Transparen: Kwa hiyo hao uliowataja hawapo hadi aje yeye? Ni nadra kumwona CDF kwenye press conference. Labda kuwe na tangazo la hatari linaikabili nchi hasa kutoka nje ya mipaka ya Tanzania. Mgawanyo wa madaraka ni kwamba Polisi wanashughulika na usalama wa raia na mali zao na JWTZ ni usalama wa nchi na mipaka yake. Ni maoni yangu kwamba asiaibishe hadhi ya JWTZ. Hilo ni jeshi letu pendwa lenye heshima iliyotukuka. Mambo ya ndani awaachie polisi. Kuingiliana majukumu hakuna ufanisi.