Ni nani mchezaji wako bora wa Simba SC kwa msimu huu wa 2023/24?

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,906
4,846
Naaaje wazee,

Ligi ya NBC inaelekea ukingoni huku Bingwa akiwa ameshafahamika tayari. Kwa sasa vita ipo sehemu nne tu:

1. Nafasi ya Pili
2. Nafasi ya nne
3. Kujinasua kucheza Playoff
4. Kujinasua kushuka daraja

Tutakuwa tunakutana kwenye nyuzi kujadili mambo mbalimbali ya msimu huu unaoisha na huo unaotarajiwa kuanza. Leo tuijadili Simba SC na mwenendo wake wa msimu huu. Nafahamu fika mashabiki wa Simba wamepoteza confidence kutokana na kiwango cha kusuasua kwenye ligi Kuu kwa msimu huu.

Hata hivyo, pamoja na misukosuko na kiwango kisichoridhisha cha timu, wapo baadhi ya Wachezaji wanaweza kuinuka kifua mbele kwa mchango wao ndani ya timu.

Kwa upande wangu naona pamoja na kiwango kibovu cha timu lakini Wachezaji Zimbwe Jr na Che Malone wamejitahidi kufanya majukumu yao katika hali zote.

Vipi wewe ukiambiwa uchague mchezaji wa kumpa tuzo ndani ya Simba kwa msimu wa 2023/24 utamchagua nani?
 
Ni bora Simba imalize ya 3 na kujipanga upya. Bado haina timu ya kushindana champions league na inahitaji kusajili wachezaji kama 8 wapya na kutengeneza uongozi unaosikilizana na timu yenye ari mpya.

Wapunguze pressure msimu ujao huku wakitafuta zaidi kikombe cha ligi ili kurudisha imani kwa wanachama na mashabiki wake.

Wakubali kushiriki shirikisho ambapo hakuna pressure.

Huo ni ushauri wangu kama shabiki wa Coastal Union.
 
Back
Top Bottom