Ni pombe gani hutakuja kuisahau maishani mwako?

pombe imenifanyia visa sana ukinywa pombe nyingi sehemu ya vibe unaweza kufanya vioja sana
 
Pole sana mkuu umenikumbusha habari ya valeur
nilikuwa na mwanangu mmoja mungu amlaze pema alikuwa akija likizo ni mwendo wa valeur vile vichupa vidogo siku tupo wanne
tukaamua kujirudishia shukrani na valeur vitoto box zima mama muuza akasema zimeisha tukaamia nyingine ya pakiti ilikuwa inaitwa samson
baada ya pakiti 3 nilifika home fresh wenge la taa likanichanganya nikaanza kurudisha chenji ghafla
nilitoka nje nikalala shambani kutoka saa nne mpaka majogoo
na mara ya mwisho kunywa hicho kinywaji na kupaki bus kizembe
Noma Sana aisee!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nimejikuta nacheka mkuu kipindi cha ujana wangu na huyu manka tulikaa kama miez 5 tukazinguana akaondoka na kibendi nakuja kupata taarifa ngoma ina miez 3 na kitu siku namvalisha pete sikuamini asee nilifurah mno Nilipiga Magic Moment chupa 3 nikaja kuzinduka nipo hospitalini manka akanifichia siri home wakajua naumwa kumbe nilizima Magic Moment
 
Aisee.pombe ilimfanya vibaya rafiki yangu,tunakaribia kupiga pepa la mwisho kidato cha sita kule mkoani morogoro jamaa angu alipiga ulanzi akachanganya na gongo akapitiliza kabisa kunywa ,anarudi skuli usiku mnene mlango wa bwenini anauona mdogo,Mara anajaribu kuinama ili aingie ndani bwenini yan utafikiri mlango wa kuingilia bwenini ni kama mlango wa banda la kuku kumbe ni mlango mkubwa tu,basi jamaa alitukana bweni zima na kutapika koridoni na baraza za nje ya bweni zilijaa matapishi yake na kesho yake tulikuwa na pepa ngumu kumesa,kesho siku ya pepa alibaki analia tu kwenye exams room kila wakati anaomba abadilishiwe calculator...
Hahahaa!!!!matokeo vipii!!
 
Magaritha, pombe hii inaseviwa ikiwa na barafu, (ice), kwenye glasi iliyopakwa chumvi pembeni na kipande ChA limao. Hivyo unakunywa huku unaramba chumvi na limao. Glasi ya kwanza niliifurahia, yapili nikamwambia asiwe mabarabu maana yanapunguza Wingi WA kinywaji kwenye GLASI LAKINI MHUDUMU ALINISHANGAA lakini alitii maagizo yangu akanipa bila barafu ndani. Kwakweli sikujuwa kuwa kumbe Ile pombe ni kali SanA ikaniunguza mdomo na koo lote Hali yangu ilikuwa tete kidogo niondoke,
Mmhhh!
 
Mm siyo mnywaji wa mara kwa mara, ila siku nikisema naenda kunywa lazima mkimbie nyie.
Kuna siku niliingia boardroom sinza nimepiga chupa 2 za Hennessy zile size ya kati wanauza 1 elf60, nimekuja kustua kesho yake saa 2 usiku nipo home hoi bin taabani
Hahhahaaa jaman hennesy sio ya kwenda nayo kibabe hata kidg..niliwah kunywa glas 2 toka aaa5 mchana had saa8..lakini nilikua nimelewa siku2...yaan noma mnoo mno
 
Kuna siku nilienda kumtembelea jamaa yangu gheto kwake. Mida ya jioni akanitoa out mimi na washkaji wengine.

Binafsi sinywi pombe, nilipiga grand malt zangu nila wenge. Around saa mbili au tatu kasoro tukarudi gheto. Alipopanga, nyumba ina fensi.

Sasa tushaingia ndani, jamaa akafunga na geti kabisa. Dakika chache mbele kuna mtu akawa anagonga geti huku akiita na kuomba afunguliwe. Jamaa yangu akaanza kuwaka, yule ni nani anasumbua watu mida ile wakati yeye (jamaa yangu) alishaweka sheria, akiingia ndani, ambao mko nje mtafute pa kulala (hapo kumbuka nyumba sio yake, amepanga).

Kumbe bhana anabishana na mwenye nyumba . Yule faza house baada ya kuona maneno ya shombo yamezidi, akaamua kuondoka (alikuwa mfupi tena kibonge, asingeweza ruka ukuta).

Hiyo ndio ilikuwa mara ya mwisho jamaa yangu kuishi pale, japo kodi ilikuwa bado sana kuisha.

Hahahahhahaa mbavu zangu mm jaman .uwiii🤣🤣🤣🤣🤣😍
 
Nikiwa darasa la tatu, siku ya jumapili nimetoroka home kuingia kitaa ili nisiende kanisani. Nikaenda kukutana na masela wangu tukaenda nyumbani kwa mmoja wetu walikuwa wamepika pombe ya kienyeji. Basi tukagonga masalia weee...tukalewaaa, tukalala kwenye vivuli vya miti. Kuanzia asubuhi tukaamka jioni kabisa.😀

Kumbe huku natafutwa niende kanisani, narudi jioni nimechafuka balaa, nanuka pombe plus hangover. Nilipewa kipondo heavy weight😀😀😀😀

Sikuwahi kunywa baada ya hapo, sasa hivi ni mwendo mirinda nyeusi.
 
Kuna siku nilikuwa na hamu ya kuzimua kidogo, nikaingia baa...nikaagiza castle lite na nyagi ndogo ( kasichana) nikapiga, bia ikaisha nikaongeza bia mbili Tena ili kuimalizia konyagi.

Ilipoisha nikaanza kupiga lite za kutosha! Sijakaa sawa akaja rafiki yangu dokta akasema tuchukue mzinga mkubwa wa Valeur.

Tukauchukua, tukaanza kuupiga mpaka ukaisha, ebwana eeee.....!!! Nikaanza kutoka baani kwenda home saa nane usiku kwa mguu, kumbe geji inapanda**.

Nilipofika home badala ya kuingia ndani nilipitiliza kwenye fensi yenye miiba...nikawa nafosi kupita pale...yaani nilichomwa miiba balaa!

Nilichafuka huku naangukia miba..baadae sijui ikawaje nikaingia chumbani nikalala...

Kuamka asubuhi kila sehemu nimekwaruzwa Kama viwembe hivi..njaaa....halafu macho yanatoa machozi fulani hivi yanaumaa!

Nikapigia boda akaleta nyama nusu, maji makubwa ya baridiii, na Pepsi baridiii.

Nikaandaa supu..nikainywa mdogo mdogo.

Nilishinda nimo ndani tu, kumbe Kuna dada mmoja aliniona ile night navyofakamia ile fensi Kama mbogo.
Baada ya siku mbili baadae akaniuliza kumbe kaka unakunywa? Niliona aibu maana sikuwahi kuonekana nimekunywa!

Huo usiku nilkuwa full yaani yeyote akikaa mbele nilijiapiza anachezea mkono, sijui hayo mawazo yalitoka wapi. Nilipita sehemu walipo vibaka nawatafuta kwa kuwaita kabisa nikielekea home.

Sikujua nikuwa nalazimisha nivuke fensi niende wapi!

#Valeur haifai#

Hahahhaa na ww ulimix sana dah🤣🤣🤣
 
Kabisa iko hivyo.
Ile spirit inadhalilisha sana.
Mie Saint Anna huwa silewi...nikinywa nasikia kulala tu.
Mie huwa nachanganya Kvant na safari...hilo vibe lake si mchezo.
Nasaula tu popote.
Hahahahahahahhaa....nakufa mie kwa kicheko dah..madame bwan🤣🤣
 
Wanywaji wenzangu:

-Ulishagundua baada ya kutapika ni kama ulevi unaongezeka mara dufu na nertwork zinakata.

-Kuna wale hangover haiishagi yani mpaka ulale sanaaa...

-Ukiwa club kwenye mziki unakula gambe unajiona kam bado upo mzima na unacheza vizuri...Ukitoka sasa ukaenda penye utulivu au ukaenda gheto ndio unaanza kusikia kichwa kama kimefungwa mortar kinavyozunguka

-Wataalamu wa kukimbilia energy drink wakiona mambo yaananza kuwa sio.

-Wale ambao hatukumbukagi tuliingiaje ndani, unaamka mdomo mchunguuuu yaani huo mswaki unaotumia inabidi uutupe kabisa na kichwa nzitoo.

-Wale tunaoamini uchawi hauendagi kwa mla gambe .

-Wale ambao ukiamua kuvumilia siku tatu bila gambe koo linawasha.

-Wale ambao ukila gambe ndio unaona kuwa akili zipo sawa yaani confidence na kushusha mapoint .

- Tuliopatia kazi kwenye gambe.

Hivi ambao hawajawahi kula gambe maisha yakoje?
 
Aisee.pombe ilimfanya vibaya rafiki yangu,tunakaribia kupiga pepa la mwisho kidato cha sita kule mkoani morogoro jamaa angu alipiga ulanzi akachanganya na gongo akapitiliza kabisa kunywa ,anarudi skuli usiku mnene mlango wa bwenini anauona mdogo,Mara anajaribu kuinama ili aingie ndani bwenini yan utafikiri mlango wa kuingilia bwenini ni kama mlango wa banda la kuku kumbe ni mlango mkubwa tu,basi jamaa alitukana bweni zima na kutapika koridoni na baraza za nje ya bweni zilijaa matapishi yake na kesho yake tulikuwa na pepa ngumu kumesa,kesho siku ya pepa alibaki analia tu kwenye exams room kila wakati anaomba abadilishiwe calculator...
,,,Eti anaomba abadilishiwe calculator
 
🤣🤣🤣🤣huwa wambea na wanafiki
 
Aisee.pombe ilimfanya vibaya rafiki yangu,tunakaribia kupiga pepa la mwisho kidato cha sita kule mkoani morogoro jamaa angu alipiga ulanzi akachanganya na gongo akapitiliza kabisa kunywa ,anarudi skuli usiku mnene mlango wa bwenini anauona mdogo,Mara anajaribu kuinama ili aingie ndani bwenini yan utafikiri mlango wa kuingilia bwenini ni kama mlango wa banda la kuku kumbe ni mlango mkubwa tu,basi jamaa alitukana bweni zima na kutapika koridoni na baraza za nje ya bweni zilijaa matapishi yake na kesho yake tulikuwa na pepa ngumu kumesa,kesho siku ya pepa alibaki analia tu kwenye exams room kila wakati anaomba abadilishiwe calculator...

🤣🤣🤣🤣🤣🤣👐👐👐🙌🙌🙌
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom