Ni Tukio lipi hautalisahau maishani mwako ?

Utawala2025

JF-Expert Member
Oct 20, 2023
330
1,060
Habari.

Tukiwa Tumeanza mwaka 2024 naomba tushare visa vichache wana Jf.

Ebu tuambizane Tukio gani Hautakuja kulisahau maishani mwako.

Tuambie tujifunze na kuna kitu kinaweza kutujenga maishani?
 
_20240301_011742.JPG
 
Habari.

Tukiwa Tumeanza mwaka 2024 naomba tushare visa vichache wana Jf.

Ebu tuambizane Tukio gani Hautakuja kulisahau maishani mwako.

Tuambie tujifunze na kuna kitu kinaweza kutujenga maishani?
Siku ya kwanza kupaa na ungo.. Nakumbuka jioni ile tulienda kwa kiongozi mchawi mkuu, tukavua nguo na kubaki na chupi tuu tukapelekwa kwenye Kilinge katikati ya shamba la migomba huko tulipakwa madawa meusi na kupewa kaniki na ungo.. Kaniki tukajifunga lubega nyungo tukazishika mkono wa kulia na kutoka kinyumenyume

Tulienda hivyo mpaka kwenye uwanja wa shule ya msingi na kuamriwa kwa ishara hakuna kuongea kuchuchumaa huku mkono wa kushoto Ukishika chini

Ilipofika saa sita kamili usiku tuliamriwa kupanda nyungo zetu na kukaa kisha kiongozi akatupa usinga kama control panel
Ukiunyoosha mbele hiyo ni D
Ukiunyoosha juu ni kupaa
Ukiuelekeza chini ni kushuka
Usafiri wa ungo hauna rivasi

Nilipoanza kupaa niliogopa sana lakini nilipofika juu na kuweka D woga wote uliisha
 
Mmh dunia ina mambo
 
9/11.

Hii siku nakumbuka kila kitu.

Nilikuwa bado niko mwanafunzi chuoni.

Mchana wa hiyo siku nilikuwa nina darasa moja tu.

Nilikuwa senior nimebakiza credits chache tu kumaliza chuo.

Nilikuwa December graduate.

Madarasa/ masomo yote yaliahirishwa.

Asubuhi yote nilikuwa naangalia coverage ya CNN.

Nilikuwa naishi off-campus.

Muda wa kwenda darasani ulipofika, si profesa si wanafunzi, Hakuna mtu aliyekuwa na hamu ya kufundisha wala kufundishwa.

Tuliingia darasani. Mwalimu akaja. Akasema maneno machache. Akaruhusu na wanafunzi waseme machache.

Baada ya hapo wote tukatawanyika.

Sitoisahau hii siku. Nilishuhudia mubashara kabisa wakati moja ya yale maghorofa likiporomoka.

Ilikuwa ni kama ndoto flani hivi.

Tokea siku hiyo maisha yakabadilika kabisa.
 
Mimi siwezi kusahau nimewahi kuongea na Mungu nikiwa usingizini pasipo kumuona na alinijibu pasipo sauti kwa kukubali ombi langu ndiomana niko hai, Mungu uliye Mkuu na uliye hai unisamehe sana mimi ni mdhaifu bali naishi natambua upo na upo kweli na uhai. Asante sana Mungu mwenyewe huruma na mwenye upendo.🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏
 
Ilikuwa siku nimechoka maisha ya mkoani, nikaamua kudandia treni kutoka Mwanza kwenda Dar
Nikala dili na mpishi wa behewa la buffet, ni kukaa buffet huku nikiagiza soda au bia ya kuvutia muda, ila ikawa kila TT akipita niende kuning'ing'inia nje kwenye mlango huku treni inaenda.
Mara ghafla bin vuuh , TT huyu hapa anauliza watu tiketi kwenye behewa la buffet, nikachomoka na kwenda kujibanza nje,
Khaaah!11
nilikutana na nyomi full mziki inatembea na treni, ikawa ni fujo kugombania sehemu ya kuning'iinia mlangoni
Nilijikuta nimeshikilia fremu ya dirishani na vidole tu huku treni inaenda usiku mnene kwenye maeneo ya bonge la korongo yaani ukichomoa tu umekwisha.
Nashukuru Mungu,TT hakukawia sana buffet, nikarudi ndani, mpaka leo hii imekuwa ni ndoto la kutisha
 
Siku ya kwanza kupaa na ungo.. Nakumbuka jioni ile tulienda kwa kiongozi mchawi mkuu, tukavua nguo na kubaki na chupi tuu tukapelekwa kwenye Kilinge katikati ya shamba la migomba huko tulipakwa madawa meusi na kupewa kaniki na ungo.. Kaniki tukajifunga lubega nyungo tukazishika mkono wa kulia na kutoka kinyumenyume

Tulienda hivyo mpaka kwenye uwanja wa shule ya msingi na kuamriwa kwa ishara hakuna kuongea kuchuchumaa huku mkono wa kushoto Ukishika chini

Ilipofika saa sita kamili usiku tuliamriwa kupanda nyungo zetu na kukaa kisha kiongozi akatupa usinga kama control panel
Ukiunyoosha mbele hiyo ni D
Ukiunyoosha juu ni kupaa
Ukiuelekeza chini ni kushuka
Usafiri wa ungo hauna rivasi

Nilipoanza kupaa niliogopa sana lakini nilipofika juu na kuweka D woga wote uliisha
Aisee! Ila wachawi naskia mnaweza kwenda popote na kurudi pasipo vikwazo
 
Back
Top Bottom