Ni njia zipi zitaweza kumsaidia mwanamke huyu ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni njia zipi zitaweza kumsaidia mwanamke huyu ?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by hollo, Jun 13, 2008.

 1. hollo

  hollo JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 781
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Mwanamke katika jamii amekuwa akionekana ni last class katika kila akitu !
  ELIMU :Asilimia kubwa ya wanawake hawapatiwi elimu,na hata wakiwa shuleni wengi hawafanikiwi katika elimu,pia katika masomo ya sayansi kuna idadi ndogo sana ya wanawake ukilinganisha na wanaume.
  SIASA :Katika siasa mfano katika bunge kuna idadi ndogo sana ya wanawake pamoja na kuwepo kwa viti vya upendeleo.
  UCHUMI :Asilimia kubwa na wanawake hali zao ni mbaya sana kiuchumi.
  Sasa swali ni kwamba kwa nini wanawake wako nyuma katika kila kitu ?Je wasaidiweje ili na wenyewe wawe mbele au kuwa sawa na wanaume ?
   
 2. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2008
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,867
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Dawa ni kwamba jamii iwe na mtazamo positive kuhusu mwanamke. Kuanzia pale wazazi wanapopata mtoto wa kike wamthamini sawa na mtoto wa kiume, wamlee vizuri akue na kuwa na afya nzuri. Baada ya hapo wamsaidie kupata elimu bora na wampe misingi mizuri ya kiroho na kijamii ikiwemo kujiamini. Mara akisoma na kuhitimu kwa kadri ya uwezo wake jamii imuamini katika nafasi yoyote atayoamua kuitumikia Wakati akiitumikia jamii hiyo, Mwanamke huyu ajiamini na kuangalia mbele. Mifano halisi ya wanawake waliokuwa na vision ya kusonga mbele ipo na tunawafahamu!!! Mchango wangu unaishia hapo kwa leo ili kuwapa nafasi na wengine watoe maoni yao.
   
 3. M

  Malila JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2008
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Mimi nachangia njia mojawapo ya kumkomboa mwanamke; jamii yetu ibadilishe mafundisho/malezi juu ya mwanamke.Miongoni mwa sehemu ambako kunatakiwa kuangaliwe ni ktk imani zetu; kwa mfano; Mwanamme ni kichwa cha nyumba; kazi ya kupika ni ya wanawake,vipi hapo? mwanaume ruksa kurudi nyumbani usiku,kule kwetu mwanamke hagawiwi ardhi, mwanamke hawezi kusema mbele ya wanaume.

  Kwa ufupi mambo ni mengi sana yanayo jenga udhaifu kwa mwanamke. Hayo ni maoni yangu, na wengine watachangia.
   
 4. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Elimu tu ndiyo dawa .... tuwape fursa watoto wetu wasome ... hata kama atapata mimba tupiganie sana arudi shule ... na wale waliolewa wakakatishwa masomo ... wajitahidi aleast wapate nafasi ya kusoma...
   
 5. hollo

  hollo JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 781
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Kweli Elimu ndo dawa!kumuelimisha mtoto wa kike ni kuelimisha jamii nzima!Tumpe elimu mtoto wa kike!tumfundishe kujiamini kwamba anaweza!Maana wakati mwingine kuna inferiority complex ambayo amajengewa mwanamke na kumfanya ajiamini kuwa hawezi!
  kuanzia akiwa mtoto!mtoto wa kike anatakiwa kufundishwa kujiamini na si vinginevyo!
   
 6. Single D

  Single D JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 459
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wanawake wengi leo wamesoma na wana uelewa mpana sasa katika mambo ya jamii na pia uchumi wao si haba.Hayo yote hayatawasaidia bila kuthubutu kuonyesha kwa vitendo kuwa wanaweza hata kuongoza na kusimamia masuala mbalimbali.Kama waziri anaulizwa swali general la utalii anashindwa kujieleza,tutegemee nini kwa wanawake?Tusisubiri kuonekana wakati tu wa uchaguzi kama Anna Senkoro baadaye unapotea.
  Waonyeshe kwa utendaji wao katika nafasi walizo nazo sasa hivi kuwa wanaweza kuwashawishi umma kuwa marais,mawaziri,wabunge wa kuchaguliwa(not special seats),wakuu wa mikoa n.k.
  Pia wasirudikane TAWLA,TAMWA,Wizara ya maendeleo,jinsia na watoto waende pia wizara ya ulinzi na JKT,Kilimo n.k
   
Loading...