Mimi nimeamua kuhamia TIGO. Last week Jumamosi TAREHE 28/6/2014 nilinunua kifurushi cha Internet unlimited cha wiki Shs 6000. Wakakata hela lakini hawakuwezesha mtandao. Nikapiga 100 customer care nikajibiwa muda wangu wa kupiga huko umeisha eti nisubiri mpaka August au nilipie Shs 100 niongee nao. Nikajaribu hii option ya pili. Kila nikilipia inajirudia kudai nilipie. Mchezo huu uliendelea mpaka nika-give up. Hata hivyo kwa vile nilikuwa nahitaji sana kutuma e-mail niliamua ninunue unlimited ya saa 24 nikakatwa Tshs 1000. Hakuna kitu. Nikarudia tena, Hakuna kitu. Nikaachana nao. Eti Jumatatu mchana ndio wananitumia sms unlimited ya saa 24 imewezeshwa. Hapo hapo napokea message nyingine kuwa imeisha. NIMEWAAGA, SITAKI KUWASIKIA NA HATA KUWAONA. KWA HIYO SITADAI PESA WALIZONIIBIA.