Ni rasmi sasa VODA inafukuza wateja

Ha ha ha Baba lao tunatesa tu. Airtel ndo kiboko yenu. Vifurushi bei nzuri. Ukimpigia mtu kama hapatikan ni kweli hapatikani na sio hao Voda+Tigo
 
Nami sasa nahamia airtel, nimechoshwa, nimechoka, nimechoshwa sana na hii voda japo nimedumu nayo zaidi ya miaka 10. Mambo gani hayo mnatufanyia wateja wenu hata bila kutujulisha? Nadhan voda wameshagundua namna ambavyo mauzo yamebadilika tangu waleta hayo matapishi ya vifurushi.
 
Voda lazima yawe majizi maana jizi kubwa Rostam Aziz linamiliki share ya 60%,na mimi nawalia denge voda muda si mrefu nawapiga chini,nyambafu wamenitesa sana,nawadai makato hewa ya sh 15,000 bado sijapewa hata cent,voda haifai,wezi tu.
 
Wengine Voda tulikwisha ihama zamani .
Takriban kampuni kadhaa za simu hapa Tz zina ubabaishaji lakini Voda inaongoza.
 
HAWAFAI VODACOM hawafai
jana tu nimeingiza vocha nilipojiunga wakaniambia

  • salio lako halitoshi
  • kuulizia salio kweli wameshakata na sababu siijui
 
Hawa voda ni wezi kabisa.hawafai hata kidogo.nilishanunua BB ya wiki sikuipata siku tatu nzima!mwisho nikaamua kuweka chip ya tigo.halafu customer care staff wana kauli mbaya kwa wateja.
 
Jamani Musilaumu! Tupo tunaandaa vifurushi vya kufungia mwaka,mutafurahi nyinyi! kuwa na subira. VODACOM KAZI NI KWAKO!

Kama ni mfanyakazi wa voda wafikishie ujumbe wahusika wakuu. Si ajabu watakuwa wanakunywa juice kwa mrija wakidhani mambo yako sawa kumbe ...
 
Nili Post "KUTOKA VODA HADI AIRTEL" wakaibania. Bonyeza
*149*99# AIRTEL
*149*01# VODA
CHAGUA MITANDAO YOTE. Uone tofauti
 
hata hivyo voda wanajiskia sana kwa ndo wenye wateja wengi kuliko mitandao mengine. mimi wamenoboa hadi nimechoma line...
 
mkuu pengine umeshindwa kuvielewa hivyo vifurushi na umejikuta una potosha alaf tusi sahau hii ni biashara.

Walicho fanya voda ni kufanya mabadiliko kidogo kwenye muda wa kupiga mitandao mingine ukilinganisha na voda -voda.

Mfano vifurushi vya masaa24

tsh400=900sec(voda-voda)+45sec(mitandao mingine)+100sms+50mb.

Tsh500=1200sec(voda-voda)+50sec(mitandao yote)+250+100mb

tsh1000=3000sec(voda-voda)+60sec(mitandao mingine)+300+100mb

ukijaribu kuangalia vifurishi hivi utagundua kuwa sec zilizokuwa zina tumika mitandao yote kwa sasa zina tumika voda-voda na bado wametoa sekunde kwa mitandao mingine.

Si kweli kuwa hupigi mitandao mingine bali muda wa kupiga umepunguzwa, na hii ni biashara.

Msemaji wa kampuni?
 
Voda majanga hata network ni uchwara sn. Njoo maeneo ya mabibo hostel uone kama utaweza hata kupiga simu yani ni kichefuchefu. Modem ndio ziro kbs na hakuna anaejali.daah
 
Back
Top Bottom