Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Kuna topic tayari inazungumzia ufisadi wa Sitta ambayo ilitetwa na GT. Pitia huko ndiyo utajua. Ufisadi siyo EPA, Richmond na Kagoda tu. Kama Spika anatumia UDS 8000 kwa mwezi kulipia nyumba, thamani za ndani Tshs 250 million then nafikiri utajaza mwenyewe.......!!!!!!!!!!!!!!

Mi simtetei Sitta, ila ninachohitaji ni Source documents!, hizo topic mi nilishazipitia zote, ila sijaona sehemu yenye source documents zinzoonesha ufisadi wa Sitta. Kagoda na EPA nilisoma report yote na kuona source documents. Sasa kwa nini tuamini hear says?, Hapa JF huo si utamaduni watu wanakuwa convinced na source documents. Vinginevyo itaendelea kuchukuliwa kama udaku mpaka hapo tutakapoona source documents za ufisadi huo.
 
Lakini Tanzania Daima wameqoute waraka uliosambazwa,hata wememqoute mwenyewe kwamba amesema ni wa kipuuzi uzushi na chuki ,kwa hiyo mwanzisa thread hii analojambo anapo link majibu ya Spika na kushushuliwa kwa Gazeti. Spika siangeona imekuwa vizuri gazeti limeweka peupe waraka unaosambazwa .ni hiari yake kuudharau kama hauna ukweli ndani yake au kuusimamisha kwa kuutolea maelezo haitoshi tu kusema maadui zake wanamuwinda yeye ni kuueleza umma ukweli ni upi jamii inatabia yakuamini roumors apende asipende atakuwa na maadui wengi kwa sababu umekuwa mtindo wa CCM sasa hivi kuuana wenyewe kwa kutumia vyombo vya habari utakuta akina Mkapa akina Sitta na wengine na wengine,hatusomi tena habari za maendeleo ya nchi kila siku ni matatizo tuu hali hii inaudhi sana.


Kama ni msomaji mzuri wa magazeti utakuwa umegundua kwamba Tanzania Daima ndilo limekuwa likiandika sana habari chafu dhidi ya Spika, bila kujali chanzo cha habari hizo. Kutaka maoni yake ni kuhalalisha tu habari zao na ndivyo wanavyoelekezwa na hao mafisadi wanaowatuma. Nani asiyejua kwamba kuna watu wana kisasi na Spika?
 
Last edited:
"Kuna kikundi kipo dsm kinatunga haya na kyaweka kwenye Internet baada ya hapo wan magazeti yao wanakopi kwenye magazeti yao na kuandika kama Tanzania Daima,Tazama n.k hawa watu wanatumia hela nyingi sana kutoka kwa wafadhili wao na baadhi wanapeleka jimboni urambo lakini wanasaidia kupunguza umaskini na kugawa pikipiki hata hivyo uchaguzi ujao nitashinda na Mungu akiniweka hai nitaendelea kuwa spika wa bunge hili,
Ndugu Waziri mkuu naomba niongezewe ulinzi hawa watu wanaweza kunimaliza"

Nukuu ya leo kutoka kwa Spika Je tumuongezee Spika ulinzi kwa ufisadi unaosemekana???
 
Yeye ni muwindaji porini hivyo lazima arudi na Nyama nyumbani
 
Baada ya yote kila fisadi ahame nchi ,one day yes tutawatia mikononi tu ,hilo halina ubishi.
 
Kama ni msomaji mzuri wa magazeti utakuwa umegundua kwamba Tanzania Daima ndilo limekuwa likiandika sana habari chafu dhidi ya Spika, bila kujali chanzo cha habari hizo. Kutaka maoni yake ni kuhalalisha tu habari zao na ndivyo wanavyoelekezwa na hao mafisadi wanaowatuma. Nani asiyejua kwamba kuna watu wana kisasi na Spika?


Pitapitia thread utaona kuwa ufisadi wa Sitta pia ushajadiliwa humu. Unless unataka kusema GT ni mmoja wa wafanyakazi wa Tanzania Daima.

Kodi USD 8000 kwa mwezi, fenicha za Tshs 250 m?? need to say more????
 
Jambo la msingi kwa mzee wetu huyu ni kueleza upande wa pili ambao anaamini kuwa ndio sahihi na akithibitisha kwa vielelezo.
Hivi hao waliotuhumu mbona hawakutuletea vielelezo? Tumewaamini kwa maneno yao tu, kwa nini na huyu tusimwamini kwa maneno yake tu? Sheria zetu zifauata principle ya commonweath-You are innocent until proved guilty. Let the accusers prove that Sitta is guilty kabla hatujamkondemn mzee wa watu
 
hivi anatumia viagra au kuna mizizi ya kinyamwezi anaweza kweli kuwa nao wanawake kumi ,atupe hizo skills basi

Wanasema katembea na wabunge 12 hadi wa upinzani yule mdada wa chadema Mdee na yeye kampitia??
 
Mzeepunch umetumwa hapa na spika sitta nini?
Mimi binafsi nimemsikia alivyosema. Ilikuwa ni baada ya kutambulisha utitiri wa wageni wa bunge.
Kwanza nashangaa mzeepunch ulivyohusisha thread hii na Tanzania Daima wakati ameitaja ikiwa ya pili baada ya gazeti la Tazama. Sasa mbona Tazama haimo kwenye heading yako? inaonekana amekutuma uiseme TD.
Kwa mujibu wa maelezo yake nimeona ni kama anavyofanya siku zote anapotuhumiwa. Huwa ana kawaida ya kusukumia zigo kwa wabaya wake kisiasa bila ya kuwataja ni wapi hao na siku zote amekuwa akiwa link na magazeti lakini hajawahi kukana tuhuma nzito zinazomkabili, ikimaanisha ni kweli yale anayotuhumiwa ila tu sasa wabaya wake wame capitalize kwa hayo ili kumbomoa. Hii haiwezi kumuepusha na tuhuma na lazima awajibike kuliko kulialia.
Yeye amekuwa akijifanya msafi kumbe si msafi kiasi hicho hicho kidogo kama wengine.
Kisha angalia alivyojichanganya. Yeye anasema kuwa wabaya wake wanakaa na magazeti na kufanya mikakati kutengeneza tuhuma kuanzia kwenye mitandao na kisha magazeti yanajifanya ku refer habari hizo kwenye mtandao. Bila shaka hapa inahusishwa JF. Lakini anasahau kuwa kashfa nyingi sana zimeanzia hapa JF na hata kuleta mabadiliko yasiyo ya kawaida.
Na kwa sababu hiyo si ajabu mzeepunch katumwa kuja kufanya matengenezo kwa kuleta haya anayoleta. Ningeamini anayosema kama angesema yote aliyosema mzee Sitta.
Mwisho siwezi kuamini yote anayotuhumiwa Sitta lakini kuna moja ninalojua kwa hakika huyu mzee ni mgonjwa kwalo nalo ni kufungua zip. Hapo kwa namna yoyote kuna kaukweli maana huu huwa ni ugonjwa wake.
Na si yeye pekee bali waheshimiwa wetu wengi wana kaugonjwa haka.
Anaweza kujitetea anavyoweza lakini ukweli utabaki rohoni mwake.
 
Pitapitia thread utaona kuwa ufisadi wa Sitta pia ushajadiliwa humu. Unless unataka kusema GT ni mmoja wa wafanyakazi wa Tanzania Daima.

Kodi USD 8000 kwa mwezi, fenicha za Tshs 250 m?? need to say more????


Official residence ya Spika ilishauzwa kwa Spika aliyetangulia (Msekwa), unataka Spika wa sasa akakae Tandale? Unaweza kuona USD 8,000 ni nyingi sana, lakini inategemea na hadhi yako. Hayo ni makosa ya serikali kuuza nyumba bila kufikiri.
 
Kupendwa na kuchukiwa mahara pa kazi ni mamboa ambayo yapo tuu,ila kwa experience yangu a,abongo akichukiwa kazini ujue ni mnoko sijui na kwa sita ni ivyoooooooooo!!!!!!!
 
Tusipuuze haya mambo mtu hawezi kaa na kuanza ku cook information. bila shaka wahusika watayafanyia kazi na ujumbe umefika
 
Ana hakika kwa sababu ya ile kamati aliyoitambulisha bungeni imemuhakikishia kumpa fadhila ya kuisafirisha kwenda Dodoma😀 Na anatisha competitors wake
 
Spika Sitta amekula akilazimisha kukiukwa kwa kanuni za bunge ili tu kuwapa nafasi wabunge wenzaki walio katika kambi moja kuisulubu serikali ili kuwaaminisha wananchi serikali ni ya hovyo bali yeye na wabunge hao ndiyo wana uchungu wa kweli na taifa hili.
hii ndio sababu ya yote hayo??
 
Anatumia vyombo vya umma kufanya ufuska

Sina uhakika kama kichwa changu kimeelewa hii sentensi practically inakuwaje. Yaani SS anatumia VYOMBO vya umma kumega wanawake....kivipi yaani? au huo ufuska una maanisha nini hapo? na vyombo vya umma ni vipi hivyo? jeshi, mahakama, bunge au nini?

Tuhuma nyingine tunazozirusha jamaani....kazi kweli kweli!
 
Baada ya kuchoshwa na tuhuma nyingi zinazoelekezwa kwake kupitia magazetini, muda mfupi uliopita spika samwel sitta amesema tuhuma hizo zinapikwa na watu wasiompenda wakiyatumia magazeti ya tanzania daima na tazama. Huko nyuma tuliwahi kusikia kuwa wahariri wa gazeti la tanzania daima (absalom kibanda na charles mulinda) wamenunuliwa na mafisadi wakiongozwa na r.a. Ili kuwashambulia maadui zao, akiwemo spika sitta. Hawa wamekuwa pia wakilitumia pia jamvi hili la jf kupenyezaa upuuzi wao. Akizungumza kwa kujiamini spika ameonyesha kukerwa zaidi na tuhuma kwamba anapanga njama za kuchoma ofisi za bunge ili kuharibu ushahidi wa baadhi ya tuhuma. Sasa amemuomba waziri mkuu amuongezee ulinzi kwani anadhani watu hao ni hatari.

Siwezi kujibu kuhusu unachokiita matumizi yangu… kwa mtu kama mimi siwezi kukosa maadui katika nchi hii, nimeusoma huo upuuzi, si lolote, wanachotaka ni Bunge, poa,” alisema Spika

THAT HAS SUMMED ALL? hat Lowassa alitumia maneno karibu ya haya.
 
Kunaweza kukawa na mambo matatu;
1. Inawezakana ikawa kweli hivyo tusipuuzie.

2. Inawezekana kuna mtu anataka kugombea jimbo la Mheshiwa six hivyo anatumia njia mbalimbali kumchafua ili wapiga kura wamchukie. Kama hii ni kweli atashindwa kwa sababu ukiangalia maneno yaliyoandikwa hapo ukumwambia mtu atoe ushahidi hawezi. Hivi mh. six anaweza akawa mmbanjuaji namna hiyo mpaka awabanjue wabunge 12 na hao wahasibu?

3. Inawezekana walioandika wana wivu wa kupindukia kuona wenzao wanaendelea na wao wako hapo hapo. Unajua mtu akishakuonea wivu anatafuta kila njia ya kukuharibia na akiwa mchawi anakuondoa moja kwa moja.
Naona tupime hili jambo kwa njia hizo 3.
Nawakilisha wakuu.
 
Hata hivyo Spika 6 tusimwamini saana kana kwamba ana governor ya kutopenda kujinufaisha. Lazima tujue kwamba lisemwalo lipo
 
Back
Top Bottom