Ni Mh. Lema tena na Mh. Mrisho Gambo hiyo kesho

Ni Mh. Lema tena na Mh. Mrisho Gambo hiyo kesho

Ndiyo maana mimi ni kati ya watu waliofurahia sana uvumi wa kutenguliwa kwa Gambo, kwa sababu anakwamisha maendeleo ya wananchi wa arusha
Acheni uzushi nyie Gambo ndie anayehitajika kwa wana Arusha na sio huyo Lema wenu anayefanya mambo ya kitoto mbele ya wafadhili.
 
subira na Busara zitumike kama alivyoasa Mh. Zitto. Tunaweza kupata Umaarufu sana kwa kutumia Mgogoro huu na Wajinga wakaushangilia lakin mwenye hasara ni Mwananchi wa Kawaida ambae nae sometimes anaweza kuwa miongoni mwa Washangiliaji
Umeongea jambo la msingi sana.
 
Kesho kutakuwepo na kikao cha bodi ya barabara ya mkoa wa Arusha. Wajumbe wa mkutano ni RC, RAS, ma-DC wote, ma-DED wote, Wabunge wote, TANOROADS, NCAA na Wahandisi wa Halmashauri zote.

Kwa utaratibu mwenyekiti wa kikao huwa ni mkuu wa mkoa {by default}, na makamu mwenyekiti anatokana na wabunge.

Hivyo Mwenyekiti atakuwa Gumbo na makamu Mh. Lema

Sipati picha ya kikao
Hakuna tatizo lolote hapo GAMBO ni kiongozi makini
 
Gambo Alichofanya jana ni utoto, na hili la kughushi barua ili kumprempty Rais ni utoto mwingine ili iyonekane ni wapinzani ndo wamefanya hivi..., Huyu jamaa bado ana akili za kitoto mno. Arusha imemshinda
Kwaiyo hajafukuzwa mana iyo barua inasambaa
 
Ishu ni kudanya namna eneo lilivyopatikana, na nani ameshughulika na nini. Si busara kwa kiongozi kuanganyà tenà mbele ya hadhara.
Hata kama alidanganya huwezi kurupuka na kumkanusha mbele ya hadhara....isitoshe ye ndo kiongozi mkubwa na wa juu kabisa kwa Arusha....hii inaonyesha Lema ana chuki za wazi kwa Gambo....!! Inaonesha pia ni mpenda sifa, juhudi za lema zitaonekana tu kwa wana Arusha na wataendelea kumchagua....kupambana na mkuu Wa mkoa hakutamsaidia....
 
Yote uliyoeleza ni hulka za Lema wala io Gambo! Kuleta mradi isiwe Nongwa. Labda atueleze dhumuni la mradi labda ndio tutamuelewA!
Utamuelewa vipi wakati akili yako umei tune kwa Gambo,ila wahisani na wananchi wa Arusha pamoja na watanzania tunaojielewa ndo tumemwelewa Lema
 
hebu kwanza tupeni update ya barabara kutoka tengeru kuna town imefikia wapi? Maana Mara ya mwisho nliwaacha wanarekebisha Mto nduruma pale
Cc Pozzers
 
...cheo kinachotolewa kwa vigezo huombwa kupitia application na hupitia mchakato wa vetting kwa njia ya competition.... Hicho cheo cha huyo RC wa Arusha hakuomba bali kapewa... Na lengo ni kuvuruga upinzani Arusha... Watashindwa...


Cheo kinatolewa kwa vigezo. Ubunge sitaki kusema sana. kwa wale wanaotaka kutumia siasa kujineemesha zama hizi imekula kwao! Go Gambo Go!
 
Kama kawa Gambo
Ukiona adui analialia jua umempa za USO
Wewe usiangalie sura ya mtu

Awe Lema au Mbowe wewe piga kazi tu
 
Na kwa maoni yangu Mkuu asimhamishe Gambo wala kutengua uteuzi labda kama yeye mwenyewe ndiyo akawe RC huko.

Lema aliapa kumdhibiti Gambo kama walivyodhibitiwa machoko Saudia siku moja baada ya Gambo kuapishwa kwa hiyo hata kama atampeleka nani huko,mindset ya Lema ni kwamba kazi ya RC yeyote ni kuhujumu upinzani.

Kumhamisha or kutengua uteuzi wa Gambo ni kuhamasisha hizi figisu majimbo mengine na kumfanya Lema ajione kijogoo.

Kwa hiyo, hiyo hostility spirit ataiendeleza hata kwa atayekuja baada ya Gambo.

Awaache watifuane tu labda kuna siku watapima athari za mgogoro wao kwa wananchi.
 
Lema ndio kadharaulika. Kwa akli yako unadhani kwa nini Wafadhili hawakumuita Lema ndio awe Mgeni Rasmi?!?!?! Jamani naomba CV ya Lema kwanza nimuelewe vizur! maana isije kuwa ni kupoteza muda na nguvu bure!
Ona hili nalo!! Yaani wafadhili ndiyo waliomuita Gambo?? Kwanza wanamjulia wapi? Waache kumjua Lema aliyewatafuta!akawaomba msaada! Aka propose! Akawapokea!na kumtambulisha mugambo kwao ili tu huyo Gambo azindue shughuli hiyo Ndiyo wamjue kiivyo? Yeye mwenyewe hajijui!nani atamjua?
 
hebu kwanza tupeni update ya barabara kutoka tengeru kuna town imefikia wapi? Maana Mara ya mwisho nliwaacha wanarekebisha Mto nduruma pale
Cc Pozzers
Kwa upande wa tengeru barabara tayari ila cha kushangaza ile ya katikati ni pana kuliko hii magari yanayopita ni nyembamba[emoji16][emoji16][emoji16][emoji2][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Ni bahati mbaya kuwa aliyemteua alishasema "Hajaribiwi" na akasisitiza kuwa ukiona adui yako "anapiga kelele" ujue umemkamata kisawasawa!!

Sasa kwa sbb yeye hajaribiwi;na alijiapiza kutokujaribiwa,basi hawezi kukubali "jaribu" hili la watu kutaka amuondoe Gambo Arusha.Na kwa sbb mkuu mwenyewe anaamini mtendaji wake anayezongwazongwa na watu ndio aliyewashika "pabaya" wapinzani,basi hili la Gambo litakuwa linamfurahisha sana,maana kigezo chake cha kwanza kwa mtendaji kuwakamata vizuri wapinzani ni lawama abazopewa.

Halafu tukisimama kwenye madhabahu tunaomba sala na maombi!!!Lkn tunasahau kuwa amri kuu kupita zote ni "Upendo".Tunasahau kuwa msingi wa uongozi si kisasi na fitina,bali HEKIMA na BUSARA.

Hata Mungu alipompa nafasi Suleiman ya kuomba chochote aktakacho,Mfalme Suleiman aliona kimoja tu "HEKIMA"....Akasema,Ee bwana Mungu unipe HEKIMA ili niwaongoze watu wako kwa haki na amani.Hakutaka kuomba majeshi na mali,wala mifugo na mateka,bali HEKIMA.

Inawezekana Mungu angekuwa na wasaa wa kuendelea kuongea na watawala wa dunia ya sasa,wangepewa nafasi ya kuomba,Kuna watu wangesema "Eeee Mungu naomba unisaidie kuwaondoa wapinzani wooote na vyama vyao ili nitawale kwa raha mustarehe.Ipige upofu minara yote na cable internet igome Nchi nzima".Halafu mwisho anageomba wake na masulia wengi zaidi ya marehemu Masabali

Ndio maana Mungu kaamua kwenda mafichoni hadi Leo.watu hawaaminiki.
 
Cheo kinatolewa kwa vigezo. Ubunge sitaki kusema sana. kwa wale wanaotaka kutumia siasa kujineemesha zama hizi imekula kwao! Go Gambo Go!
Acha unafiki vigezo gani vinatumika kutoa vyeo? Hasa cha wakuu wa mikoa?
 
Back
Top Bottom