Ni Nini Hatma ya Ndoa ya Gwajima + Lowassa na UKAWA kwa Taifa Letu?

W. J. Malecela

Verified Member
Mar 15, 2009
14,056
2,000
MCHUNGAJI wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima sasa amejipapambunua hadharani msimamo wake, jambo ambalo ni tofauti kabisa na viongozi wengine wote wa Dini nchini akiwa sanjari na swahiba wake Edward Lowassa anayempa mbinu za kufufua mizimu, ili wapate wafuasi.

Viongozi ni binadamu na wanastahili kuwa na utashi wa kisiasa, lakini hili la mmiliki wa Kanisa kusimama kiongozi wake kwa swahiba wake Edward Ngoyai Lowassa, ndiko ambako awali watathamini wa siasa nchini walisema, tatizo si Lowassa peke yake na genge lililowazunguka nalo kama likiingia IKULU ni tatizo ambalo heri mara 100 ya CCM ya sasa.

Lowassa ambaye CHADEMA badala ya kumfanyia kampeni kwa wakati huu wanamhangaikia kumsafisha, huku wanaomzunguka nao wakiwa wachafu mikononi, usoni na mioyoni mwao. Wana sifa nyingi zenye mushkeli kwa afya ya mustakabali wa amani,upendo na pasipo na chuki wala IKULU kuvamiwa na genge la walanguzi walio midomo wazi wakiisubiria kama Mafisi.

Gwajima swahiba wa Lowassa aliwahi kuutangazia umma wa Watanzania kuwa anataka kumfufua kada na mbunge wa viti maalum CCM, marehemu Amina Chifupa aliyekuwa mke wa marehemu Meddy Mpakanjia ‘CK'.
Gwajima mwenye kushabihiana mambo mengi na mgombea wa CHADEMA Lowassa kikauli na mitazamo, pia alipata kutoa kauli nyingine ngumu ambazo nazo hadi sasa hazijatekelezwa ikiwemo ya kutaka kumfufua aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine.

Kushabihiana kwao, kiahadi zao na aina ya matendo ya kusema maneno magumu kwa mgombea wa CHADEMA, Edward Ngoyai Lowassa ambaye nae naye amewaahidi Watanzania kuwaletea aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, marehemu Daud Balali.

Ufufuo wa Lowassa unatofauti gani na ndoto za mchana za Gwajima ambaye alipata kufikishwa mahakamani kwa tabia na kauli zake kuwa atafufua misukule? maana yake ni kutaka kupata wafuasi wengi kanisani kwake ambao kimsingi wana matarajio tofauti na mmiliki wao.
Lowassa maana yake anataka kumsuta mhariri mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Nevil Meena gazeti linalomilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Bwana Meena ni katibu wa jukwaa la wahariri ni mtu makini sana, mwenye kuiheshimu taaluma yake, sijui atapotoka vipi leo akituaminisha kuwa habari alizotuhuthibitishia Watanzania kuwa Balali alikufa, si kweli yu hai.

Akiwa mhariri wa Mwananchi Jumapili wakati huo, Meena alikwenda kuihoji familia ya Balali nchini Marekani na kupiga picha ya kaburi la marehemu Balali. Katika habari ile aliwahoji mke, dada na watu wa karibu kabisa wa familia hiyo, waliothibitisha kifo cha ndugu yao na kuwa alizikiwa nchini Marekani, inawezekanaje leo aseme habari ile ni uongo, ukweli ni anaosema Lowassa.

Tuache siasa, tusitake kwenda IKULU kwa uongo wa kupata wafuasi. Mbali ya gazeti la Mwananchi, pia gazeti la Mtanzania liliandika habari hiyo ikiwemo na uthibitisho wa familia iliyopo kijijini kwao na waliopo nchini Marekani. Meena alikwenda Marekani ambako ni zaidi ya masaa 15 kutoka Tanzania kwa usafiri wa Ndege kwenda kusaka ukweli na kuondoa minong'ono iliyokuwa imetanda kuwa Balali yu hai.

Si haki hata chembe kuitumia familia ya marehemu Balali kuingilia IKULU, walipata msiba mzito sana, waliumia sana, lakini kwa kuwa ni kazi ya Mungu, walishukuru na kumuombea astarehe kwa amani, leo hii mnawatangazia ataletwa Tanzania, nini maana yake? Akitokea wapi? Lowassa nawe ni mzee wa ufufuo?

Gwajima si mtu safi, hata kidogo ukimsikiliza Dk. Willbroad Slaa katika hotuba zake zote, hata siku moja hakupata kuzungumzia mahusiano ya kifamilia, si kwa Freeman Mbowe, Tundu Lissu wala kwa Gwajima mwenyewe ambaye hajajisafisha hadharani madai ya kuzaa na mwimbaji wa nyimbo za Injili, Frola Mbasha, ambaye ni mke wa mtu.

Leo hii waliokuwa wakimtetea Gwajima kwa sakata lile la kumpora Emmanuel Mbasha mkewe, hata kama wanampenda vipi mchungaji huyu, ni wazi usafi wake umeingia matundu kiasi si rahisi waamini vinginevyo kutokana na maneno yake na matendo yake ya sasa.

Lowassa amewaahidi Watanzania kuwa atamtoa Nguza Viking na Pappii Kocha, je katika utafiti wake kuwa vifungo vyao vinatia shaka amewauliza walimu wa shule ya msingi Mapambano pale Sinza? Amewauliza majirani wa Sinza kijiweni? Atapata aibu maana wazazi walioathirika na jambo lile, mioyo yao itapata kutu kumsikiliza binadam huyu asiye na huruma kwa malaika wale waliodhalilishwa.
Jaji Thomas Mihayo aliyekazia hukumu ya maisha kwa Babu Seya ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa Baraza la Habari Nchini, ni mtu mwenye kuaminika sana katika jamii, ana heshma kubwa sana jaji huyu mstaafu leo hii ukimwambia hukumu yake aliitoa kwa maelekezo sidhani kama Jaji yeyote nchini anayemjua na walimsifia sana wakati akistaafu kwa hukumu ile, majaji wa Tanzania watakuelewa?

Ni kujenga chuki ndani ya jamii yetu ni kuondoa dhana ya utawala bora. Gwajima mshenga wa Lowassa kuingia CHADEMA, ni maswahiba wa kauli zao ngumu, ahadi zao zenye kukinzana na Mwenyezi Mungu, wanaweza mshambulia mtu yeyote ilimradi waende IKULU, aah mzee wa maharage ya wapi! mjinga mmoja, asiyefaa mmoja !.

Hakukosea kuwa mshenga wa mzee wa maamuzi magumu mwenye uwezo pia wa kufufua watu ambaye pia mwenye kutaka ushindi wake utokane na waumini wa dhehebu lake, loh kama mwalimu angekuwepo leo angetoka hadharani na sijui angetamka nini dhidi ya Watanzania hawa wawili.

Hatahivyo, Hongereni kwa urafiki wenu. Watanzania tuwe makini sana tunaofikiria kuwapa mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.

Le Mutuz Nation
 
Cool Runnings

JF-Expert Member
Feb 4, 2013
278
195
Tehetehetehe, sera za CCM mbona hatuzisikii majukwaani tunasikia matusi tu!?

Au hali hiyo nayo imesababishwa na Lowassa na Gwajima?

Mgombea wenu hawezi hata kukampeni na mkewe!!
 
fugees

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
2,872
2,000
MCHUNGAJI wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima sasa amejipapambunua hadharani msimamo wake, jambo ambalo ni tofauti kabisa na viongozi wengine wote wa Dini nchini akiwa sanjari na swahiba wake Edward Lowassa anayempa mbinu za kufufua mizimu, ili wapate wafuasi.

Viongozi ni binadamu na wanastahili kuwa na utashi wa kisiasa, lakini hili la mmiliki wa Kanisa kusimama kiongozi wake kwa swahiba wake Edward Ngoyai Lowassa, ndiko ambako awali watathamini wa siasa nchini walisema, tatizo si Lowassa peke yake na genge lililowazunguka nalo kama likiingia IKULU ni tatizo ambalo heri mara 100 ya CCM ya sasa.Lowassa ambaye CHADEMA badala ya kumfanyia kampeni kwa wakati huu wanamhangaikia kumsafisha, huku wanaomzunguka nao wakiwa wachafu mikononi, usoni na mioyoni mwao. Wana sifa nyingi zenye mushkeli kwa afya ya mustakabali wa amani,upendo na pasipo na chuki wala IKULU kuvamiwa na genge la walanguzi walio midomo wazi wakiisubiria kama Mafisi.Gwajima swahiba wa Lowassa aliwahi kuutangazia umma wa Watanzania kuwa anataka kumfufua kada na mbunge wa viti maalum CCM, marehemu Amina Chifupa aliyekuwa mke wa marehemu Meddy Mpakanjia ‘CK’.
Gwajima mwenye kushabihiana mambo mengi na mgombea wa CHADEMA Lowassa kikauli na mitazamo, pia alipata kutoa kauli nyingine ngumu ambazo nazo hadi sasa hazijatekelezwa ikiwemo ya kutaka kumfufua aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine.

Kushabihiana kwao, kiahadi zao na aina ya matendo ya kusema maneno magumu kwa mgombea wa CHADEMA, Edward Ngoyai Lowassa ambaye nae naye amewaahidi Watanzania kuwaletea aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, marehemu Daud Balali.

Ufufuo wa Lowassa unatofauti gani na ndoto za mchana za Gwajima ambaye alipata kufikishwa mahakamani kwa tabia na kauli zake kuwa atafufua misukule? maana yake ni kutaka kupata wafuasi wengi kanisani kwake ambao kimsingi wana matarajio tofauti na mmiliki wao.
Lowassa maana yake anataka kumsuta mhariri mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Nevil Meena gazeti linalomilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Bwana Meena ni katibu wa jukwaa la wahariri ni mtu makini sana, mwenye kuiheshimu taaluma yake, sijui atapotoka vipi leo akituaminisha kuwa habari alizotuhuthibitishia Watanzania kuwa Balali alikufa, si kweli yu hai.

Akiwa mhariri wa Mwananchi Jumapili wakati huo, Meena alikwenda kuihoji familia ya Balali nchini Marekani na kupiga picha ya kaburi la marehemu Balali. Katika habari ile aliwahoji mke, dada na watu wa karibu kabisa wa familia hiyo, waliothibitisha kifo cha ndugu yao na kuwa alizikiwa nchini Marekani, inawezekanaje leo aseme habari ile ni uongo, ukweli ni anaosema Lowassa.Tuache siasa, tusitake kwenda IKULU kwa uongo wa kupata wafuasi. Mbali ya gazeti la Mwananchi, pia gazeti la Mtanzania liliandika habari hiyo ikiwemo na uthibitisho wa familia iliyopo kijijini kwao na waliopo nchini Marekani. Meena alikwenda Marekani ambako ni zaidi ya masaa 15 kutoka Tanzania kwa usafiri wa Ndege kwenda kusaka ukweli na kuondoa minong’ono iliyokuwa imetanda kuwa Balali yu hai.

Si haki hata chembe kuitumia familia ya marehemu Balali kuingilia IKULU, walipata msiba mzito sana, waliumia sana, lakini kwa kuwa ni kazi ya Mungu, walishukuru na kumuombea astarehe kwa amani, leo hii mnawatangazia ataletwa Tanzania, nini maana yake? Akitokea wapi? Lowassa nawe ni mzee wa ufufuo?

Gwajima si mtu safi, hata kidogo ukimsikiliza Dk. Willbroad Slaa katika hotuba zake zote, hata siku moja hakupata kuzungumzia mahusiano ya kifamilia, si kwa Freeman Mbowe, Tundu Lissu wala kwa Gwajima mwenyewe ambaye hajajisafisha hadharani madai ya kuzaa na mwimbaji wa nyimbo za Injili, Frola Mbasha, ambaye ni mke wa mtu.

Leo hii waliokuwa wakimtetea Gwajima kwa sakata lile la kumpora Emmanuel Mbasha mkewe, hata kama wanampenda vipi mchungaji huyu, ni wazi usafi wake umeingia matundu kiasi si rahisi waamini vinginevyo kutokana na maneno yake na matendo yake ya sasa.

Lowassa amewaahidi Watanzania kuwa atamtoa Nguza Viking na Pappii Kocha, je katika utafiti wake kuwa vifungo vyao vinatia shaka amewauliza walimu wa shule ya msingi Mapambano pale Sinza? Amewauliza majirani wa Sinza kijiweni? Atapata aibu maana wazazi walioathirika na jambo lile, mioyo yao itapata kutu kumsikiliza binadam huyu asiye na huruma kwa malaika wale waliodhalilishwa.
Jaji Thomas Mihayo aliyekazia hukumu ya maisha kwa Babu Seya ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa Baraza la Habari Nchini, ni mtu mwenye kuaminika sana katika jamii, ana heshma kubwa sana jaji huyu mstaafu leo hii ukimwambia hukumu yake aliitoa kwa maelekezo sidhani kama Jaji yeyote nchini anayemjua na walimsifia sana wakati akistaafu kwa hukumu ile, majaji wa Tanzania watakuelewa?

Ni kujenga chuki ndani ya jamii yetu ni kuondoa dhana ya utawala bora. Gwajima mshenga wa Lowassa kuingia CHADEMA, ni maswahiba wa kauli zao ngumu, ahadi zao zenye kukinzana na Mwenyezi Mungu, wanaweza mshambulia mtu yeyote ilimradi waende IKULU, aah mzee wa maharage ya wapi! mjinga mmoja, asiyefaa mmoja !.

Hakukosea kuwa mshenga wa mzee wa maamuzi magumu mwenye uwezo pia wa kufufua watu ambaye pia mwenye kutaka ushindi wake utokane na waumini wa dhehebu lake, loh kama mwalimu angekuwepo leo angetoka hadharani na sijui angetamka nini dhidi ya Watanzania hawa wawili.Hatahivyo, Hongereni kwa urafiki wenu. Watanzania tuwe makini sana tunaofikiria kuwapa mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
Le Mutuz Nation
Magamba ka kuiga mambo tumechoka sasa.
 
kioju

JF-Expert Member
Apr 28, 2014
805
250
Gwajima na Lowassa ni marudio tu ya Mrema na Kakobe....

Nchi hii askofu na mchungaji yeyote anaweza kumpigia mtu kampeni waziwazi

ngoja siku BAKWATA wataje mgombea wao waziwazi uone watakavyo shambuliwa.....
Na unatakiwa ufanye utafit na kujiridhisha kwanin hawa wanafanya hvyo? Hujafanya utafit matokeo yake unakuja kuropoka utumbo na uchafu wake.
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
11,690
2,000
Gwajima na Lowassa ni marudio tu ya Mrema na Kakobe....

Nchi hii askofu na mchungaji yeyote anaweza kumpigia mtu kampeni waziwazi

ngoja siku BAKWATA wataje mgombea wao waziwazi uone watakavyo shambuliwa.....

Bora Mwanasiasa na mchungaji/askofu kuliko ya mwanasiasa na mganga wa kienyeji kama ilivyokuwa kwa Kikwete na Sheikh Yahya!
 
STDVII

JF-Expert Member
Nov 24, 2014
1,585
2,000
Tehetehetehe, sera za CCM mbona hatuzisikii majukwaani tunasikia matusi tu!?

Au hali hiyo nayo imesababishwa na Lowassa na Gwajima?

Mgombea wenu hawezi hata kukampeni na mkewe!!
CCM ina timu ya kampeni CDM taja 7 tuone kama wapo CDM asilia
 
W. J. Malecela

Verified Member
Mar 15, 2009
14,056
2,000
Tehetehetehe, sera za CCM mbona hatuzisikii majukwaani tunasikia matusi tu!?

Au hali hiyo nayo imesababishwa na Lowassa na Gwajima?

Mgombea wenu hawezi hata kukampeni na mkewe!!

- Hahahahaha kwa sera za Babu Seya na Uamsho, ndio maana CCM imeona hamna mashindano wala sababu ya kwenda na Mke, hahahahah KIDUMU CHAMA TAWALA!!

le Mutuz
 
W. J. Malecela

Verified Member
Mar 15, 2009
14,056
2,000
Magufuli ameshindwa kumwongoza mke wake mmoja, hawezi kuliongoza Taifa! Akajifunze kwanza kumwongoza mkewe, halafu ajaribu tena 2020!
- hahahaha anyegombea urais ni Magufuli sio mke wake, mgombea wenu afya yake sio nzuri ndio maana lazima mke wake ampigie kampeni hahahahahha na gwajima hahahahaha

le Mutuz
 
happymalya

Senior Member
Sep 1, 2015
116
0
asante sana kaka kwa kutoaaa ukweliii... mwenye hatma n Dr. MAGUFULI tuuuuuu . Afu namshangaaa sana ngwajimaaa mchungaji anyejichanganya na siasa. inatishaaa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom