Ni sahihi Mwanaume kumkopa Mchumba wake hela?

Ni sahihi Mwanaume kumkopa Mchumba wake hela?

osmaney

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2017
Posts
1,042
Reaction score
1,000
Habari wana Jf!

Poleni sana na majukumu ya siku ya leo, nawapa hongera pia kwa utaftaji. Mungu azidi kuwabariki katika shughuli zenu[emoji120]

Kama mada inavyojieleza pale juu, kiukweli kwa upande wangu sijawai kumkopa, sema leo sijui nijaribu.[emoji28] dahh sema sijui atanichukuliaje?

Anyway ngoja kwanza nikusanye maoni apa jukwani kwanza kisha ushauri wenu nichanganye na akili zangu kisha nitoe maamuzi sasa.

Naheshimu sana maoni yenu.

karibuni[emoji116]
 
ukiachana na mapenzi, mahusiano kazi yake nyingine ni kusaidizana hivo usione aibu kumkopa na majibu yake ndo yatakupa mrejesho kama anakupenda au la.
shukran mkuu, sasa nazid kupata moyo wakufanya hivyo
 
endapo nitarudisha?
Hilo siwezi kujibu sijui uaminifu wako upoje,sio unadaiwa hela baadae unaona unaonewa unataka usamehewe kwasababu ya mapenzi 😅😅Wengi wanajisahau kama deni ni deni tu 😊 lakini kama ni mwanamke muelewa atakusaidia na kukupa hio pesa ila kukopeshana kwenye mapenzi ni mtihani rafiki!
 
Kumkopesha mpenzi kwakweli ni changamoto.....ata mimi nsingempa labda kwa kumsaidia ambayo haitakuwa mkopo wa kudai
Apo bora kutumia kauli gan, naomba nikope au naomba nisaidie?
 
Hilo siwezi kujibu sijui uaminifu wako upoje,sio unadaiwa hela baadae unaona unaonewa unataka usamehewe kwasababu ya mapenzi [emoji28][emoji28]Wengi wanajisahau kama deni ni deni tu [emoji4] lakini kama ni mwanamke muelewa atakusaidia na kukupa hio pesa ila kukopeshana kwenye mapenzi ni mtihani rafiki!
hahah nikakiasi kadogo tu, staki kumpa mzigo mzito binti wa watu[emoji28]
 
Back
Top Bottom