Uliwezaje kuzivuka changamoto na magumu uliyopitia maishani?

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
18,143
32,887
Habari za muda huu ndugu zanguni.

Maishani mwetu wakati mwingine hutokeza changamoto na magumu mbali mbali yanayotukabili na kukabiliana nayo.

Changamoto za kimaisha na magumu kwenye harakati za maisha wakati fulani hutufanya kuvunjika mioyo na kuona kama dunia imekuelemea.

Lakini nyakati hizo ngumu hupaswi kuvunjika moyo na kukata tamaa bali kukabiliana na magumu.

Lakini pia kujua ya kuwa haupo peke yako kwenye changamoto na magumu hayo kunaweza kuongeza nguvu na ari ya kukabiliana nayo kupitia simulizi na habari za watu waliopitia changamoto na magumu maishani vinaweza kufufua tumaini lililokufa maishani mwako na kuyashinda majaribu.

Najua hata humu jamvini wapo watu walio wahi kupitia mikasa, visa na changamoto mbali mbali maishani lakini waliweza kuvuka na kuwa washindi na kubakia historia maishani mwao.

Kama hautojali unaweza uka share nasi kisa chako na kuwapa mwanga watu wanaopitia changamoto na magumu maishani humu jamvini.

Karibuni Sana wanajamvi.
 
Changamoto zipo kila sku na hazita kaa ziishe , hakuna kitu kizuri kama kuhakikisha afya yako ya akili ipo vizuri ili kukabiliana na mambo hasi yanayotukabili kwenye maisha yetu kila siku.
1704945904451.jpg
 
Tumia njia ya kushukuru Kwa kila jambo , hii huitwa Gratitude power IPO na nguvu Sana .

Maisha haijalishi unamiliki nini au unaishi wapi Kama binadamu lazima upitie katika vipindi vya changamoto ikiwa sio wewe basi wale unaowategemea na kuwapenda kikubwa kuwa MTU Wa kushukuru sana kuliko kulalamika.
 
Habari za muda huu ndugu zanguni.

Maishani mwetu wakati mwingine hutokeza changamoto na magumu mbali mbali yanayotukabili na kukabiliana nayo.

Changamoto za kimaisha na magumu kwenye harakati za maisha wakati fulani hutufanya kuvunjika mioyo na kuona kama dunia imekuelemea.

Lakini nyakati hizo ngumu hupaswi kuvunjika moyo na kukata tamaa bali kukabiliana na magumu.

Lakini pia kujua ya kuwa haupo peke yako kwenye changamoto na magumu hayo kunaweza kuongeza nguvu na ari ya kukabiliana nayo kupitia simulizi na habari za watu waliopitia changamoto na magumu maishani vinaweza kufufua tumaini lililokufa maishani mwako na kuyashinda majaribu.

Najua hata humu jamvini wapo watu walio wahi kupitia mikasa, visa na changamoto mbali mbali maishani lakini waliweza kuvuka na kuwa washindi na kubakia historia maishani mwao.

Kama hautojali unaweza uka share nasi kisa chako na kuwapa mwanga watu wanaopitia changamoto na magumu maishani humu jamvini.

Karibuni Sana wanajamvi.
Uvumilivu, na sala ndo kila kitu na risk taking basi.

Kumbuka vitu vizuri haivihitaji haraka.
And faith is the antidote of failure- napoleon hill
 
Back
Top Bottom