwa mambo mengi lkn kwa hili sipo pamoja naye hata kidogo. baba aliingia kwenye ndoa akajuta lkn alikwisha chelewa.kumbuka alimpa likizo ya ghafla mwanasheria wake na akaazima mwanasheria toka naijeria ili amuandalie raasimu ya muungano chapu chapu akijua kabisa mwanasheria wake asingekubaliana naye. sasa mwana anavunja ndoa kuna dhambi gani??je dunia haijapata kushuhudia uwepo wa ussr???? je leo hii iko wapi?????
Hii nchi ni yetu sote na ni lazima sote tuulizwe. Tunaweza kushangaa hapo watakapokuta kuwa machogo nasi hatuutaki Muungano! Huku kutingisha kiberiti lazima kuwe na mwisho wake. Hii imani ya kuwa tuko tayari kuulinda Muungano kwa gharama yeyote ndiyo inayowapa kiburi. Watapojua kuwa hatuko tayari kumwaga damu kwa kitu ambacho ni figment ya imagination pengine watasita kabla ya kufanya upuuzi huu. Wasitugeuze Spain na Catalanya!
Amandla.......