Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,272
Ninakumbuka familia moja ya Wahindi nikiwa mdogo. Mke na mume wote walikua madaktari wa macho. Walijaliwa kupata watoto wawili wakiume na wa kike. Walikua na clinic yao ya macho kwenye nyumba yao ya ghorofa. Chini ndiyo ilikuwa ofisi na juu waliishi wenyewe.
Niliwafahamu zaidi wale watoto kwakusoma wote tuition jioni. Jumamosi walishinda kwenye ofisi ya wazazi wao wakisaidia shughuli. Baada ya form six wote walikwenda kusomea u daktari Canada.
Yule wa kiume si jui alioa au kutoa mahari lakini huyo mke/mchumba alihamia kwa wakwe akiwa anasoma form five na six. Na yeye alianza kufundishwa kazi Jumamosi. Alikuwa kama mtoto wa familia aliyebaki pale nyumbani.
Sasa hivi yule mtoto wa kiume ndiye daktari wa ile clinic na wana watoto wakubwa pia anawatunza wazee wake.
Nilpenda kuona walivyomuandaa kijana wao na mkwe wao walimlea wenyewe.
Familia nyingi za Kiafrika kwanza biashara ni siri ya Baba. Mradi mnakula, mnavaa na mnasoma msihoji mengine. Pili kuishi na wakwe ni mtihani.