Ni namna ipi nzuri ya kutoa fungu la kumi?

Zaka na fungu la kumi ni sawa/kitu kimoja?

Kiwango kilipangwa na watu au kimetoka kwenye maandiko?

Naomba kujuzwa
ndio mkuu ni kitu kimoja. tenth au tithes.
ndio 1/10 ya upatacho, unapaswa kumrudishia Mungu ishara ya utii na kumtambua kama yeye ndiye mpaji.
zaka ni sehemu ya kumi (walawi 27:30-32).

Zoezi hilo limeambatana na ahadi tele na Mungu amesema umjaribu.
1)Ameahidi kubariki hata pasiwepo sehemu ya kutosha. Unahaki ya kudai.
2)Atazuia majanga yasikupate wewe na mali zako.
Malaki 3:10,11
 
H
Mkuu hata ukitoa kwa wahitaji ambao wasiojiweza ni sawa tuu.
hapana hili sio sawa fungu la kumi linatolewa kanisani.
ukitoa kwa wahitaji hiyo ni sadaka nyingine na inabaraka zake lakini jukumu la fungu la kumi ni kulijenga kanisa ikiwa ni pamoja na kugharamia ujenzi na uendeshaji wa kanisa na wala si fedha za mchungaji.
 
Fungu la kumi ni Sadaka au sio sadaka ?

Nijibu hilo kwanza

Sent from my GT-I9505 using JamiiForums mobile app
 
aliyeleta andiko kauliza namna nzuri ya kutoa fungu la kumi wengi tumejikita wapi tupeleke fungu la kumi
 
Niseme ukweli....napenda sana kutoa fungu la kumi ila nikikumbuka wapigaji wa church looooh naghairi!

Nimebaki kupeleka kwa watoto yatima tuu
 
mitale na midimu nashukuru umewajibu wadau muswano kutokana na mada hapo juu.
Binafsi napenda na ninajisikia faraja pale ninapo toa fungu la kumi kwa wasio jiweza, wagonjwa, walemavu napia watoto yatima. Zaidi ya hapo, nadhani imani ya dini yako (Msahaf/biblia) pamoja na utashi ni jambo kubwa na muhimu ili kukuongoza kwenye kile unacho kiamini.

Kutoa fungu la kumi ni agizo la agano la kale ikumbukwe hili lilikuwa sharti la kila mwenye kupata zao au mfugo alete sehemu ya kumi ya pato hekaluni (mambo ya walawi 27:30; hesabu 18:26; kumbukumbu la torati 14;24; mambo ya nyakati ya pili 31:5).

Agano jipya halina pahala linazungumzia fungu la kumi. Ila fahamu tu 10th ni biblical
Alafu msijifanye hamna masikio na midomo, maandiko yapo wazi kuhusu utoaji wa Zaka na Sadaka.

Lakini pia mnaojifanya hamsomi 'eti agano jipya halijasema kuhusu utoaji zaka, msijipe unajisi wadau hii hapasoma:
Mathayo 23:1-
Luka 11:42-
Luka 18:12-

NB.
zaka ni kwa ajili ya wachungaji wa mabhabuni siyo vilema na wahitaji ambao haki yao ni sadaka
.
 
Nilivyosema kiwango nilimaanisha 1/10.
Je kimewekwa na watu au?

Na muda wa kutoa zaka/fungu la 10 ni upi?
Haijawekwa na watu hii ni Mungu ametoa mwenyewe

Hakuna muda maalum wa kutoa sababu kuna wafanyabiashara na wafanyakazi hawa mapato yao ni wanayapata tofauti

Kama ni mwaminifu unaweza tumia week nzima kuiombea ndipo ukatoe, kama unaona utakula unapo pata iombee ili usiingie majaribuni uitoe mapema

Sababu ulimwengu wa giza upo na trick sana unaweza pata shida na huna pesa umebakiwa na hiyo hiyo unaweza ukaila

Hakikisha unajiombea hofu ya Mungu ndani yako usile vya Mungu.
 
Nami ndo utaratibu wangu
Binafsi napenda na ninajisikia faraja pale ninapo toa fungu la kumi kwa wasio jiweza, wagonjwa, walemavu napia watoto yatima. Zaidi ya hapo, nadhani imani ya dini yako (Msahaf/biblia) pamoja na utashi ni jambo kubwa na muhimu ili kukuongoza kwenye kile unacho kiamini.
 
Somo la fungu la kumi ama Zaka ni pana sana ,hasa kwa kipindi hiki ambacho mafunuo mengi yanatokea.

Fungu la kumi lina zama tatu ambazo zote,Mungu anazikubali

1. Kuna kipindi cha kabla ya sheria,enzi za akina Adam,Kaini na Abeli,ilikuwa mtu anatoa kwa kujisikia na Mungu alikuwa anaweza kukataa ama kuikubali zaka yako.

2. Kipindi cha pili ni kipindi cha Musa,Ama wana wa Israel..Walitengenezewa Sheria kuhusiana na matoleo ikiwemo na Zaka yenyewe..ambapo ndio lile neno la "leta zaka kamili"linapatikana sababu ilikuwa na kiwango aina ya mtu na nafasi yake.hivyo ilikuwa tayari kuna kiwango.

3.Zama za 3 ni baada ya Kristo kuja hizi ni zama za Neema,hakuja kuitengua torati ila kuitimiliza yaani hakuja kuivunja sheria ila kuitimiza,hapa utoaji unapewa kipaumbele kwa neema,yaani amri kuu tuliyoachiwa "Upendo" ikiwa na maana ukimpenda jirani yako utamsaidia,utamshauri na kufanya vyote kwa huo upendo.hata katika utoaji ukitoa kwa upendo unabarikiwa zaidi,sasa huku kwa ishu ya zaka ni kwamba unatoa kwa jinsi ulivyobarikiwa na kuvuviwa rohoni mwenyewe na Bwana ataipokea na kukubariki kwa kiwango chako,(Nijaribuni katika matoleo) hii ikimaanisha toa kwa moyo na uaminifu nae atakubairikia zaidi.

Sasa senario ya zaka kikanisa kwanza iko tofauti,kulingana na hali na zama zaka imefanywa kuwa pesa ndio zaka,lakini ukiiangalia kwa umakini zaka ni 1/10 ya kazi za mikono yako (mwili wako)...hivyo zaka sio pesa tu kwanza pesa ni matokeo ya kazi za mikono sio kazi ya mikono yako.Kama ni mwalimu fundisha kanisani pia hiyo ni zaka,kama ni mshauri shauri kanisani pia hiyo ni zaka...tenga muda wa kazi inayokuingizia kipato kuifanya kanisani ni zaka yako halisi,lakini kulingana na hali ya maisha na hakuna sheria ya ulawi kanisa limeipeleka sana kwenye pesa ili zisaidie kuhudumia kanisa.

Hivyo usifungwe na zama tuko kipindi cha Neema,toa kwa moyo Mungu atakubariki baraka zako zitaendana na sadaka yako.Lakini pia rohoni ukinuia kuifanya kwa mtindo wa sheria 1/10 ya kazi za mikono pia Bwana atakubariki kwani ni agano lako kwake.

Mbarikiwe na Bwana.
 
Kutoa fungu la kumi ni agizo la agano la kale ikumbukwe hili lilikuwa sharti la kila mwenye kupata zao au mfugo alete sehemu ya kumi ya pato hekaluni (mambo ya walawi 27:30; hesabu 18:26; kumbukumbu la torati 14;24; mambo ya nyakati ya pili 31:5).

Agano jipya halina pahala linazungumzia fungu la kumi. Ila fahamu tu 10th ni biblical

Hata wale wanafunzi walileta 'sehemu' ya walichokuwa nacho...rejea simulizi ya Anania na Safila...nk nk
Anania na safila hao sio wa agano jipya?
 
Nilivyosema kiwango nilimaanisha 1/10.
Je kimewekwa na watu au?

Na muda wa kutoa zaka/fungu la 10 ni upi?
1/10 aliiweka Mungu mwenyewe,ukisoma kitabu cha Mambo ya Walawi utakuta ipo na pia hii iliwekwa sababu walawi walipewa kazi ya kuvitunza vyombo vya Bwana hivyo kabila liliteuliwa ili kuvitunza pamoja na uzao wa Haruni.

Ukisoma hapo utaona kulikuwa na sadaka ya kila kitu,hata unapoenda kutubu,kupatanishwa sadaka zake zilikuwa wazi ili toba yako ipate kibali.
 
Sadaka unaweza kutoa popote, ukampa yoyote...

Fungu la kumi pelekea kanisani au msikitini, hayo ndiyo mapato na matumizi yao...

Cc: mahondaw
 
Fedha au Mali ipo hivi? Ukilipa shuleni inaitwa Ada,kwenye Gari ni nauli,ukimpa Mtu bila kulipia au kukuomba inatwa Zawadi,Ukimsaidi mwitaji inaitwa Msaada/Sadaka na Kadhalika .na Ndivyo ilivyo kwenye Fungu la kumi peleka ka kiongozi wako wa kiroho ww utakuwa umenawa .
 
Jibu lako linaweza kuwa au lisiwe kweli ndugu!
Unaweza pia kuelekezwa na Roho Mtakatifu wapi upeleke fungu la kumi.
Wakati mwingine unaweza elekezwa kupeleka fungu la kumi kwa watumishi wa Mungu wasio na makanisa. Anapokuelekeza Roho Mtakatifu kupeleka ndio mahali sahihi, inaweza kuwa kanisani au la!

Tofautisha kati ya fungu la kumi na sadaka
Sadaka unapeleka popote lakin fungu la kumi linaenda kanisani nyumbani ya bwana biblia ipo wazi kabisa
Kusaidi masikini yatimana vilema iyo ni sadaka siyo fungu la kumi
Fungu la kumi ni kwajir ya wachungaji wapate ela ya kuendesha familia zao na kuendesha injir
Kuendesha injir ni gharama kubwa sana so ndio maana Mungu anataka kuchangia sana injir kuliko kitu chochote coz injir inairajika sana dunia na kuokoa watu kutoka kwny utumwa wa shetani
Ni muhimu sana kuchangia injir coz ata yesu alisema aliwambia masikin sina cha kuwapa zaidi ya neno la uzima nalo litawaweka huru
 
Habari zenu wakuu, hongera kwa kila anayewajibika muda huu pia kwa wanaopumzika katika staili zao wajuazo wao.

Naomba nisivute muda na wakati muhimu kama huu.Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, naomba mjadiliane ni namna gani nzuri ya kutoa fungu la kumi?

Je, ni lazima kanisani, au hata kusaidia watu kwa ile asilimia kumi ni sawa? Na kwanini tunatakiwa kutoa fungu la kumi kanisani.

Sina ushahidi wa namna yoyote ya kutoa fungu la kumi kwa kutumia maandiko ya biblia ila nataka kujua kwa wanaojua tujuzane umuhimu katika kujua namna sahihi ya kumtolea bwana fungu la kumi.

Karibuni wote.
Hakuna haja ya kutoa fungu la kumi iwe kanisani ama msikitini. Fungo lako mpatie yule mwenye shida ama anayehitaji msaada siyo kwa matapeli wa makanisani na misikitini
 
Tofautisha kati ya fungu la kumi na sadaka
Sadaka unapeleka popote lakin fungu la kumi linaenda kanisani nyumbani ya bwana biblia ipo wazi kabisa
Kusaidi masikini yatimana vilema iyo ni sadaka siyo fungu la kumi
Fungu la kumi ni kwajir ya wachungaji wapate ela ya kuendesha familia zao na kuendesha injir
Kuendesha injir ni gharama kubwa sana so ndio maana Mungu anataka kuchangia sana injir kuliko kitu chochote coz injir inairajika sana dunia na kuokoa watu kutoka kwny utumwa wa shetani
Ni muhimu sana kuchangia injir coz ata yesu alisema aliwambia masikin sina cha kuwapa zaidi ya neno la uzima nalo litawaweka huru
Hao ni matapeli tu soyo kuendesha familia ili wanunue train na ndege na magari ya kifahari. UTAPELI MTÙPU
 
Uko sahihi ndugu lakini pia tambua kwamba Mungu anaweza kufanya jambo kupitia taratibu tofauti na zile zilizoandikwa.
Isaya 8:20
"Na waende kwa Sheria na ushuhuda, Ikiwa hawasemi sawa sawa na neno hili, bila shaka kwao hakuna asubuhi"
Taratibu hata kama zikiwa tofauti, haziwezi kupishana na zile ambazo tayari zimeshawekwa na kufafanuliwa faida na hasara zake.
Roho wa Manabii huwatii manabii. 1 wakorintho 14:32.
nadhani kikubwa ni kutii taratibu njema alizoziasisi Mungu. Manabii au watuishi wa Mungu wote tangu mwanzo hadi ufunuo hawapingani, sitegemei atokee roho wa kutuongoza kwenda knyume na kanuni alizoziweka mwenyewe.

Mtazamo wangu lkn mkuu.
 
Back
Top Bottom