Ni sahihi Mwanaume kumkopa Mchumba wake hela?

Ni sahihi Mwanaume kumkopa Mchumba wake hela?

Ndugu, mke, mchumba, hawara, mchepuko, nyumba ndogo huwa hawakopeshwi hiyo ni sheria namba moja katika kanuni za ukopeshaji
 
Maisha kusaidiana. Siyo unakuwa na mtu ambaye hata ukiwa na shida hakupi msaada wowote.
 
Inategemea na mahusiano yenu yakoje
Bond yenu ikoje kama ipo vizuri sidhani kama ni big deal kukopeshana pale mmoja wetu anapokua na shida

Coz mahusiano ni kusaidiana nyakati zote tukijua kupokea tujue na kutoa pia
 
Inategemea na mahusiano yenu yakoje
Bond yenu ikoje kama ipo vizuri sidhani kama ni big deal kukopeshana pale mmoja wetu anapokua na shida

Coz mahusiano ni kusaidiana nyakati zote tukijua kupokea tujue na kutoa pia
Naomba tuwe wapenzi unikopeshe
 
mimi kipindi nipo kwenye rait traki wapenzi wangu niliwapa maisha mazuri sana...
nilijitoa kwao na kwenye shida zao !
ingawa wote wako na kazi zao nzuri tu lakini nilipokuwa na pesa extra nilikuwa nawawekea na kwenye akaunti zao..

ya mungu mengi sasa hivi sina kazi yaani nimepigika na hali hii sikuwahi kuitarajia...
nilitumia tumia balance niliyokuwa nayo kama kusoma lugha zingine na kulipia ada watoto!
kumbuka hapo sipati income kubwa kama ya mwanzo hivyo baada ya huu mwaka kuanza mambo yakazidi kuwa tight..
kiukweli wale wapenzi wangu nilienda nao vizuri tuu na walijua kipindi nnachopitia!sikuwa naomba au kuwakopa ila nilikuwa natia huruma tuu na wao wenyewe kujiongeza sababu ni waelewa..

ila mmoja ameanza dharau hivyo nimempotezea kiaina..maana sitaki kufika kwenye kuleteana dharau.

mwingine bado nipo nae tunaendelea kulisongesha na karibuni ataitwa mama.

maisha ni kupanda na kushuka katika kipindi unapitia magumu ndio utawajua watu na akili zao.hasa hawa wapenzi au wake
 
Kama umekwama sana na hauna namna nyingine fanya hivyo, ila sasa usifanye mazoea. Kama lengo lenu ni kuja kuishi kama mume na mke hapo baadaye usifanye mazoea kabisa, safari itaishia njiani.

Yaani anakuamini kabisa wewe ni jembe na mpambanaji mara ghafla yeye ndo anageuka mtatua matatizo kiuchumi, kengele itagonga kichwani mwake.
Huo ndo ukweli wenyewe.
 
Hata siku moja siwez kumkopa mwanamke pesaaa...Nitafanya hvo Endapo tu yy hanaa Pesa na ana shida ya pesa....Uwa namwambia kama kuna mtua anaeza akampa pesa achukue then me ntarudishaa...ila siez kumuomba pesa mtu wangu ata siku mojaa...Ata iweje....Sina Amani kutumia pesa yake ukizingatia nimemuacha mbali kimshahara
 
Khaa yaan mwanaume hujanioa ushaanza kauli za "nisaidie hela" si hata mahari utaomba nikusaidie kulipa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] pambana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Inategemea na mahusiano yenu yakoje
Bond yenu ikoje kama ipo vizuri sidhani kama ni big deal kukopeshana pale mmoja wetu anapokua na shida

Coz mahusiano ni kusaidiana nyakati zote tukijua kupokea tujue na kutoa pia
"mahusiano ni kusaidiana nyakati zote"

"inategemeana na mahusiano"

shukrani mkuu, nimepata kitu
 
Back
Top Bottom