Ni nani atamrithi Prof. Mukandala UDSM?

Hiyo nafasi siku zote ni lazima ishikiliwe mtu ambaye kwanza ni kada mtiifu wa CCM; manbo ya umahiri katika usimamizi wa utoaji taaluma na kufanya tafiti siyo muhimu sana.

Baada ya Pius Msekwa kutoka UDSM (kama VC) katikati ya miaka ya 70, aliteuliwa kuwa katibu mtendaji wa CCM na nafasi yake ikachukuliwa na Ibrahim Kaduma ambaye kabla alikuwa waziri wa mambo ya nje. Kaduma alifuatiliwa na Nicolaos Kuhanga ambaye kabla alikuwa waziri wa elimu. Prof Goefrey Mmari alimrithi kwa muda mfupi sana Kuhanga kabla hajaondolewa kutokana na "kutokuweka maslahi ya chama mbele chuoni".

Mmari alifuatiwa na "makada shupavu" Prof Mettew Luhanga na hatimaye Mukandala. Miaka ya 80 mwanzoni Mukandala alikuwa mwenyekiti wa CCM tawi la UDSM.

Wakati Pius Msekwa akiwa bado VC UDSM, ndipo alipoandika kitabu "Towards Party Supremacy"; na mawazo yake kwenye hiki kitabu yalitumika sana katika kuandaa mpango wa kuifanya CCM ishike hatamu za dola na uongozi wa nchi (chama dola). Huu uchama dola wa CCM ulihalalishwa kikatiba na bado unaendelezwa chini ya katiba ya sasa.
 
Watushirikishe alumns tuchangie mawazo kuhusu mwenye weledi wa kusogeza chuo chetu mbele. Haya mambo ya wanasiasa kutuchagulia viongozi wa taasisi nyeti kama UDSM yameshapitwa na wakati. Au watangaze kabisa watu washindane na atakayefaulu vigezo husika ndo ateuliwe na Rais.
Huo utaratibu umeanza lini? Tuiachieni mamlaka ya uteuzi ifanye kazi yake jamani!!
 
Prof. Kitila Mkumbo ni chaguo sahihi kwa wakati huu!! Huyu anajitambua sio kama hao akina B na B.
 
kila la heri wana Vyuo Vikuu, maana UDOM na Ardhi nako wakuu wamemaliza muda wao, ni zamu ya damu changa sasa kutamalaki.
 
Tunahitaji watu makini ili angalau wanetu waje kufaidi matunda ya uwekezaji mkubwa katika elimu ya cchuo kikuu.
 
atakayepandisha vyuo vikuu vyetu kwenye ngazi za kimataifa (World's universities Rankings mithili ya HARVARD ama OXFORD).
 
Back
Top Bottom