Ni Maswali Gani Serikali Inapata Shida Kuyajibu kwenye Hoja za Tundu Lissu?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,992
2,000
Hakuna swali lisilojibika. Mtu akijibu "sijui" nalo ni jibu. Kuna maswali na hoja nyingi zimeibuliwa na Lissu kabla ya jaribio la kuuawa dhidi yake na muda wote wa matibabu hadi hivi sasa anapoendelea kutengemaa kiafya. Majibu mbalimbali ambayo yamekuwa yakitolewa ama na vyombo vya dola au wanasiasa wa chama tawala au watendaji mbalimbali yanaonekana ama si ya kuridhisha au yasiyogusa moja kwa moja maswali na hoja za Lissu.

Kwa baadhi yetu tunaomuunga mkono Magufuli baadhi ya majibu haya yanaudhi na yanafanya watu wajiulize kama serikali haina watu wenye uwezo kweli wa kujibu hoja na maswali mbalimbali... hadi hivi sasa ni maswali au hoja gani za Lissu ambazo unaona hazijajibiwa vizuri, kwa usahihi, na hata weledi fulani... na zipi unaona zimejibiwa kisiasa zaidi...

Kumbuka hata jibu la "sijui" nalo ni jibu...

Nataka nione kama ningekuwa mimi katika Usemaji wa Serikali au mtu fulani ambaye anatakiwa kutoa majibu (Polisi, Bunge n.k) ningetoa majibu gani kama mazingira yote yangekuwa ni haya haya...
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
21,587
2,000
Hakuna jibu ambalo Serikali yetu itatoa liliridhishe maadui wa TZ yetu, unamjibu nini mtu anayekwenda foreign media kusema kwamba Raisi Magufuli amempiga risasi, sacrosanct ?

Hakuna jibu lolote litakalokubalika na haijalishi nani au uchunguzi gani umefanyika kama hautasema ,,Raisi Magufuli kampiga Tu ndu Lisu risasi “ sasa kuna haja gani kuwajibu watu ambao tayari wana jibu?

Kwa maoni yangu iko jinsi ilivyo na Tu ndu & Co. fanyeni mnavyotaka kufanya na kama mbwai na iwe mbwai.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
20,085
2,000
..1. Ni nani alitoa maelekezo ulinzi usiwepo area D siku aliyoshambuliwa TL?

2. kwanini serekali ilikataa ombi la familia ya TL kuwashirikisha WACHUNGUZI TOKA NJE ktk suala hili?

3.Kwanini serekali imegoma kutafuta msaada wa Polisi wa Kenya na Ubelgiji ili TL na dereva wake wachukuliwe maelezo?
 
Chrismoris

JF-Expert Member
Oct 27, 2017
13,198
2,000
Jamaa wa MATAGA mbona hawatupi taarifa za Bomberdiers, Dreamliner na Airbus...vipi zile safari za nje ya nchi zimeanza? Tukiwa wadogo niliwahi kusikia story za mtu mwny GUNDU. Eti chochote anachokifanya hakifanikiwi. Sijui Meko ana GUNDU?
 
Imany John

Verified Member
Jul 30, 2011
2,907
2,000
Jamaa wa MATAGA mbona hawatupi taarifa za Bomberdiers, Dreamliner na Airbus...vipi zile safari za nje ya nchi zimeanza? Tukiwa wadogo niliwahi kusikia story za mtu mwny GUNDU. Eti chochote anachokifanya hakifanikiwi. Sijui Meko ana GUNDU?
Mtu mwenye bahati mbaya. (Tafta alfu lela u lela) kazungumzwa humo kwa kirefu.
 
soine

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
1,823
2,000
Hakuna jibu ambalo Serikali yetu itatoa liliridhishe maadui wa TZ yetu, unamjibu nini mtu anayekwenda foreign media kusema kwamba Raisi Magufuli amempiga risasi?[/QUOTE

CCM yangu na serikali yake wamekataa msaada wa vyombo vya nje kusaidia upelelezi, cha ajabu hadi hakuna hata kajibu ka nani anahusika.

Swali linabaki ni wasiojulikana ni akina nani?

Je, lissu kuituhumu serikali yake sio ajabu, hata mimi ningesema hivyo ili nipewe jibu.

Adui kawa adu9
 
nkuwi

JF-Expert Member
Feb 11, 2013
3,956
2,000
..1. Ni nani alitoa maelekezo ulinzi usiwepo area D siku aliyoshambuliwa TL?

2. kwanini serekali ilikataa ombi la familia ya TL kuwashirikisha WACHUNGUZI TOKA NJE ktk suala hili?

3.Kwanini serekali imegoma kutafuta msaada wa Polisi wa Kenya na Ubelgiji ili TL na dereva wake wachukuliwe maelezo?
Swali la nyongeza, CCTV camera Nani aliziondoa baaada ya tukio,?? Kwanini??

Zipo wapi Kwa SASA??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
redio

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
2,114
2,000
Hakuna swali lisilojibika. Mtu akijibu "sijui" nalo ni jibu. Kuna maswali na hoja nyingi zimeibuliwa na Lissu kabla ya jaribio la kuuawa dhidi yake na muda wote wa matibabu hadi hivi sasa anapoendelea kutengemaa kiafya. Majibu mbalimbali ambayo yamekuwa yakitolewa ama na vyombo vya dola au wanasiasa wa chama tawala au watendaji mbalimbali yanaonekana ama si ya kuridhisha au yasiyogusa moja kwa moja maswali na hoja za Lissu.

Kwa baadhi yetu tunaomuunga mkono Magufuli baadhi ya majibu haya yanaudhi na yanafanya watu wajiulize kama serikali haina watu wenye uwezo kweli wa kujibu hoja na maswali mbalimbali... hadi hivi sasa ni maswali au hoja gani za Lissu ambazo unaona hazijajibiwa vizuri, kwa usahihi, na hata weledi fulani... na zipi unaona zimejibiwa kisiasa zaidi...

Kumbuka hata jibu la "sijui" nalo ni jibu...

Nataka nione kama ningekuwa mimi katika Usemaji wa Serikali au mtu fulani ambaye anatakiwa kutoa majibu (Polisi, Bunge n.k) ningetoa majibu gani kama mazingira yote yangekuwa ni haya haya...
Majibu yote kashatoa Mollel.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
7,292
2,000
Hata lile gari lililo kuwa linamfuatilia mpaka ataja namba zake hatukupatiwa majibu ..

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo ndipo maswali yalipoanzia huku kwingine ni blah blah! WAMEJISAHAULISHA WANAPIGA SIASA.
Kinachonishangaza zaidi ni mtoa mada badala ya kusaidiana na wenzake kumjibu TL yeye anawalaumu inamaanisha tunakoelekea WATAWEKA MPIRA KWAPANI
 
UCD

JF-Expert Member
Aug 17, 2012
7,390
2,000
Hakuna swali lisilojibika. Mtu akijibu "sijui" nalo ni jibu. Kuna maswali na hoja nyingi zimeibuliwa na Lissu kabla ya jaribio la kuuawa dhidi yake na muda wote wa matibabu hadi hivi sasa anapoendelea kutengemaa kiafya. Majibu mbalimbali ambayo yamekuwa yakitolewa ama na vyombo vya dola au wanasiasa wa chama tawala au watendaji mbalimbali yanaonekana ama si ya kuridhisha au yasiyogusa moja kwa moja maswali na hoja za Lissu.

Kwa baadhi yetu tunaomuunga mkono Magufuli baadhi ya majibu haya yanaudhi na yanafanya watu wajiulize kama serikali haina watu wenye uwezo kweli wa kujibu hoja na maswali mbalimbali... hadi hivi sasa ni maswali au hoja gani za Lissu ambazo unaona hazijajibiwa vizuri, kwa usahihi, na hata weledi fulani... na zipi unaona zimejibiwa kisiasa zaidi...

Kumbuka hata jibu la "sijui" nalo ni jibu...

Nataka nione kama ningekuwa mimi katika Usemaji wa Serikali au mtu fulani ambaye anatakiwa kutoa majibu (Polisi, Bunge n.k) ningetoa majibu gani kama mazingira yote yangekuwa ni haya haya...
Hoja zingine huhitaji kuzijibu kama hazina mantiki. Halafu ujue zingine ni propaganda tu!
 
dolevaby

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
11,065
2,000
Naongezea swali la 4 kwanini ripoti ya kamati ya ulinzi na usalama ya Bunge ilizuiwa kusoma ripoti yake baada yakufanya uchunguzi na kupangiwa siku yakuisoma
..1. Ni nani alitoa maelekezo ulinzi usiwepo area D siku aliyoshambuliwa TL?

2. kwanini serekali ilikataa ombi la familia ya TL kuwashirikisha WACHUNGUZI TOKA NJE ktk suala hili?

3.Kwanini serekali imegoma kutafuta msaada wa Polisi wa Kenya na Ubelgiji ili TL na dereva wake wachukuliwe maelezo?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom