Ni namna ipi nzuri ya kutoa fungu la kumi?

Kipanga boy

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,407
1,207
Habari zenu wakuu, hongera kwa kila anayewajibika muda huu pia kwa wanaopumzika katika staili zao wajuazo wao.

Naomba nisivute muda na wakati muhimu kama huu.Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, naomba mjadiliane ni namna gani nzuri ya kutoa fungu la kumi?

Je, ni lazima kanisani, au hata kusaidia watu kwa ile asilimia kumi ni sawa? Na kwanini tunatakiwa kutoa fungu la kumi kanisani.

Sina ushahidi wa namna yoyote ya kutoa fungu la kumi kwa kutumia maandiko ya biblia ila nataka kujua kwa wanaojua tujuzane umuhimu katika kujua namna sahihi ya kumtolea bwana fungu la kumi.

Karibuni wote.
 
peleka fungu la kumi kanisani, watumishi wapate cha kula.
fungu la kumi ni tofauti na sadaka, hiyo unatoa popote.
hata kama wanafuja, Mungu anajua jinsi atakavyowashughulikia ila wewe baraka zao ziko palepale.

malaki 3:10
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
 
Ingia facebook yapo masomo ya fungu la kumi kutoka waalimu mbalimbali na utoaji wake.
Uzoefu wangu ni kuusikiliza moyo wako.
Biblia iko wazi wanaostahili kupewa ila wakati na muda nafsi yako itakusemesha. Wapo watumishi wahitaji kwelikweli.
Yapo makanisa.
Zipo kwaya. Wapo walemavu wanaohitaji viti.
Wapo wagonjwa mahospitalini wa kulipiwa bili, chakula, dawa au nauli.
Wapo yatima wanaotafuta ada za shule.
Wafungwa magerezani wanaotafuta biblia na maandiko wasome.
Wapo watoto waliozaliwa magerezani kwa sababu mama zao walifungwa na mimba zao.
Orodha ni ndefu. Usitoe madhabahuni kama unaona utaumia rohoni kwa jinsi ya watumishi walivyo.
 
Kutoa fungu la kumi ni agizo la agano la kale ikumbukwe hili lilikuwa sharti la kila mwenye kupata zao au mfugo alete sehemu ya kumi ya pato hekaluni (mambo ya walawi 27:30; hesabu 18:26; kumbukumbu la torati 14;24; mambo ya nyakati ya pili 31:5).

Agano jipya halina pahala linazungumzia fungu la kumi. Ila fahamu tu 10th ni biblical

Hata wale wanafunzi walileta 'sehemu' ya walichokuwa nacho...rejea simulizi ya Anania na Safila...nk nk
 
Binafsi napenda na ninajisikia faraja pale ninapo toa fungu la kumi kwa wasio jiweza, wagonjwa, walemavu napia watoto yatima. Zaidi ya hapo, nadhani imani ya dini yako (Msahaf/biblia) pamoja na utashi ni jambo kubwa na muhimu ili kukuongoza kwenye kile unacho kiamini.
 
Habari zenu wakuu, hongera kwa kila anayewajibika muda huu pia kwa wanaopumzika katika staili zao wajuazo wao.

Naomba nisivute muda na wakati muhimu kama huu.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, naomba jadiliane ni namna gani nzuri ya kutoa fungu la kumi?
Je, ni lazima kanisani, au hata kusaidia watu kwa ile asilimia kumi ni sawa? Na kwanini tunatakiwa kutoa fungu la kumi kanisani.

Sina ushahidi wa namna yoyote ya kutoa fungu la kumi kwa kutumia maandiko ya biblia ila nataka kujua kwa wanaojua tujuzane umuhimu katika kujua namna sahihi ya kumtolea bwana Fungu la Kumi.

Karibuni wote.
Somo la matoleo au sadaka limerugwa sana maana ndipo zilipo ofisi za wahusika hapo.

Kifupi kabisa ni kuwa, Mungu amefanya kazi na wanadamu kwa namna nyingi na amekuwa akibadili utaratibu mara kwa mara.

Hapo zamani kabla ya Yesu, wayahudi waliamriwa kutoa matoleo ya namna mbalimbali na kila matoleo yalikuwa na kazi mahususi. Yalikuwepo fungu la kumi, ahadi, malimbuko(mzaliwa wa kwanza wa mwanadamu, mnyama, ndege na mazao) sadaka za unga, za dhabihu na mengine mengi.

Waisrael waliamriwa kutoa yote na ilikuwa amri kutoa yote hayo.

Lakini mara baada ya Yesu kuja, Mungu alimtoa mwanae kuwa sadaka ya pekee ili kuzifuta sadaka nyingi zilizotolewa na waisrael nyakati zile.

Hivyo ni kusema, nyakati za Yesu hakuna fungu la kumi, hakuna zaka, hakuna ahadi, hakuna malimbuko, hakuna sadaka za dhabihu n.k.

Kitu pekee kilichosalia ni michango/sadaka kwa kadri mtu alivyofanikiwa kwa ajili ya kusogeza mbele injili ya Kristo. Imeandikwa katika 1kor16:1-3. Changizo ni kwa ajili ya watakatifu na si vinginevyo.

Na watakatifu inafanyika kwa namna mbili.

1. Wapo tayari watakatifu ambao lazima hukutana kwa ajili ya Bwana. Ili shuguuli mbalimbali za kumwabudu Mungu zifanikiwe, ni changizo ndiyo hutumika. Lakini pia, miongoni mwa watakatifu, iwapo yeyote ana shida, basi kanisa kupitia changizo lapaswa kumsaidia.

2. Namna ya pili ni ya kitume zaidi. Kuwatafta watakatifu zaidi. Kutoa kwa yatima na wajane au yeyote mwenye kuhitaji ni kuhubiri na ni chanzo cha watu kumrudia Mungu. Kufadhili shughuli za uinjilist ndio kazi kubwa tuliyoachiwa.

Kifupi ni kuwa, sisi sote tu makuhani wa Bwana Yesu. Iwapo wote ni makuhani, haipaswi mtu yeyote aishi kwa jasho la mtu mwingine. Inatakiwa kila mtu afanye kazi ya kumpatia kipato ili awe na uwezo wa kumtumikia Mungu kwa nguvu, akili na moyo pia. Siyo kusubiri michango ya waumini kujilipa posho au mishahara.

Imeandikwa, mchungaji wa mshahara, huyo si mchungaji.
 
peleka fungu la kumi kanisani, watumishi wapate cha kule.
fungu la kumi ni tofauti na sadaka, hiyo unatoa popote.
hata kama wanafuja, Mungu anajua jinsi atakavyowashughulikia ila wewe baraka zao ziko palepale.

malaki 3:10
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Siyo zama hizi za Yesu. Kwa Yesu hakuna utapeli huo. Funua kuanzia mathayo hadi ufunuo, hakuna mtu anayepaswa kuishi kwa jasho la mwingine
 
Kutoa fungu la kumi ni agizo la agano la kale ikumbukwe hili lilikuwa sharti la kila mwenye kupata zao au mfugo alete sehemu ya kumi ya pato hekaluni (mambo ya walawi 27:30; hesabu 18:26; kumbukumbu la torati 14;24; mambo ya nyakati ya pili 31:5).

Agano jipya halina pahala linazungumzia fungu la kumi. Ila fahamu tu 10th ni biblical

Hata wale wanafunzi walileta 'sehemu' ya walichokuwa nacho...rejea simulizi ya Anania na Safila...nk nk
Hawakuleta fungu la kumi, ila walileta sehemu ya kufanikiwa kwao. Wakristo yaani wanafunzi wa Yesu hayo mambo hayawahusu kabisa.
 
Ingia facebook yapo masomo ya fungu la kumi kutoka waalimu mbalimbali na utoaji wake.
Uzoefu wangu ni kuusikiliza moyo wako.
Biblia iko wazi wanaostahili kupewa ila wakati na muda nafsi yako itakusemesha. Wapo watumishi wahitaji kwelikweli.
Yapo makanisa.
Zipo kwaya. Wapo walemavu wanaohitaji viti.
Wapo wagonjwa mahospitalini wa kulipiwa bili, chakula, dawa au nauli.
Wapo yatima wanaotafuta ada za shule.
Wafungwa magerezani wanaotafuta biblia na maandiko wasome.
Wapo watoto waliozaliwa magerezani kwa sababu mama zao walifungwa na mimba zao.
Orodha ni ndefu. Usitoe madhabahuni kama unaona utaumia rohoni kwa jinsi ya watumishi walivyo.
nimetaman kuyafanya haya ila kwa mwongozo upi wa biblia
 
Habari zenu wakuu, hongera kwa kila anayewajibika muda huu pia kwa wanaopumzika katika staili zao wajuazo wao.

Naomba nisivute muda na wakati muhimu kama huu.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, naomba jadiliane ni namna gani nzuri ya kutoa fungu la kumi?
Je, ni lazima kanisani, au hata kusaidia watu kwa ile asilimia kumi ni sawa? Na kwanini tunatakiwa kutoa fungu la kumi kanisani.

Sina ushahidi wa namna yoyote ya kutoa fungu la kumi kwa kutumia maandiko ya biblia ila nataka kujua kwa wanaojua tujuzane umuhimu katika kujua namna sahihi ya kumtolea bwana Fungu la Kumi.

Karibuni wote.
Malaki 3:9 leteni zaka kamili ghalani mwangu... Zaka ni kodi hivyo si yako na unapaswa kuirudisha ni tofauti na sadaka, sadaka unaweza kutoa popote ila zaka ni kuirudisha ghalani mwa Bwana
 
Siyo zama hizi za Yesu. Kwa Yesu hakuna utapeli huo. Funua kuanzia mathayo hadi ufunuo, hakuna mtu anayepaswa kuishi kwa jasho la mwingine
Yachunguze maandiko mkuu upate maarifa sahihi .

1 Corintho 9:13,14
"Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekaluni, na wale wahudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu?, Na Bwana vivyohivyo ameamuru (COMMAND) wale waihubirio injili wapate riziki kwa hiyo injili"

Ni agizo la Yesu (Bwana aliyemuamuru paul) hao watu wa injili wale katika injili.
Peleka zaka kanisani, watumishi wapate chakula cha kututumikia mkuu.
Hii inawahusu wale ambao maisha yao 100% wameyatoa kwa ajili ya injili na sio kazi nyingine.
Ikiwa wapo matapeli Mungu ndiiye Muhukumu atawashughulikia.
 
Hawakuleta fungu la kumi, ila walileta sehemu ya kufanikiwa kwao. Wakristo yaani wanafunzi wa Yesu hayo mambo hayawahusu kabisa.
Huwezi kuelewa agano jipya kama huelewi agano la kale mkuu.
inabidi tujifunze kila kitu kichofanyika agano la kale na tujiulize kwa nini vifanyike au visifanyike katika agano JIPYA.
 
peleka fungu la kumi kanisani, watumishi wapate cha kula.
fungu la kumi ni tofauti na sadaka, hiyo unatoa popote.
hata kama wanafuja, Mungu anajua jinsi atakavyowashughulikia ila wewe baraka zao ziko palepale.

malaki 3:10
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Jibu lako linaweza kuwa au lisiwe kweli ndugu!
Unaweza pia kuelekezwa na Roho Mtakatifu wapi upeleke fungu la kumi.
Wakati mwingine unaweza elekezwa kupeleka fungu la kumi kwa watumishi wa Mungu wasio na makanisa. Anapokuelekeza Roho Mtakatifu kupeleka ndio mahali sahihi, inaweza kuwa kanisani au la!
 
Somo la matoleo au sadaka limerugwa sana maana ndipo zilipo ofisi za wahusika hapo.

Kifupi kabisa ni kuwa, Mungu amefanya kazi na wanadamu kwa namna nyingi na amekuwa akibadili utaratibu mara kwa mara.

Hapo zamani kabla ya Yesu, wayahudi waliamriwa kutoa matoleo ya namna mbalimbali na kila matoleo yalikuwa na kazi mahususi. Yalikuwepo fungu la kumi, ahadi, malimbuko(mzaliwa wa kwanza wa mwanadamu, mnyama, ndege na mazao) sadaka za unga, za dhabihu na mengine mengi.

Waisrael waliamriwa kutoa yote na ilikuwa amri kutoa yote hayo.

Lakini mara baada ya Yesu kuja, Mungu alimtoa mwanae kuwa sadaka ya pekee ili kuzifuta sadaka nyingi zilizotolewa na waisrael nyakati zile.

Hivyo ni kusema, nyakati za Yesu hakuna fungu la kumi, hakuna zaka, hakuna ahadi, hakuna malimbuko, hakuna sadaka za dhabihu n.k.

Kitu pekee kilichosalia ni michango/sadaka kwa kadri mtu alivyofanikiwa kwa ajili ya kusogeza mbele injili ya Kristo. Imeandikwa katika 1kor16:1-3. Changizo ni kwa ajili ya watakatifu na si vinginevyo.

Na watakatifu inafanyika kwa namna mbili.

1. Wapo tayari watakatifu ambao lazima hukutana kwa ajili ya Bwana. Ili shuguuli mbalimbali za kumwabudu Mungu zifanikiwe, ni changizo ndiyo hutumika. Lakini pia, miongoni mwa watakatifu, iwapo yeyote ana shida, basi kanisa kupitia changizo lapaswa kumsaidia.

2. Namna ya pili ni ya kitume zaidi. Kuwatafta watakatifu zaidi. Kutoa kwa yatima na wajane au yeyote mwenye kuhitaji ni kuhubiri na ni chanzo cha watu kumrudia Mungu. Kufadhili shughuli za uinjilist ndio kazi kubwa tuliyoachiwa.

Kifupi ni kuwa, sisi sote tu makuhani wa Bwana Yesu. Iwapo wote ni makuhani, haipaswi mtu yeyote aishi kwa jasho la mtu mwingine. Inatakiwa kila mtu afanye kazi ya kumpatia kipato ili awe na uwezo wa kumtumikia Mungu kwa nguvu, akili na moyo pia. Siyo kusubiri michango ya waumini kujilipa posho au mishahara.

Imeandikwa, mchungaji wa mshahara, huyo si mchungaji.
Na kila mwenye ufahamu alijue hili ya kuwa kwa Bwana ni Rehema na Neema sio sadaka
 
Jibu lako linaweza kuwa au lisiwe kweli ndugu!
Unaweza pia kuelekezwa na Roho Mtakatifu wapi upeleke fungu la kumi.
Wakati mwingine unaweza elekezwa kupeleka fungu la kumi kwa watumishi wa Mungu wasio na makanisa. Anapokuelekeza Roho Mtakatifu kupeleka ndio mahali sahihi, inaweza kuwa kanisani au la!
ninamaoni tofauti kidogo.
Roho mtakatifu hawezi kukuongoza kufanya kinyume na vitu ambavyo Mungu tayari ameshavitolea ufafanuzi.
Mungu ni wa utaratibu sio machafuko.
 
Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom