Ni nani huandaa maigizo ya CCM?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,845
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimechoka kuliko uchovu wenyewe. Ikifika mahali chama kikishindwa hata kwenye mambo mepesi kabisa! Basi tambua chama kimezeeka kuliko umri wake na kimechoka kuliko kuchokwa!

Miujiza kwa asilimia 99 inayofanywa na manabii na mitume kwenye makanisa yao ni ya uongo mkubwa na ya kutengenezwa. Shuhuda zinazotolewa na wanaoitwa waumini ni za uongo na za kutengenezwa, lakini hawa mitume na hawa manabii wana timu bora za kusaka vipaji vya waigizaji kwenye miujiza na shuhuda.

Wale waigizaji hufanya kwa usahihi sana kiasi cha kutengeneza uhalisia na kuaminika miongoni mwa wengine, kitu kinachowapa mileage kubwa mitume na manabii wasanii.

Kinachowashinda CCM ni kipi? Kwanini huwa wanashibdwa vibaya sana linapokuja suala la kutengeneza maigizo? Si wawaazime basi wale wasanii wa akina mwamposa?

Shida kubwa kongwe na sugu ya CCM ni upigaji, maokoto na kula kwa urefu wa kamba kiasi kwamba fungu linalotengwa kwa jambo fulani mpaka limfikie mlengwa linakuwa limeshapita kwenye mikono zaidi ya mitatu na kila mkono unanyofoa chake! Matokeo yake ni kufeli kwa jambo husika.

Mitume na manabii ni wakweli na waaminifu kwenye jambo moja! Kutimiza ahadi za malipo kwa waigizaji wao kwenye ibada zao. Aisee huwa hawawapunji hata senti tano. Wanalipa walichoahidi na kukubaliana na kwakuwa malipo ni mazuri na hayana ubabaishaji basi waigizaji nao hujitahidi sana kufanya kwa usahihi bila kukosea!
  • Hii huwezi kuita ni coincidence hata siku moja
  • Wamama watu wazima wote
  • Wenye sare mpya wote na zinazofanana
  • Waliowekwa sehemu moja
  • Wainuke kwa pamoja kama kwaya
  • Wasogee eneo moja
  • Walale chini kwa pamoja na kwa mfanano
  • Kisha waanze kupiga kelele mfano wa watu wanaolia nknk
  • Yaani utadhani ni maroboti yamesetiwa na kuendeshwa kwa rimoti
Aaaah jamani CCM this is too much bwana! Mnamdhalilisha mno Mwenyekiti wenu mjue, au mmemchoka?!

20230920_015434.jpg
 
Kuna Jamaa alimtoa mkuku bi mkubwa wake hapa dom nikichoka sana ilikua HIvi mwana ni boda mama mtu wa vyombo tena vya kienyeji kangara Maza alipata mchongo kilabuni unapewa kitenge na wanzuki kesho mkutanoni kazi ni kugaragara na kushukuru hahahha wana wakaja kumshtua mama yake yuko anagaragara mkutanoni kwenda kumchukua yuko bwiii balaa.
 
Kuna Jamaa alimtoa mkuku bi mkubwa wake hapa dom nikichoka sana ilikua HIvi mwana ni boda mama mtu wa vyombo tena vya kienyeji kangara Maza alipata mchongo kilabuni unapewa kitenge na wanzuki kesho mkutanoni kazi ni kugaragara na kushukuru hahahha wana wakaja kumshtua mama yake yuko anagaragara mkutanoni kwenda kumchukua yuko bwiii balaaa
Wana wakaja kumshtua mama yake yuko anagaragara mkutanoni kwenda kumchukua yuko bwiii balaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom