Kangaroo Courts - Muendelezo wa Maigizo (Nchi haiendeshwi kwenye Luninga)

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
12,496
19,533
Kinachoendelea inabidi kifanyike kuanzia ngazi ya mtaa kwa wanajamii, Kinachoendelea inabidi kifanywe na wabunge majimboni kwao kwa kukusanya kero za wananchi,

Kinachoendelea kufanywa na CCM sioni tatizo sababu ni propaganda na kampeni na watanzania wanapenda matukio (kwahio haya maigizo huenda ni entertainment kwa watu) ingawa athari zake kubwa za haraka ni mbili:-
  • Kutumia kodi zetu (ruzuku) kwa maigizo ambayo huenda hayana tija ya moja kwa moja kwa mwananchi..., (hivyo huenda tunavipa hivi vyama pesa nyingi ambazo wanaweza kuzitumia kwa ulaghai
  • Pili watumishi / watendaji wanaoitwa pale na kuhojiwa kwa haraka huenda isiwe haki kwao.., au wale ambao wanaitwa wezi bila kupewa muda wa kujitetea hio huenda ikawa slander....
Narudia mikutano kama hio ni muhimu kukusanya Kero na kufikisha Kero ila sio kitu cha zima moto cha kufanya kwa siku moja au masaa kadhaa..., Na kuhukumu watu Kwamba huyu ni Jambazi au kusikiliza Kero ambazo huenda ziko mahakamani ni Kama kuwa na Mbwa ambaye hana Meno (anapika kelele ila hawezi kungata) ila ndio hivyo huenda kelele hizo ni mziki kwa wengine, ila ni mziki wenye gharama kubwa kuliko faida
 
Back
Top Bottom