Ni nani atakuwa Waziri Mkuu Mpya!

Tupunguze hisia wakuu, mbona tunakuwa kama hatuijui nchi yetu!?
Kinachoendelea dodoma ni igizo la wabunge wa ccm kutaka kuwahadaa wananchi wajinga ili waone bado ccm ni chama chao na kwamba wabunge wa ccm pia wanajua kubwata!
Hamna wa kuangusha serikali pale, tunachokitaka toka kwa wabunge wa ccm ni kikubwa kuliko uwezo wao wa kutenda kwa mazoea!
Sisi tulioelevuka japo kidogo tukianza kulewa hisia utafikiri kinachotokea bungeni ni kipya sana ndo tutawayumbisha masikini wengine kuona uh kumbe hata wabunge wa ccm wanafanya kazi wakati hamna chochote walichofanya mpaka sasa.
Tuwaangalie mwisho wao kwanza
Mkuu, nakubaliana na wewe kuwa serikali haitaanguka, lakini kinachoendelea hapa Dodoma si mchezo wa kuigiza hata kidogo. Nilichokibaini baada ya kufuatilia kwa karibu kuwa tunayoyashuhudia ni matokeo ya makundi ambayo CCM ilishindwa kuyazika. Wapo wabunge ambao kwa dhati kabisa wamedhamiria kuliangusha baraza la mawaziri na serikali nayo, ikiongozwa na Lukuvi, inahaha kuhakikisha hilo halitokei. Tatizo wanalokumbana nalo hao wanaotaka kuiwajibisha serikali ni kuwa mpaka hivi sasa hajapatikana mwenye ujasiri wa kuleta hoja binafsi ya kutokuwa na imani ya baraza la mawazi.
Lakini hata hivyo, kwa kuona kuwa wasipochukua hatua lolote linaweza kutokea, mchana huu CCM imewaita wabunge wake wote kwenye kikao chao. Huko ndani nasikia wamemwambia Pinda amwambie JK afukuze mawaziri kadhaa na mtendaji wa TRA. Kama haiwezekani, basi Pinda ajiuzulu, serikali ivunjike ili iundwe upya. Kikao chao bado kinaendelea na tupo hapa tunafuatilia
 
Hivi magufuri john pombe yuko wapi??? Ni kweli amepata stroke na yuko hospitalini????

Naomba kujuwa kwa sasa niko nje ya tanzania - kikazi


yuko dodoma hospitali amelazwa ICU na sukari yake imepanda sana iko 24 na presha juu huku akisumbuliwa na vichomi pia ubavu wa kushoto.
 
kwa leo msitegemee kitu kikubwa sana toka serikali ya hii..hakuna atakayejiuzuru wala kuwajibishwa....
 
kwa leo hakuna jipya sana kuwa eti waziri mkuu atawajibishwa sana..aliye na wakati mgumu ni waziri wa fedha
 
hata mwaka 2008 hawa wabunge wa ccm waliongea na kutoa povu jingi sana...msihadaike mkadhani kuwa leo wameamua kulinda maslahi ya wananchi
 
Hakuna anayefaa. Rais alivunje Bunge na aitishe uchaguzi mkuu mapema
Hata mwanzo alivunja baraza lakin haikusaidia huo sio muarobain wa matatizo yetu,tunahitaji viongoz na chama imarana wenye uadilifu.
 
Wabunge wa Magamba wanaigiza, spirit waliyonayo sasa nakumbuka kuishuhudia ktk sakata la Ngereja na stil anapeta.
 
Kumbuka yaliyompata Lowasa!

Sidhani kama Pinda hata leo hii ni maarufu kama Lowasa na isitoshe Lowasa alikuwa na mtandao mkubwa!

Pinda wala hakutegemea kupata nafasi hiyo na wala simuoni kuwa na ambitions za kwenda juu. Hivyo so far kisha uchinja maana akitoka hapo pension yake ya maisha kama waziri mkuu itakuwa inaingia. Ataendelea kuridhika na ubunge!!
 
Those who are capable to be included in the effective cabinet we are currently not members of Parliament. Thus if His Excellence J Kikwete loves Tanzania he should dissolve the parliament and announce new general election
 
Kwani katika Tanzania ya Sasa hiki cheo kinahitaji sana? Kama Rais anaweza kufanya maamuzi yote, mawaziri wanaweza kusimamia wizara zao, makamu wa Rais anaweza kumshauri Rais, Waziri Mkuu ana kazi gani za Maana??? Ni kuongeza gharama za serikali hiki cheo kifutwe tu!!! Hakina kazi, kama Bungeni mwanasheria Mkuu akasimamie shughuli za serikali.
 
Hamna lolote. kwa kutumia neno la Tundu Lissu: Yanayoendelea bungeni sasa ni "circus"
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom