Ni mwaka wa tatu sijapata kitambulisho cha NIDA

Nilijiandikisha NIDA tangu March,2019. Mwaka Jana 2020 nikapata namba, nikaambiwa kitambulisho Bado. Mwaka huu nimefuatilia sana naambiwa tu subiri kikiwa tayari utapigiwa simu. Mbaya zaidi watumishi wa pale wala lugha mbaya sana. Ukiuliza swali kwa ustaarabu wanakujibu kama ugomvi vile. Eti "kama umeshapata namba umefuata nini hapa?"!

Naomba mwenye kujua alternative procedures nipate kadi maana ninashida na kadi na siyo namba.

Ahsante.
Mimi toka 2018 mpaka sasa halafu mtu anasema watu 1.1M hawajachukua vitambulisho wakati ukienda unaambiwa bado kipo kweny process
 
D
Mkuu pole sana, hata mimi kuna kipindi nilikua operator na nilivokuja kujiandikisha pia nilipata wasiwasi sana kupata namba, ila Mungu mkubwa nna namba nangoja kitambulisho tu.
daah!mm nlikuwa nmejiandikisha tayari kwa hyo taarifa zilipoingiliana wakaamua kupiga pin
 
NIDA wenyewe wanakupa control number alafu ndo unaenda kulipia crdb bank. Sawa na ukitaka kurekebisha majina au simu ulioandika NIDA utaratibu ni huo.
Mimi kasoro ipo kwenye umri lakini nasubiri wakati wa kurenew 2024 ndio nikarekebishe sijui napo watatoza?
 
D daah!mm nlikuwa nmejiandikisha tayari kwa hyo taarifa zilipoingiliana wakaamua kupiga pin
Pole mkuu nadhani ni opalerators wengi wamepata hiyo shida, kwa maana hiyo hapo sio wewe tu na kuna wengine wengi ambao uliwasaidia nao watakua wamepigwa pin.
 
Namshukuru Mungu mm nimepata mwezi uliopita nilijiandikisha 2019

Kilichonisaidia mm nilikuwa napiga simu NIDA makao makuu toka mwaka huu mwez wa tano nikawa nawasumbua kila wiki napiga nakuwadanganya kuwa nimepata chuo nje so wanataka ID ya taifa

Mwez wa nane mwanzon nikawapigia wakaniambia mbona kimetoka nenda ofisi yako ya mtaa ulipojiandkikishia

Kweli nilipoenda nikakipata kitambulisho changu

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Namba zao
 
Nilijiandikisha NIDA tangu March,2019. Mwaka Jana 2020 nikapata namba, nikaambiwa kitambulisho Bado. Mwaka huu nimefuatilia sana naambiwa tu subiri kikiwa tayari utapigiwa simu. Mbaya zaidi watumishi wa pale wala lugha mbaya sana. Ukiuliza swali kwa ustaarabu wanakujibu kama ugomvi vile. Eti "kama umeshapata namba umefuata nini hapa?"!

Naomba mwenye kujua alternative procedures nipate kadi maana ninashida na kadi na siyo namba.

Ahsante.
nenda ofisi za kata yako utakuta tiyari, ukikosa nenda nida uwaeleze hali halisi. Wakuambie tatizo ni nini
 
Back
Top Bottom