Moja ya Taasisi hizi zipewe jina la Edward Lowassa kama njia ya kumuenzi

kikaniki

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
502
938
Edward Lowassa amefariki na leo tumempunzisha. Pole sana kwa Taifa na familia yake.

Nimekaa, nimewaza kwa kuwa Hayati Lowassa amefanya mengi sana hapa Tanzania ninashauri yafuatayo. Baadhi ya Taasisi ziitwe Kwa jina lake. Mfano:-

Chuo cha Ualimu Monduli ambapo Hayati Lowassa alisoma kiitwe Monduli Edward Lowassa Teachers College. Au Chuo cha CDTI cha Monduli, kiitwe Edward Lowassa CDTI. Au hata Ukumbi wa Mikutano wa Arusha (AICC) uitwe Ukumbi wa Mikutano wa Edward Lowassa ikizingatiwa kuwa amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ukumbi huo

Ninawasilisha. Mama Samia Rais wetu kwa kuwa huwa anapitia humu Jf ikimpendeza, basi tufanye hivyo.
 
Na nyinyi ifikie wakati mtuache tupumzike sasa. Kila kitu mnataka mkiite kwa majina yenu as if kama hivyo vitu mlijenga kwa pesa zenu za mifukoni!

Kuenzi! Kuenzi!
 
Edward Lowassa amefariki na leo tumempunzisha. Pole sana kwa Taifa na familia yake.

Nimekaa, nimewaza kwa kuwa Hayati Lowassa amefanya mengi sana hapa Tanzania ninashauri yafuatayo. Baadhi ya Taasisi ziitwe Kwa jina lake. Mfano:-

Chuo cha Ualimu Monduli ambapo Hayati Lowassa alisoma kiitwe Monduli Edward Lowassa Teachers College. Au Chuo cha CDTI cha Monduli, kiitwe Edward Lowassa CDTI. Au hata Ukumbi wa Mikutano wa Arusha (AICC) uitwe Ukumbi wa Mikutano wa Edward Lowassa ikizingatiwa kuwa amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ukumbi huo

Ninawasilisha. Mama Samia Rais wetu kwa kuwa huwa anapitia humu Jf ikimpendeza, basi tufanye hivyo.
TANESCO itapendeza zaidi.
 
Kwani chadema wanamuenzi vipi mgombea wao wa urais? Au walitaka watajwe tu kwenye historia ya marehemu bila wao kumtambua kwa lolote?
 
Edward Lowassa amefariki na leo tumempunzisha. Pole sana kwa Taifa na familia yake.

Nimekaa, nimewaza kwa kuwa Hayati Lowassa amefanya mengi sana hapa Tanzania ninashauri yafuatayo. Baadhi ya Taasisi ziitwe Kwa jina lake. Mfano:-

Chuo cha Ualimu Monduli ambapo Hayati Lowassa alisoma kiitwe Monduli Edward Lowassa Teachers College. Au Chuo cha CDTI cha Monduli, kiitwe Edward Lowassa CDTI. Au hata Ukumbi wa Mikutano wa Arusha (AICC) uitwe Ukumbi wa Mikutano wa Edward Lowassa ikizingatiwa kuwa amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ukumbi huo

Ninawasilisha. Mama Samia Rais wetu kwa kuwa huwa anapitia humu Jf ikimpendeza, basi tufanye hivyo.
Acheni mawazo mfu.
 
Ni kweli kabisa na mimi naunga mkono hii hoja.Ila Noboresha hilo jina la chuo ulilolipendekeza:Hilo jina lianze kabisa hivi:EDWARD LOWASA,MONDULI TEACHERS COLLEGE.
 
Ingependeza CHADEMA lile pagale lao la Mikocheni waliite Edward Lowassa House baada ya kuwasaidia kupata ruzuku za kutosha mwaka 2015.
 
Back
Top Bottom