Ni Mh. Lema tena na Mh. Mrisho Gambo hiyo kesho

Ni Mh. Lema tena na Mh. Mrisho Gambo hiyo kesho

Pozzers

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2013
Posts
337
Reaction score
560
Kesho kutakuwepo na kikao cha bodi ya barabara ya mkoa wa Arusha. Wajumbe wa mkutano ni RC, RAS, ma-DC wote, ma-DED wote, Wabunge wote, TANOROADS, NCAA na Wahandisi wa Halmashauri zote.

Kwa utaratibu mwenyekiti wa kikao huwa ni mkuu wa mkoa {by default}, na makamu mwenyekiti anatokana na wabunge.

Hivyo Mwenyekiti atakuwa Gambo na makamu Mh. Lema

Sipati picha ya kikao
 
Hii ishu ya Lema na Gambo inaudhi na kuchosha sana....Am like
1476882403296.jpg
 
subira na Busara zitumike kama alivyoasa Mh. Zitto. Tunaweza kupata Umaarufu sana kwa kutumia Mgogoro huu na Wajinga wakaushangilia lakin mwenye hasara ni Mwananchi wa Kawaida ambae nae sometimes anaweza kuwa miongoni mwa Washangiliaji
 
Hii ishu imenipita kushoto kweli,kwani ilikuaje maana nyuzi nyingi zinaongelea hospital,magambo na huyo lema
 
Walioweka suala la uzoefu wa kazi unayoajiriwa kwayo hawakuwa wajinga kwani walikuwa na uelewa mpana wa utendaji.
Gambo akae kitako ajitafakari kama hiyo nafasi inamtoshea na ataimudu. Najiuliza,mbona ni kama kila akaapo anavuruga tu badala ya kuongoza ipasavyo? Kama vipi ajiengue tu tukutane jua Kali kijiweni.
 
..Lema hana shida...hata Kama ni kunywa kahawa anaweza Sana....shida iko kwa huyo dogo RC ambae ana madharau kwa wakubwa zake kwasababu ya cheo cha kupewa...hio ndio shida Arusha...
Cheo kinatolewa kwa vigezo. Ubunge sitaki kusema sana. kwa wale wanaotaka kutumia siasa kujineemesha zama hizi imekula kwao! Go Gambo Go!
 
Walioweka suala la uzoefu wa kazi unayoajiriwa kwayo hawakuwa wajinga kwani walikuwa na uelewa mpana wa utendaji.
Gambo akae kitako ajitafakari kama hiyo nafasi inamtoshea na ataimudu. Najiuliza,mbona ni kama kila akaapo anavuruga tu badala ya kuongoza ipasavyo? Kama vipi ajiengue tu tukutane jua Kali kijiweni.
Gambo kapigwa kipayupayu na RC Tibenda kwa jinsi alivyomfitini haiwezekani Mungu akashushia neema katika umri mdogo halafu ukawa mwehu namna hiyo aige kwa mwenziwe Makonda alivyoona hawawezi akina kubenea na Jacob Meya Kinondoni akgeuzia mbinuzake kushirikiana na wakwepa kodi wa zamani Home shopping centre aka GSA wanasema wanarudisha kwa wananchi kufanya vitu vya maendeleo humsikii tena anagombana na mtu wa upinzani
 
Cheo kinatolewa kwa vigezo. Ubunge sitaki kusema sana. kwa wale wanaotaka kutumia siasa kujineemesha zama hizi imekula kwao! Go Gambo Go!
kwa seriklai hii inayotoa vyeo kwa watu wenye matusi kama akina Gambo na Makonda hatushangai ndio maana kudharaurika hakuna command ya serikali kwa sasa nchi inajiendesha tu another lost decade
 
subira na Busara zitumike kama alivyoasa Mh. Zitto. Tunaweza kupata Umaarufu sana kwa kutumia Mgogoro huu na Wajinga wakaushangilia lakin mwenye hasara ni Mwananchi wa Kawaida ambae nae sometimes anaweza kuwa miongoni mwa Washangiliaji

hilo la hasara kwa mwananchi wa kawaida liko wazi kwa ajili ya siasa za kipuuzi kwa ulevi wa madaraka. Hapo tutapata funzo ukiwa madarakani sio sehemu ya kutumia madaraka hayo kwa faida ya chama chako, huo ni upuuzi ukiopita mipaka. Watu wafanye ushawishi wa miaka 6 halafu uje na mtazamo wa itikadi kupuuza waliojitolea kisaidia wananchi!!!
 
Aseeh...itafanyikia wapi mkuu maana nimechoka kuhadithiwa bhana..??
 
kwa seriklai hii inayotoa vyeo kwa watu wenye matusi kama akina Gambo na Makonda hatushangai ndio maana kudharaurika hakuna command ya serikali kwa sasa nchi inajiendesha tu another lost decade
Lema ndio kadharaulika. Kwa akli yako unadhani kwa nini Wafadhili hawakumuita Lema ndio awe Mgeni Rasmi?!?!?! Jamani naomba CV ya Lema kwanza nimuelewe vizur! maana isije kuwa ni kupoteza muda na nguvu bure!
 
Lema atakuwa Dodoma kwenye Kamati za Bunge
 
Ni bahati mbaya kuwa aliyemteua alishasema "Hajaribiwi" na akasisitiza kuwa ukiona adui yako "anapiga kelele" ujue umemkamata kisawasawa!!

Sasa kwa sbb yeye hajaribiwi;na alijiapiza kutokujaribiwa,basi hawezi kukubali "jaribu" hili la watu kutaka amuondoe Gambo Arusha.Na kwa sbb mkuu mwenyewe anaamini mtendaji wake anayezongwazongwa na watu ndio aliyewashika "pabaya" wapinzani,basi hili la Gambo litakuwa linamfurahisha sana,maana kigezo chake cha kwanza kwa mtendaji kuwakamata vizuri wapinzani ni lawama abazopewa.

Halafu tukisimama kwenye madhabahu tunaomba sala na maombi!!!Lkn tunasahau kuwa amri kuu kupita zote ni "Upendo".Tunasahau kuwa msingi wa uongozi si kisasi na fitina,bali HEKIMA na BUSARA.

Hata Mungu alipompa nafasi Suleiman ya kuomba chochote aktakacho,Mfalme Suleiman aliona kimoja tu "HEKIMA"....Akasema,Ee bwana Mungu unipe HEKIMA ili niwaongoze watu wako kwa haki na amani.Hakutaka kuomba majeshi na mali,wala mifugo na mateka,bali HEKIMA.

Inawezekana Mungu angekuwa na wasaa wa kuendelea kuongea na watawala wa dunia ya sasa,wangepewa nafasi ya kuomba,Kuna watu wangesema "Eeee Mungu naomba unisaidie kuwaondoa wapinzani wooote na vyama vyao ili nitawale kwa raha mustarehe.Ipige upofu minara yote na cable internet igome Nchi nzima".Halafu mwisho anageomba wake na masulia wengi zaidi ya marehemu Masabali
 
Back
Top Bottom