Ni pombe gani hutakuja kuisahau maishani mwako?

Grants na Valuer...hivi vinywaji vilitaka kunitoa roho...Lakini walevi huwa hatukomi!!...Naombeni ushauri wa kuacha pombe i see
 
Grants na Valuer...hivi vinywaji vilitaka kunitoa roho...Lakini walevi huwa hatukomi!!...Naombeni ushauri wa kuacha pombe i see
Walevi wooote huwa wanaombaga ushauri wa kuacha pombe ila hakuna aliepatiwaga ushauri akaufatilia...Grants, naipenda sanaaaa pole mkuuu, unataka uache pombe ufanye nini sasa?? Acha ujinga mzee kidding
 
Dah! pombe hizi jamani ni noma, juzi nimekula tungi kinoma... Nakuja kushtuka asubuhi nimelala kwenye pool table halafu hata sikumbuki nimefikaje 😂😂
 
Elezea kisa kilichokukuta mpaka ukasema hutakuja kuigusa pombe ya aina fulani
Magaritha, pombe hii inaseviwa ikiwa na barafu, (ice), kwenye glasi iliyopakwa chumvi pembeni na kipande ChA limao. Hivyo unakunywa huku unaramba chumvi na limao. Glasi ya kwanza niliifurahia, yapili nikamwambia asiwe mabarabu maana yanapunguza Wingi WA kinywaji kwenye GLASI LAKINI MHUDUMU ALINISHANGAA lakini alitii maagizo yangu akanipa bila barafu ndani. Kwakweli sikujuwa kuwa kumbe Ile pombe ni kali SanA ikaniunguza mdomo na koo lote Hali yangu ilikuwa tete kidogo niondoke,
 
Desperados - niliipenda ila hapana kwa sasa, ilibaki padogo nitapikie BENNETON GEMS Sea cliff i halafu pombe yenyewe sikuinywa hapo imagine mtu unaingia unafikia kutapika Uzuri tu ukimaliza ukuta wa gems uko toilet nilitapika jamani hee sitasahau macho yakawa yana maji maji kama nalia afu watu wananiambia Ooh so sorry aibu kama nini...
SERENGETI LITE - Chungu ,mbaya sauti ilibadilika nikawa naongea kama mwanaume

desperados inanipenda na mi naipenda balaa i can drink it mpk nichoke kitu kimenishinda ni (cognac) km hennessy
 
Walevi wooote huwa wanaombaga ushauri wa kuacha pombe ila hakuna aliepatiwaga ushauri akaufatilia...Grants, naipenda sanaaaa pole mkuuu, unataka uache pombe ufanye nini sasa?? Acha ujinga mzee kidding
Hakuna utopolo sijanywa si Bia, Brandy, Spirit, Whiskey, Vodka....nataka kustahafu
 
Kuna siku nilienda kumtembelea jamaa yangu gheto kwake. Mida ya jioni akanitoa out mimi na washkaji wengine.

Binafsi sinywi pombe, nilipiga grand malt zangu nila wenge. Around saa mbili au tatu kasoro tukarudi gheto. Alipopanga, nyumba ina fensi.

Sasa tushaingia ndani, jamaa akafunga na geti kabisa. Dakika chache mbele kuna mtu akawa anagonga geti huku akiita na kuomba afunguliwe. Jamaa yangu akaanza kuwaka, yule ni nani anasumbua watu mida ile wakati yeye (jamaa yangu) alishaweka sheria, akiingia ndani, ambao mko nje mtafute pa kulala (hapo kumbuka nyumba sio yake, amepanga).

Kumbe bhana anabishana na mwenye nyumba . Yule faza house baada ya kuona maneno ya shombo yamezidi, akaamua kuondoka (alikuwa mfupi tena kibonge, asingeweza ruka ukuta).

Hiyo ndio ilikuwa mara ya mwisho jamaa yangu kuishi pale, japo kodi ilikuwa bado sana kuisha.
katisha
 
Aisee.pombe ilimfanya vibaya rafiki yangu,tunakaribia kupiga pepa la mwisho kidato cha sita kule mkoani morogoro jamaa angu alipiga ulanzi akachanganya na gongo akapitiliza kabisa kunywa ,anarudi skuli usiku mnene mlango wa bwenini anauona mdogo,Mara anajaribu kuinama ili aingie ndani bwenini yan utafikiri mlango wa kuingilia bwenini ni kama mlango wa banda la kuku kumbe ni mlango mkubwa tu,basi jamaa alitukana bweni zima na kutapika koridoni na baraza za nje ya bweni zilijaa matapishi yake na kesho yake tulikuwa na pepa ngumu kumesa,kesho siku ya pepa alibaki analia tu kwenye exams room kila wakati anaomba abadilishiwe calculator...
 
Kuna siku nilikuwa na hamu ya kuzimua kidogo, nikaingia baa...nikaagiza castle lite na nyagi ndogo ( kasichana) nikapiga, bia ikaisha nikaongeza bia mbili Tena ili kuimalizia konyagi.

Ilipoisha nikaanza kupiga lite za kutosha! Sijakaa sawa akaja rafiki yangu dokta akasema tuchukue mzinga mkubwa wa Valeur.

Tukauchukua, tukaanza kuupiga mpaka ukaisha, ebwana eeee.....!!! Nikaanza kutoka baani kwenda home saa nane usiku kwa mguu, kumbe geji inapanda**.

Nilipofika home badala ya kuingia ndani nilipitiliza kwenye fensi yenye miiba...nikawa nafosi kupita pale...yaani nilichomwa miiba balaa!

Nilichafuka huku naangukia miba..baadae sijui ikawaje nikaingia chumbani nikalala...

Kuamka asubuhi kila sehemu nimekwaruzwa Kama viwembe hivi..njaaa....halafu macho yanatoa machozi fulani hivi yanaumaa!

Nikapigia boda akaleta nyama nusu, maji makubwa ya baridiii, na Pepsi baridiii.

Nikaandaa supu..nikainywa mdogo mdogo.

Nilishinda nimo ndani tu, kumbe Kuna dada mmoja aliniona ile night navyofakamia ile fensi Kama mbogo.
Baada ya siku mbili baadae akaniuliza kumbe kaka unakunywa? Niliona aibu maana sikuwahi kuonekana nimekunywa!

Huo usiku nilkuwa full yaani yeyote akikaa mbele nilijiapiza anachezea mkono, sijui hayo mawazo yalitoka wapi. Nilipita sehemu walipo vibaka nawatafuta kwa kuwaita kabisa nikielekea home.

Sikujua nikuwa nalazimisha nivuke fensi niende wapi!

#Valeur haifai#
Pole sana mkuu umenikumbusha habari ya valeur
nilikuwa na mwanangu mmoja mungu amlaze pema alikuwa akija likizo ni mwendo wa valeur vile vichupa vidogo siku tupo wanne
tukaamua kujirudishia shukrani na valeur vitoto box zima mama muuza akasema zimeisha tukaamia nyingine ya pakiti ilikuwa inaitwa samson
baada ya pakiti 3 nilifika home fresh wenge la taa likanichanganya nikaanza kurudisha chenji ghafla
nilitoka nje nikalala shambani kutoka saa nne mpaka majogoo
na mara ya mwisho kunywa hicho kinywaji na kupaki bus kizembe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom