Mizani ya vigwaza ni jipu jingine kipindi cha Mvua

Norshad

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
5,128
12,216
Habari wakuu,

Katika kipindi hichi cha mvua za El nino, kumekuwepo na muendelezo wa tabia mbaya inayoendelezwa pale mizani ya vigwaza, ambayo imekuwa ikisababisha foleni kubwa ya magari ya mizigo na mabasi yaendayo mikoani na kuwapa wakati mgumu mno askari wa usalama barabarani kuongoza magari hasa kipindi cha asubuhi.

Iko hivi.

Kwa madereva wa maroli, unaweza toka bandarini ukiwa umepima vizuri na mzani ukasoma sahihi kabisa, lakini ukifika vigwaza figisu zitaanza, utaambiwa gari imezidisha mzigo, utarudishwa upime upya, ama ukapange mzigo, mchezo huu umekuwa ukijirudia sana kipindi cha mvua, tunajua kama huwa wanaichezea mizani, tunaomba mamlaka husika waliangalie hili sababu limekuwa likizorotesha shughuli za kijamii, kibiashhara na limekuwa ni kero kwa abiria hasa wanaosafiri mikoa ya mbali
 
Sheria imekaaje mtu binafsi kuweka mzani hapo mlandizi kuverify kama mzigo umekaa poa kabla ya kufika hapo vigwaza.... Hata akicharge 5000 per vehicle, seem to be a good business.
Umeshaambiwa Wafanyakazi wa mizani Wana bills za kulipa. So Lazima uwaachie Chochote ili uwe salama
 
Back
Top Bottom