ni nani atawakemea wasanii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ni nani atawakemea wasanii?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Raia Fulani, May 20, 2009.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  wasanii wetu hasa wa bongo fleva huwa wakati mwingine wana nyimbo nzuri sana sema tatizo ni matamshi ya maneno katika nyimbo hizo. hili nadhani linachangiwa na lahaja na kiwango cha elimu pia. mfano kuna wimbo mmoja wa juma necha 'usicheze mbali unga robo' ni wimbo mzuri sema 'kaharibu ile mbaya. kuna sehemu anaongea, "hari ii itakwisha rini?" (hali hii itakwisha lini?) yaani hata hao maproducer hawajui lugha? nani wa kuwanyooshea kiswahili hawa wasanii?
   
 2. M

  Mwanawani JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndugu yangu we hacha tu. Hutaumia bure hukihanza kufikiliha ayo wanayoyafanya ao ndugu zetu. Hangalia hau sikiliza alafu hachana naho. Uwazezi ao! Wanachafuha lugha yetu, hambapo kizazi kijacho kitarithi iyo lafudhi.
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  ebwana nawe unahitaji msasa kweli! Au utoe singo tuisikie
   
 4. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mziwanda ngoja niingie studio.... niwarudi hawa vijana by the way sasa hivi beat inakua composed pale sei records tuwaoneshe vijana kuwa great thinkers can do wht they can not do excatly, though they think they are doing it right
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Hili ni suala la umakini katika perfection inategemea producer mwenyewe ana interest gani.Najua kwa mfano Heartbeat Records ya Chuchu kule Zanzibar inajali sana hili suala la lugha na binafsi nimewahi kuwa na mazungumzo naye na alichokua anasisitiza ni ule umahiri wa artist kumudu lugha - kama ni kiswahili basi kiwe kiswahili kweli na kama ni kiingereza hivyohivyo.Siyo kuchanganya lafudhi ya kiswahili kwenye kiingereza na vice versa.Pia utamkaji wa maneno.Labda kuna haja ya kuwakosoa hao producers ili wawe makini zaidi.Fikiria kama wahariri wa makala/vitabu nao wasingekuwa makini kwenye kazi zao ingekuwaje.Suala la quality control ni tatizo kila nyanja TZ.
   
  Last edited: May 22, 2009
 6. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  kwa zenji nakubali kuwa wako makini kwani tanzania yote tunafuata kiswahili chao, yaani ile lahaja. kwa bara nadani maproduce ni kama wasanii wao tu. wanachojali ni mshiko bila kujua wanaua lugha ya kiswahili. itafika wakati wakenya watasema kiswahili kimeanzia kwao kama wanavyotudhulumu na mlima wetu na tanzanite yetu!
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Sijui kama nakubaliana nawe 100% kuhusu kufuata kiswahili cha Zanzibar.Pia sina uhakika na producers wote wa ZNZ kwa maana sijafuatilia kuona kazi za hao wengine.Ila the fact is Heartbeat siyo makini tu kwenye kiswahili bali hata kiingereza - ukipata wasaa sikiliza nyimbo za V2 ( kama ule wa Harusi) ambapo anaimba lugha zote kiswahili na kiingereza utafurahi jinsi lugha zote zilivyonyooka na hii ni kazi ya Chuchu.Kuna producer wa bara pia kama Said Commorien naye sijui ana asili ya ZNZ au Commoro - kazi zake ni safi sana kwenye lugha na arrangement kwa ujumla.
   
 8. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ningependa kujua kama Nature alikosea au amefanya makusudi.Wasanii dunia nzima hupewa "artists license" ku-deviate toka vitu vya kawaida.

  Granted ukiimba Opera au some other "proper" form of art, watu watategemea uwe proper.But the very essence of hip hop, and hence bongoflava, ni rebellion na kutengeneza a sub-culture.Kwa hiyo inawezekana alikuwa anawabeza watu wakuja, inawezekana alikuwa "anaweka msisitizo", inawezekana amekosea kweli lakini ndiyo kioo cha jamii yenyewe, na pengine lugha ya kiswahili ni wakati ikue na ku adapt jinsi watu wanavyoongea na si kuwalazimisha watu kuongea lugha ambayo si hai.

  Moreover, kwa kawaida, kama kuna ku-mix li na ri katika kiswahili, watu wa pwani hu default kwenye li wakati watu wa bara hu default kwenye ri, nitashangaa kama Nature, ambaye kwa kadili ninavyofahamu ni mtu wa pwani, amekosea na kuweka ri kwenye li, it will be counter to the norm.

  Hata ukiangalia kiingereza cha enzi za Shakepeare, Victoria na Dickens ni tofauti sana na cha sasa hivi, one only has to look at the King James version of the bible and see how obsolete some of the words and spelling have become.Kwa hiyo kama kosa linafanywa na watu wengi vya kutosha linaacha kuwa kosa na kuwa ndiyo standard mpya, watu ndio wanafanya lugha, lugha haifanyi watu.Kiswahili si Esperanto.

  Having said that inabidi tujitahidi sana kutumia Kiswahili fasaha na kuondoa makosa yasiyo lazima.
   
  Last edited: May 22, 2009
 9. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Hiyo asavali, na mitusi wanayoimba jumlisha na kuisifia kasumba aka ndumu aka majani aka bangi? na ulevi na mikasi kazi kweli kweli
   
 10. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Sasa na wewe hiyo "asavali" ni kutia msisitizo au?

  Mitusi unaisikia wapi? Kwenye redio au kwenye CD/Tape? Wasanii wanafanya biashara na kama hamna regulation hilo ni tatizo la regulating bodies, hii mitusi kwenye redio haitakiwi, lakini kuna wengine ndiyo wanayoitafuta hiyo na wanaona hip hop/bongoflava bila mitusi ni kama kwaya, ni sehemu ya nilichoongelea juu kuhusu "artists license" na "counter culture".Hii ni sehemu ya uhuru wa kujieleza.

  Kama vipi susia kununua kazi za wasanii wenye mitusi, watapata ujumbe, lakini kuwakataza wasiseme mitusi ni censorship.Ndiyo matatizo ya maendeleo hayo. Kuisifia ndumu wengine wanaweza kukwambia ndumu ndiyo yenyewe, haina addiction ina wa relax na kuwasaidia kiusanii, na inawafanya wasiwe na hamu ya kuingia katika hard drugs, kwa hiyo hii inaweza kuwa campaign ya kichinichini ya kuikubalisha nchi ndumu, halafu italetwa motion bungeni kui legalize kabisa.

  Ulevi na mikasi una sehemu yake vile vile, huwezi kuwa jioni kisomo all day every day, na hata ukiwa hivyo sio kila mtu atakuwa hivyo, watu wanataka kuishi.Na hii holier than thou attitude si nzuri kwa kweli.

  Kila mtu ana tendencies na hizi deadly habits, wasanii peke yao ndio wanoweza kuwa wakweli kuliko hata viongozi wa dini.Angalau kwa hilo tuwakubali kwani wanatuonyesha vijana wetu wanaenda wapi.Tukiwawekea censorship sana tutakosa hata barometer ya kujua nini kinaendelea, hususan kwa sababu nchi yetu haina umeme, sembuse simu na Gallop poll.
   
 11. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  hapo umechemsha. ina maana kwa vile umalaya uko kila sehem basi tuuhalalishe? au rushwa? ukweli ni kuwa hawa madogo wanatakiwa kurekebishwa. wakitaka basi waimbe kwa lugha za kwo tujue moja. tatizo hili limeanzia shule ya msingi kwenye somo la imla. sasa inaonekana wengi hapo walishindwa. tazama miziki ya dansi na taarab na mingine. hakuna huu upuuzi
   
Loading...