Ni sahihi kumkaribisha Muislamu nyama ambayo haikuchinjwa kidini?

Hizo bidhaa huwa zinaandikwa HALAL,,zikimaanisha zimefuata sheria za kiislamu
Hata iliyoandikwa hivyo mtu anatumia kwa imani tu. Ataaminije kama haijaandikwa kwa lengo tu la kumridhisha lakini kanuni ya uchinjaji haikuzingatiwa?
 
Hiyo dini ya hovyo sana
Imani ni kitu sensitive sana mkuu! Epuka kukejeli dini ya mtu🙏

Maajabu ya dini ni kuwa karibia kila aliyepo kwenye dini fulani huamini kuwa dini yake ndiyo bora kuliko zingine.

Ni busara kuheshimu dini za wengine hata kama hukubaliana nao. Naamini kufanya hivyo ni ishara kuwa "umekomaa" katika fikra.
 
Ule mwezi biashara inadoda sana. Sana yaani.
Inawezekana ni kwa sababu zifuatazo:
1. Wakati wa mfungo inawezekana baadhi ya Wakristo ambao ni walaji nao hujumuika na marafiki zao wa Kiislamu kufunga.

2. Inawezekana wakati wa mfungo baadhi ya Wakristo hukwepa kula Mchana kwa kuhofia kuwakwaza waliofunga
 
Kuheshimu imani ya mtu, hasa katika nchi isiyo na dini, ni suala nyeti sana. Ndiyo maana Watanzania wengi wanapotaka kufanya sherehe, kama si Waislamu, huhakikisha kuwa mchinjaji wa nyama itakayotumika ni Muislamu.

Lakini itakuwaje ikiwa wewe si Muislamu na ukatembelewa ghafla na rafiki Muislamu wakati unamla kuku uliyemchinja mwenyewe?

1. Utamkaribisha kujumuika nawe pamoja na kuwa unajua ulichinja bila kuzingatia imani ya Kiislamu?

2. Utamjulisha ukweli kuwa ulimchinja wewe mwenyewe ili aamue mwenyewe?

3. Utamwambia asubirie umwandalie cha kwake?

Upi utakuwa uamuzi wa busara?
kulen huku ana angalia
 
Yaani unaenda doea kwa watu na vifungu vya masharti? Yaani usichange hata chumvi upeleke masharti? Tumbo ni tumbo tu, haina cha muislam wala cha mbudha...
Ukienda kula pasi na kulipia, usiende na masharti
 
Chakula cha jioni! Rafiki yangu alini karibisha.. Shemeji yangu akaona Chumchang kaja, wachinje kuku, Na sababu ni Muislam na wana beki tatu Muislam basi wakampa jukumu la kuchinja😁
Nika piga honi, ajabu beki tati aliwahi kuja kufungua geti na kwa alaka akaniambia kuku utakae mkuta yeye ndio kachinja😂
Kiufupi nilikiwa chips na mayai.. Matunda nika shushia na juice ya miwa..
Jibu lako.. Sio sahihi, tueshimu imani za watu..
 
Back
Top Bottom