Makala za Tanzania Daima ni mwiba kwa JK

katumbwalala

Member
Jan 17, 2013
27
20
Paschally Mayela

RAIS wangu, jengo la ghorofa 16 limeanguka lakini serikali bado imesimama. Ni kipi kianguke kitoshe serikali kuanguka?Nyakati hizi zetu kusema serikali ianguke wenye visebusebu na waishiwa hawakawii kuwaza uchochezi.Mawazo yao yote ni uasi. Ndivyo walivyo wana wa shetani, kuwaza uovu kila siku!Ukiishiwa hoja unatafuta neno lolote unalodhani litakusaidia kutimiza uovu wako.

Hoja hii ndiyo sababu iliyomfanya ndugu yangu Dk. Harrison Mwakyembe katika ripoti yake ya Richmond kukwepa neno kuanguka akasema, "serikali ingeporomoka yote." Leo mimi nasema kuanguka serikali sijui itakuwaje!

Lakini wote tunakumbuka vema baada ya Waziri Mkuu Edward Lowassa kujiuzulu, serikali ilianguka yote akabaki Rais Kikwete na makamu wake Dk. Ali Mohamed Shein.

Hiki ndicho ninachokiongea hapa. Wala sichelei kutangulizwa kwenda mbinguni kwa Baba maana huko ndiko yaliko makao yangu ya milele! Huko nitamwona Eliya na Yakobo. Nitawaona na wazazi wangu wapendwa, walioniacha katika ulimwengu huu wa mateso, naam huko nitawakuta na marafiki zangu walionitangulia. Ole wao wautesao mwili wa nyama na kuiacha roho ya Mungu.

Rais wangu, nakumbuka vema jinsi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alivyopata shida kulinadi vema jina la chama kipya kilichotokana na muungano wa vyama viwili; TANU na Afro Shiraz Party (ASP).

Enzi hizo ilikuwa sawa na mwiko kutamka neno mapinduzi. Neno mapinduzi lilibeba maana ya uhaini. Uchochezi. Kuchochea watu kuiasi serikali yao.

Mwalimu alifundisha hadi Watanzania wakafundishika. Leo neno mapinduzi halina uasi wowote na wala halimtishi mtu. Ninaposema serikali ianguke sichochei chochote wala simchochei yeyote!

Rais wangu simama useme nani achinje. Nchi inaangukia kwenye vurugu za kumwaga damu, viongozi wa serikali wote wamekuwa na vigugumizi. Baba si umtaje mwenye haki ya kuchinja katika nchi hii.

Kwanini ndimi zenu zigandamane na mataya yenu nanyi mshindwe kusema nani achinje? Watoto wanagombania kisu baba uko kimya! Ah! Baba, ubaba haui hivyo. Kwani sheria za nchi si ziko wazi? Katiba inasemaje? Duniani kote nchi huongozwa kwa mujibu wa sheria. Ububu huu kwetu unakujaje?

Mazoea ya kuchinja yapo tokea uhuru zaidi ya miaka 50 iliyopita, lakini hayajawahi zua zogo kama hivi sasa. Kwa muda wote huo hizi dini zilikuwapo.

Hivyo si sahihi kusema mzozo wa nani achinje ni wa kidini. Ni zogo lililoanzishwa na wahuni wachache baada ya kubaini udhaifu mkubwa katika uongozi uliopo.

Kuchinja ni kuua. Tangu lini kuua kulikuwa dini ya mtu? Kiongozi anayetaka viongozi wa dini ndio wakutane kutatua mzozo huu ni mfinyu wa fikra kwa sababu huu si mzozo wa kidini.

Anaonyesha jinsi ambavyo hana uwezo wa kuongoza. Simfagilii mtu, lakini kwa uongozi ule wa Augostine Lyatonga Mrema huu usingekuwa mgogoro.

Haki ya mtu yeyote au kikundi chochote cha watu katika nchi iliyostaarabika lazima itambuliwe na ilindwe na sheria za nchi na
katiba ya nchi.

Yeyote au kikundi chochote kinachodai kuwa na haki ya kuwa na kitu fulani au haki ya kutenda tendo lolote ambalo halitambuliwi na sheria za nchi, hao ni wavunjifu wa amani. Yapasa waadhibiwe kwa mujibu wa sheria.

Majambazi hudhani ni haki yao kuwapora wengine. Makondakta nao wanadhani ni haki yao kupandisha nauli na kukatisha ‘ruti'. Hizi ni fujo, hizi ni vurugu.

Mzozo huu wa nani achinje si mzozo wa kidini. Mwenye wajibu wa kukomesha na kudhibiti fujo na vurugu katika nchi ni serikali, siyo viongozi wa dini. Rais akiwa kiongozi mkuu lazima alielewe hili.

Inapotokea viongozi wa nchi na hasa Rais wa nchi kuwatupia jukumu hili watu wengine, hata kama watu hao ni viongozi wa dini wajue kuwa wanajivua stahili yao ya kuwa viongozi. Hawatufai!

Nchi inapokuwa na viongozi wa aina hiyo inakuwa katika mkosi mkubwa. Wananchi hawana sababu ya kutafuta mchawi. Wawalazimishe viongozi waliopo kuirejesha amani waliyoipoteza wenyewe!

Rais wangu, kwa imani yangu mimi ni mkatoliki. Nyama hii kachinja nani haiwezi kuwa hoja yenye tija kwangu. Achinje Mbudha, Mhindi, Muislamu au Mpagani, nitakula.

Hata ikitokea shetani akachinja kwa mujibu wa taratibu kama zilivyofafanuliwa na Taasisi ya Chakula na Dawa (TFDA) nitakula bila kuharibu imani yangu. Kuna ubaya gani? Kwanza tumeambiwa na Kristo Yesu mwenyewe kuwa "kimwingiacho mtu hakiwezi kumtia najisi bali kimtokacho."

Muislamu kula nyama ambayo haijachinjwa na Mwislamu kwa imani ya Kiislamu ni kula haramu. Hivyo watu wa dini zingine na wale wasio na dini kutaka kuwalazimisha Waislamu kula haramu ni kuleta fujo katika nchi. Serikali ina wajibu wa kuwadhibiti waleta fujo hao.

Kama kuchinja ni ibada kufanya ibada kila mtu anajua. Ukimaliza ibada yako mambo mengine yote pamoja na malipo unamwachia Mungu. Ndiye mlipaji.

Kuchinja kwa masharti ya kulipwa miguu au shingo ya mnyama uliyemchinja na fedha juu hakuwezi kuwa ibada hata siku moja. Hiyo sasa ni biashara na ni ajira kama zingine. Wanaotaka kuwalazimisha wengine wawaajiri au wawafanyishe hiyo biashara kwa nguvu hao ni waleta fujo katika nchi. Serikali ina wajibu wa kuwadhibiti wakorofi hao.

Rais wangu, kiongozi anayetaka nchi iendeshwe kwa mujibu wa tamaduni na sio kwa mujibu wa sheria ni muishiwa. Amefilisika kiuongozi.

Zamani kule kwetu watu walikuwa na utamaduni wa kujisaidia porini. Kama viongozi waliokuja na kutukuta na utamaduni huo wangesema kwakuwa ni utamaduni tuliouzoea basi tuendelee nao, hadi leo watu wa kwetu wangekuwa wanajisaidia porini. Lakini walituambia tuchimbe vyoo na tuvitumie. Leo kwetu watu wamestarabika.

Najua katika ibada kuna sadaka. Hata kanisani kwetu padre hutueleza umuhimu wa kutoa sadaka ili Ibada ziendelee.Lakini sijawahi kumsikia Padre kanisani akisema leo humu ndani hatoki mtu hadi kieleweke, kila mtu lazima atoe sadaka.

Waziri Mkuu alikwenda Geita. Watu wamemuua mchungaji na kujeruhiana vibaya sababu ya nani achinje. Akawaambia kwa ufasaha kabisa kuwa sheria za nchi hii hata na katiba ya nchi, hakuna mahali popote zinapompa mtu yeyote au kikundi chochote haki ya kuchinja. Kwa mshangao wa wengi akasema kwa kuwa ni utamaduni basi waendelee nao. Ha! Ha! Ha! Liwe na liwalo, huu ndiyo mfano mzuri wa uongozi mbovu!

Watu waendelee kujisaidia porini! Kisa kudumisha utamaduni, du! Ni nchi ya aina gani hii inayotakiwa kuendeshwa kwa mazoea? Sheria basi zifutwe!

Rais wangu ulipohutubu ulisema ulisomewa itikafu katika misikiti mitatu ili ufe. Kwa hakika hii ni habari mbaya kabisa. Maamuma wote hawajui kuwa kifo cha mwanadamu hupangwa na Mwenyezi Mungu. Nakuombea afya njema Mwenyezi Mungu akujaalie maisha marefu.

Baba umebarikiwa kwa kuwa na ulinzi imara. Bahati hiyo wengine kama Stephen Ulimboka na Absalom Kibanda hawakuwa nayo. Unadhani bila huo ulinzi nini kingekutokea?

Rais wewe ni rais wa sisi wote. Mtu au kikundi cha watu kutaka kuondoa uhai wa mkuu wetu wa nchi ni jambo zito na la kuogopesha.

Inashangaza kuona vyombo vinavyohusika na usalama wa rais vimekaa kimya na kumlazimu rais kwenda kulalamika mwenyewe hadharani. Iweje kuwe na ushahidi wa watu kupanga njama za kumuua rais halafu waachwe watembee bila sheria kuchukuliwa dhidi yao? Hali hii inazua shaka!

Wananchi wameambiwa kuwa unyama na mateso waliyofanyiwa Ulimboka na Kibanda ni wa kitaalamu. Serikali huwasomesha utaalamu maalumu wafanyakazi wake walioko katika taasisi zake nyeti kwa ajili ya kazi nyeti. Ndiyo kusema utaalamu huu ni wa wafanyakazi fulani wa serikali peke yao.

Inapotokea kuwa katika kijiji kizima wewe tu ndiye unayefuga ng'ombe basi mazao ya wanakijiji yatakapoliwa na ng'ombe lazima utakamatwa wewe. Kumbe wamkamate nani? Inawezekana kabisa kuwa ng'ombe wale hawakutumwa na mwenye ng'ombe wakale mazao ya watu, lakini huwezi kuwakana ng'ombe wako.

Serikali kushindwa kuwakamata wahalifu wa matukio haya kunawaongezea wananchi shaka na kuwaondolea imani kwa serikali yao.
Ulisema Waislamu wanakulalamikia kuwa unawabeba Wakristo na kwamba Wakristo wanakulalamikia kuwa unawabeba Waislamu. Hapa Waislamu na Wakristo wanakubaliana katika jambo moja kuwa unabeba.

Kama wote wanasema unabeba basi baba unabeba kweli, acha! Kiongozi bora hatakiwi kumbeba yeyote. Tujitathimini katika hilo kwa maana sisi sasa ndiyo tunaonekana kuwa chanzo na kiini hasa cha vurugu zote hizi.

Tumekwishaivuruga nchi kiasi cha kutosha, na sasa machafuko makubwa yanatunyemelea.Kubeba si lazima unyanyue. Wanamichezo wanaposema refarii amepeta wanakiri kuwa refarii ameibeba timu pinzani.Wanaoleta vurugu nchini kama hawa wanaotaka kumuua rais wangu kuwanyamazia ni kuwabeba.Tunakokwenda bado ni mbali na kwa mwendo huu hatufiki.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitakiwa awe ni kiongozi wa msaada mkubwa kwa rais wangu, lakini kwa jinsi mambo yanavyokwenda ni kinyume na matarajio ya wengi. Kama kuna watu waliingia kazi katika mazingira magumu kabisa tangu uhuru wetu ni Salim Ahmed Salim aliyemrithi Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine na Mizengo Peter Kayanza Pinda aliyemrithi Waziri Mkuu Edward Ngoyayi Lowassa. Watangulizi wao katika utendaji kazi, ingekuwa ni katika uovu wangeitwa maharamia.

Walikuwa ni wachakarikaji wa kweli na waliokuwa mahiri katika kutenda. Watu wafuatiliaji wasiokuwa na shaka ambao hawakuwa na ukakasi katika kutoa uamuzi.

Salim alipoingia alikuwa muwazi. Alikiri kuwa Sokoine alikuwa mchapakazi mahiri na kipenzi cha watu. Akawaasa Watanzania kuwa yeye kama walivyo wanadamu wengine hawezi kumuenea mwanadamu mwingine. Hata hivyo kazi aliyoifanya katika kipindi chake haikuacha shaka yoyote.

Rais wangu, kuanguka ghorofa kumemweka waziri mkuu wetu katika mashaka mazito. Wanaosema ajiuzulu wana nia ya kumsaidia na kurudisha heshima iliyopotea ya serikali kuwajibika. Ripoti ambayo sasa inaitwa ripoti ya Lowassa haijamwachia kitu cha kujisitiri.
Mwanaume ukivukwa na nguo busara ni kuchutama! Ili kulinda hadhi ya ofisi ya Waziri Mkuu na hadhi yake mwenyewe, afuate nyayo za mtangulizi wake, aachie ngazi.

Tume ngapi zimeundwa katika nchi hii, lakini majibu yako wapi? Hata kuanguka kwa lile ghorofa imeundwa tume ya uchunguzi!
Kweli kwa Watanzania msemo wa wajinga ndio waliwao unapata utimilifu.

Kama Waziri Pinda asingeikalia ripoti ya Lowassa tangu mwaka 2008 leo hii jengo lile lisingeanguka kwa sababu au lisingejengwa au lingejengwa kwa viwango vinavyotakiwa!

Inachekesha lakini kwa maumivu kusikia kuwa eti kuna mtu anataka uchunguzi wa kuanguka ghorofa lile uharakishwe. Ni uchunguzi upi huo? Mbona ripoti ya Lowassa iko wazi hata kwa mbumbumbu kuielewa?

Ukisikia hivyo jua hivyo ndivyo vinaitwa katika Tanzania siasa. Hapo hakuna kitakachotoka. Nitaendelea kusema kuwa siasa na ujinga ni vitu viwili tofauti. Vitabaki kuwa tofauti hata kama wajinga au baadhi ya wanasiasa wa Tanzania wangependa kuviunganisha. Nani hajui kuwa hao wenye maghorofa uaji ndio wachangiaji wa fedha nyingi kwenye kampeni? Uchunguzi gani utafanywa tena eti kwa kuharakishwa dhidi yao?

Tunapomtafuta rais ajaye Watanzania tujifunze kwa yaliyopo. Rais ajaye awe ni mtu aliyezoea hela! Mtu ambaye hataleweshwa na uwingi wa hela. Mtu ambaye hata akichukua hela kutoka kwa matajiri bado awe na uwezo wa kuwapa amri haohao matajiri bila kuwachekea. Tumpate rais ambaye hawezi kufungwa mdomo na wenye hela kwa sababu yeye mwenyewe anazo!

Waziri Mkuu wetu ana ubavu wa kuifanyia kazi ripoti ya Lowassa ambayo inaainisha wazi kuwa wajenzi wa hayo maghorofa uaji ni watu wenye hela nyingi wakati yeye alijitambulisha kwetu kuwa ametoka katika familia ya mkulima maskini? Je, hadi leo bado ni maskini?

Kama ni kweli imeundwa tume ya uchunguzi kwa kuanguka lile ghorofa viongozi wetu wameamua kuwapiga Watanzania kama mtu anayempiga nyani bila kumtazama usoni.

Hivi kuna mjinga gani ambaye hajui kwanini lile ghorofa limeanguka hadi iundwe tume? Tume imeundwa ili kama wasemavyo mtaani ‘kupoteza soo.' Wenye maghorofa na wanaounda tume ya uchunguzi ni watu walewale!

Rais wangu waambie Watanzania kinachozuia utekelezwaji wa ripoti ya Lowassa ni nini? Kati ya maghorofa 505 yaliyokaguliwa, 147 yalikutwa hayana nyaraka za ujenzi. 81 yalikutwa yamekiuka masharti ya ujenzi huku 22 wenyewe hawakupatikana.

Bila kuifanyia kazi ripoti ya Lowassa Watanzania wategemee vifo vingi zaidi vitakavyotokana na maghorofa mengi zaidi kuanguka.
Kama Waziri Mkuu wetu atajisikia uchovu kung'atuka, basi Bunge limsaidie.

Rais sema, ni kipi kianguke kitoshe kuanguka kwa serikali?
 
mmmh maneno makali sana, natamani muda wa uraisi ingekuwa miaka mitatu maana serikali yetu ya kipindi hiki imezidi kulalamika
 
Mkuu, umeniwahi, ilikua kidogo niibandike hii na wengine waipitie, mzee ametoa somo la kutosha kabisa kwa Pinda, Kikwete, Waislam na Wakristo bila kumsahau hata Wassira though hajamtaja kwenye makala lakini nadhani ndiye muhuni aliyesababisha yote hayo ya kuchinja. Big up mzee Pascal Mayega, a.t.a mwalimu mkuu wa watu.
 
hiyo makala ni upepo tu utapita,kwanza fast jet hana muda wa kuisoma anapanga trip za majuu
 
Hivi hata kwenye ukweli kama huu kuna watu bado wanaleta ushabiki ndani yake? Hivi ni lini kwenu nyie "watu" mtakuja kubaliana na ukweli unapoandikwa humu? Au mnapinga yaliyomema kwa faida ya nani? Hivi huku kupinga mambo yaliyowazi, kweli na yamsingi kama haya si ni upumbavu? au tuuiteje?

Hizi njaa, ushabiki wa kipuuzi na mambo ya kufata mkumbo ndo yanawafanya watawala (si-viongozi) kuendelea kututendea kama wanavyofanya sasa. Nakumbuka tulionywa mapema.."..kuichagua tena CCM, ni janga la Kitaifa.." hili sasa kila mwenye akili timamu (sio wale wapumbavu) analiona.

Ndugu zanguni tubadilikeni tuikomboe Nchi yetu, unafiki huu tuufanyao utaendelea kuwaneemesha hao hao "watawala" dhalimu na nyie washabiki na familia zenu mtaendelea kuangukiwa na magorofa!!!!
 
Wow!!

Hii imetulia. JK na viongozi wake hawana masikio wala macho. Yes, sitoshangaa wapambe wake kusema kwamba ni uchochezi.

Kitu ambacho kinanifurahisha zaidi ni kwamba, Watanzania wako tayari kujitoa muhanga. Uvumilivu umetushinda na huku kuishi kwa mazoea ni fikra finyu. Hii ni ishara mbaya kwa uongozi na mafisadi kwa ujumla. Karibu wataanza kupopolewa!
 
Kuunda tume ni kuficha udhaifu wa serikali. Serikali hufanya kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni. Hivi kujua mtumishi wa umma alizingatia au hakuzingatia sheria kunahitaji tume? Tume hizi zinaendelea kutufilisi. Huenda hii ni njia mojawapo ya kupeana /kuiba fedha za srikali.
Fedha za serikali zikiibiwa tume zinaundwa. Nchi ya Tume. Siku zote ukiona serikali inaunda tume ujue viongozi hawataki lawama au wanatoa hadidu za reja ambazo huficha uovu. Hata matokeo ya tume hizo inabaki siri. Ovyo kabisa.
 
Huo ndio ukweli. Ebu angalia badala ya Rais kuwawajibisha waliosababisha maafa anawapongeza waokoaji ambopo
watu 36 wamepoteza maisha. Ukisataajabu ya Musa utayaona ya ..................
 
Kuunda tume ni kuficha udhaifu wa serikali. Serikali hufanya kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni. Hivi kujua mtumishi wa umma alizingatia au hakuzingatia sheria kunahitaji tume? Tume hizi zinaendelea kutufilisi. Huenda hii ni njia mojawapo ya kupeana /kuiba fedha za srikali.
Fedha za serikali zikiibiwa tume zinaundwa. Nchi ya Tume. Siku zote ukiona serikali inaunda tume ujue viongozi hawataki lawama au wanatoa hadidu za reja ambazo huficha uovu. Hata matokeo ya tume hizo inabaki siri. Ovyo kabisa.

Binafsi niliipenda kauli ya Mama Tibaijuka, pale kwenye eneo la tukio alisema hivi, nanukuu..." hilo jengo pacha nilazima livunjwe mara moja, hakuna cha tume, kamati wala kikao nilazima livunjwe soon.."
Huyu kathubutu na asipokwamishwa kweli litavunjwa. Ukiona zinaanza mara kamati, mara vikao basi ujue kuna maagizo toka kwa Mkuu yakumkwamisha!!!
 
Paschally Mayela

Inashangaza kuona vyombo vinavyohusika na usalama wa rais vimekaa kimya na kumlazimu rais kwenda kulalamika mwenyewe hadharani. Iweje kuwe na ushahidi wa watu kupanga njama za kumuua rais halafu waachwe watembee bila sheria kuchukuliwa dhidi yao? Hali hii inazua shaka!?

Hahaha sasa njama za wanamaombi mlitaka Usalama wa Taifa wamkamate Sheikh eti kisa kamuombea dua mbaya JK?

Au wamkamate mganga wa kienyeji kisa anamroga JK? halafu mahakamani ushahidi nini Quran? hahaha

Haya magazeti ya udaku mimi huwa sisomi
 
Paschally Mayela
Rais wangu simama useme nani achinje. Nchi inaangukia kwenye vurugu za kumwaga damu, viongozi wa serikali wote wamekuwa na vigugumizi. Baba si umtaje mwenye haki ya kuchinja katika nchi hii.

Kwanini ndimi zenu zigandamane na mataya yenu nanyi mshindwe kusema nani achinje? Watoto wanagombania kisu baba uko kimya! Ah! Baba, ubaba haui hivyo. Kwani sheria za nchi si ziko wazi? Katiba inasemaje? Duniani kote nchi huongozwa kwa mujibu wa sheria. Ububu huu kwetu unakujaje?

Mazoea ya kuchinja yapo tokea uhuru zaidi ya miaka 50 iliyopita, lakini hayajawahi zua zogo kama hivi sasa. Kwa muda wote huo hizi dini zilikuwapo.

Hivyo si sahihi kusema mzozo wa nani achinje ni wa kidini. Ni zogo lililoanzishwa na wahuni wachache baada ya kubaini udhaifu mkubwa katika uongozi uliopo.

Kuchinja ni kuua. Tangu lini kuua kulikuwa dini ya mtu? Kiongozi anayetaka viongozi wa dini ndio wakutane kutatua mzozo huu ni mfinyu wa fikra kwa sababu huu si mzozo wa kidini.

Anaonyesha jinsi ambavyo hana uwezo wa kuongoza. Simfagilii mtu, lakini kwa uongozi ule wa Augostine Lyatonga Mrema huu usingekuwa mgogoro.

Haki ya mtu yeyote au kikundi chochote cha watu katika nchi iliyostaarabika lazima itambuliwe na ilindwe na sheria za nchi na katiba ya nchi.

Yeyote au kikundi chochote kinachodai kuwa na haki ya kuwa na kitu fulani au haki ya kutenda tendo lolote ambalo halitambuliwi na sheria za nchi, hao ni wavunjifu wa amani. Yapasa waadhibiwe kwa mujibu wa sheria.

Majambazi hudhani ni haki yao kuwapora wengine. Makondakta nao wanadhani ni haki yao kupandisha nauli na kukatisha ‘ruti'. Hizi ni fujo, hizi ni vurugu.

Mzozo huu wa nani achinje si mzozo wa kidini. Mwenye wajibu wa kukomesha na kudhibiti fujo na vurugu katika nchi ni serikali, siyo viongozi wa dini. Rais akiwa kiongozi mkuu lazima alielewe hili.

Inapotokea viongozi wa nchi na hasa Rais wa nchi kuwatupia jukumu hili watu wengine, hata kama watu hao ni viongozi wa dini wajue kuwa wanajivua stahili yao ya kuwa viongozi. Hawatufai!

Nchi inapokuwa na viongozi wa aina hiyo inakuwa katika mkosi mkubwa. Wananchi hawana sababu ya kutafuta mchawi. Wawalazimishe viongozi waliopo kuirejesha amani waliyoipoteza wenyewe!

Rais wangu, kwa imani yangu mimi ni mkatoliki. Nyama hii kachinja nani haiwezi kuwa hoja yenye tija kwangu. Achinje Mbudha, Mhindi, Muislamu au Mpagani, nitakula.

Hata ikitokea shetani akachinja kwa mujibu wa taratibu kama zilivyofafanuliwa na Taasisi ya Chakula na Dawa (TFDA) nitakula bila kuharibu imani yangu. Kuna ubaya gani? Kwanza tumeambiwa na Kristo Yesu mwenyewe kuwa "kimwingiacho mtu hakiwezi kumtia najisi bali kimtokacho."

Muislamu kula nyama ambayo haijachinjwa na Mwislamu kwa imani ya Kiislamu ni kula haramu. Hivyo watu wa dini zingine na wale wasio na dini kutaka kuwalazimisha Waislamu kula haramu ni kuleta fujo katika nchi. Serikali ina wajibu wa kuwadhibiti waleta fujo hao.

Kama kuchinja ni ibada kufanya ibada kila mtu anajua. Ukimaliza ibada yako mambo mengine yote pamoja na malipo unamwachia Mungu. Ndiye mlipaji.

Kuchinja kwa masharti ya kulipwa miguu au shingo ya mnyama uliyemchinja na fedha juu hakuwezi kuwa ibada hata siku moja. Hiyo sasa ni biashara na ni ajira kama zingine.

Wanaotaka kuwalazimisha wengine wawaajiri au wawafanyishe hiyo biashara kwa nguvu hao ni waleta fujo katika nchi.

Serikali ina wajibu wa kuwadhibiti wakorofi hao.
Rais wangu, kiongozi anayetaka nchi iendeshwe kwa mujibu wa tamaduni na sio kwa mujibu wa sheria ni muishiwa. Amefilisika kiuongozi.

Zamani kule kwetu watu walikuwa na utamaduni wa kujisaidia porini. Kama viongozi waliokuja na kutukuta na utamaduni huo wangesema kwakuwa ni utamaduni tuliouzoea basi tuendelee nao, hadi leo watu wa kwetu wangekuwa wanajisaidia porini. Lakini walituambia tuchimbe vyoo na tuvitumie. Leo kwetu watu wamestarabika.

Najua katika ibada kuna sadaka. Hata kanisani kwetu padre hutueleza umuhimu wa kutoa sadaka ili Ibada ziendelee.
Lakini sijawahi kumsikia Padre kanisani akisema leo humu ndani hatoki mtu hadi kieleweke, kila mtu lazima atoe sadaka.
Waziri Mkuu alikwenda Geita. Watu wamemuua mchungaji na kujeruhiana vibaya sababu ya nani achinje.

Akawaambia kwa ufasaha kabisa kuwa sheria za nchi hii hata na katiba ya nchi, hakuna mahali popote zinapompa mtu yeyote au kikundi chochote haki ya kuchinja. Kwa mshangao wa wengi akasema kwa kuwa ni utamaduni basi waendelee nao. Ha! Ha! Ha! Liwe na liwalo, huu ndiyo mfano mzuri wa uongozi mbovu!

Watu waendelee kujisaidia porini! Kisa kudumisha utamaduni, du! Ni nchi ya aina gani hii inayotakiwa kuendeshwa kwa mazoea? Sheria basi zifutwe!

Rais wangu ulipohutubu ulisema ulisomewa itikafu katika misikiti mitatu ili ufe. Kwa hakika hii ni habari mbaya kabisa. Maamuma wote hawajui kuwa kifo cha mwanadamu hupangwa na Mwenyezi Mungu. Nakuombea afya njema Mwenyezi Mungu akujaalie maisha marefu.

Haya ni maneno yanayoonesha BUSARA kubwa saana ya Mzee mayega. Hakuna sababu ya kutetea ubabe wa kundi moja.
 
Back
Top Bottom