Ni sahihi maduka ya rejareja mtaani kuuza dawa baridi?

IKIRIRI

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
2,734
3,017
Hapa mtaani kwangu nimegundua maduka karibia yote, wanauza dawa baridi Panadol, Cofta, Paracetamol, Hedex nk.
Pia wanauza na condom.

Pia nimegundua baadhi ya dawa wanazouza ukienda maduka rasmi ya dawa baridi huwezi kupata. Pia dawa zao zimekaa muda mrefu sina hakika kama wahusika wanafuatilia.

Swali langu la msingi ni sahihi kwa maduka ya aina hii kuuza dawa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hairuhusiwi hiyo, sema unakuta sehemu nyingine hasa vijijini hakuna Famasi, au zipo mbali sana..so hayo ya rejareja yana save. Ila wanauza dawa simple tu kama anti biotics na pain killers

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kosa kubwa sana ingawa mitaani tunapoishi hii kitu ni common.

Mamlaka husika inatambua hili?
 
Sifahamu kuhusu kuruhusiwa au kutokuruhusiwa ila hilo jambo mbona lipo miaka mingi tu? nchi nyingi tu pia nilizozitembelea unapata baadhi ya dawa toka kwenye maduka ambayo sio maduka ya dawa.
 
Back
Top Bottom