Zed
JF-Expert Member
- Mar 28, 2009
- 434
- 252
Hili ni swali ambalo wananchi wanajiuliza ingawa sio kwa maneno hayo au muktasari kama lilivyo hapo juu. Wananchi wanajiuliza swali kwa maneno kama: je katiba mpya itaniletea chakula au itaondoa dhuluma, itanisadia kutumia rasilimali zangu vema? itathamini kura yangu na kuyafaa maisha yangu?
Majibu ya wanasiasa na wanaharakati wa vuguvugu la katiba mpya nayo pia hayatofautiani sana na maswali ya wananchi; wao wanayo ndoto katiba ya mfumo ule ule huku wakitegemea uwazi na uwajibika zaidi, haki zaidi sheria zaidi kupunguza nguvu za rais nk ila kwa namna gani mfumo huo utahakikishia haya hilo halibainishwi. Katiba mpya ni uhakika wa kuchaguliwa kwao kwa bunge lile lile kwa kutumia "tume huru".
Upya katika katiba mpya upo katika neno moja tu „UGATUZI“ (Devolution) „mfumo wa uwakilishaji madaraka na ugavi wa matumizi ya rasilimali kutoka serikali kuu kwenda kwa uongozi wa magatuzi au serikali za majimbo, mkoa au mitaa“ kwa namna hii ni kuwarudishia wananchi uhuru na madaraka ya kujiamulia mambo yao wenyewe kwa mstakabali na rasilimali zao na vizazi vijavyo (ambayo ndio maana demokrasia). Jambo ambalo liliporwa na wakoloni na baadae serikali baada ya ukoloni na baadae hawakuona umuhimu wa kuwarudishia wananchi hayo, hivyo wakawa wakoloni weusi.
Historia ya nchi yetu tangu ukoloni na haswa baada ya ukoloni umejenga hofu kubwa kwa jambo hili la Ugatuzi. Ikiwa ni janjanja ya kubakiza madaraka kwa wakoloni weusi ingawa Mlw Julius Nyerere 1972 alijaribu kwa tahadhari sana huku akiilinda siasa yake changa wakati huo ya ujamaa na kujitegemea kwa kuleta ugatuzi akiuta „Madaraka Mikoani“ Ila uwoga hakuitekeleza azma hiyo. Mfumo wa uteuzi wa viongozi Kama maRC na MaDC uliendelea kubaki badala ya uchaguzi
Nchi zilizo na maendeleo ya kweli nyingi ni zile zilizofanya ugatuzi: Marekani, Ujerumani, Kanada, India, Singerpore, Gabon, Austria, Malaysia, Brazil na Kenya ambayo tangu ianze kutumia mfumo huo Demokrasia yake inakua na uchumi unaanza kufanya mabadiliko majimboni na mashinani.
Ikiwa Tanzania inataka maendeleo yenye kubadisha Maisha ya watu hainabudi kutengeneza KATIBA MPYA itakayozingatia na kufanya UGATUZI.
NB Uchangiaji wa Kichuguu upo Off-point!