Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,997
Hakuna swali lisilojibika. Mtu akijibu "sijui" nalo ni jibu. Kuna maswali na hoja nyingi zimeibuliwa na Lissu kabla ya jaribio la kuuawa dhidi yake na muda wote wa matibabu hadi hivi sasa anapoendelea kutengemaa kiafya. Majibu mbalimbali ambayo yamekuwa yakitolewa ama na vyombo vya dola au wanasiasa wa chama tawala au watendaji mbalimbali yanaonekana ama si ya kuridhisha au yasiyogusa moja kwa moja maswali na hoja za Lissu.
Kwa baadhi yetu tunaomuunga mkono Magufuli baadhi ya majibu haya yanaudhi na yanafanya watu wajiulize kama serikali haina watu wenye uwezo kweli wa kujibu hoja na maswali mbalimbali... hadi hivi sasa ni maswali au hoja gani za Lissu ambazo unaona hazijajibiwa vizuri, kwa usahihi, na hata weledi fulani... na zipi unaona zimejibiwa kisiasa zaidi...
Kumbuka hata jibu la "sijui" nalo ni jibu...
Nataka nione kama ningekuwa mimi katika Usemaji wa Serikali au mtu fulani ambaye anatakiwa kutoa majibu (Polisi, Bunge n.k) ningetoa majibu gani kama mazingira yote yangekuwa ni haya haya...