Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,883
- 2,765
Ndugu yangu we hacha tu. Hutaumia bure hukihanza kufikiliha ayo wanayoyafanya ao ndugu zetu. Hangalia hau sikiliza alafu hachana naho. Uwazezi ao! Wanachafuha lugha yetu, hambapo kizazi kijacho kitarithi iyo lafudhi.
wasanii wetu hasa wa bongo fleva huwa wakati mwingine wana nyimbo nzuri sana sema tatizo ni matamshi ya maneno katika nyimbo hizo. hili nadhani linachangiwa na lahaja na kiwango cha elimu pia. mfano kuna wimbo mmoja wa juma necha 'usicheze mbali unga robo' ni wimbo mzuri sema 'kaharibu ile mbaya. kuna sehemu anaongea, "hari ii itakwisha rini?" (hali hii itakwisha lini?) yaani hata hao maproducer hawajui lugha? nani wa kuwanyooshea kiswahili hawa wasanii?
Hili ni suala la umakini katika perfection inategemea producer mwenyewe ana interest gani.Najua kwa mfano Heartbeat Records ya Chuchu kule Zanzibar inajali sana hili suala la lugha na binafsi nimewahi kuwa na mazungumzo naye na alichokua anasisitiza ni ule umahiri wa artist kumudu lugha - kama ni kiswahili basi kiwe kiswahili kweli na kama ni kiingereza hivyohivyo.Siyo kuchanganya lafudhi ya kiswahili kwenye kiingereza na vice versa.Pia utamkaji wa maneno.Labda kuna haja ya kuwakosoa hao producers ili wawe makini zaidi.Fikiria kama wahariri wa makala/vitabu nao wasingekuwa makini kwenye kazi zao ingekuwaje.Suala la quality control ni tatizo kila nyanja TZ.
kwa zenji nakubali kuwa wako makini kwani tanzania yote tunafuata kiswahili chao, yaani ile lahaja. kwa bara nadani maproduce ni kama wasanii wao tu. wanachojali ni mshiko bila kujua wanaua lugha ya kiswahili. itafika wakati wakenya watasema kiswahili kimeanzia kwao kama wanavyotudhulumu na mlima wetu na tanzanite yetu!
Hiyo asavali, na mitusi wanayoimba jumlisha na kuisifia kasumba aka ndumu aka majani aka bangi? na ulevi na mikasi kazi kweli kweli
Ningependa kujua kama Nature alikosea au amefanya makusudi.Wasanii dunia nzima hupewa "artists license" ku-deviate toka vitu vya kawaida.
Granted ukiimba Opera au some other "proper" form of art, watu watategemea uwe proper.But the very essence of hip hop, and hence bongoflava, ni rebellion na kutengeneza a sub-culture.Kwa hiyo inawezekana alikuwa anawabeza watu wakuja, inawezekana alikuwa "anaweka msisitizo", inawezekana amekosea kweli lakini ndiyo kioo cha jamii yenyewe, na pengine lugha ya kiswahili ni wakati ikue na ku adapt jinsi watu wanavyoongea na si kuwalazimisha watu kuongea lugha ambayo si hai.
Moreover, kwa kawaida, kama kuna ku-mix li na ri katika kiswahili, watu wa pwani hu default kwenye li wakati watu wa bara hu default kwenye ri, nitashangaa kama Nature, ambaye kwa kadili ninavyofahamu ni mtu wa pwani, amekosea na kuweka ri kwenye li, it will be counter to the norm.
Hata ukiangalia kiingereza cha enzi za Shakepeare, Victoria na Dickens ni tofauti sana na cha sasa hivi, one only has to look at the King James version of the bible and see how obsolete some of the words and spelling have become.Kwa hiyo kama kosa linafanywa na watu wengi vya kutosha linaacha kuwa kosa na kuwa ndiyo standard mpya, watu ndio wanafanya lugha, lugha haifanyi watu.Kiswahili si Esperanto.
Having said that inabidi tujitahidi sana kutumia Kiswahili fasaha na kuondoa makosa yasiyo lazima.