Ninakumbuka niliupo kuwa shuleni (Sekondari ya kawaida), nilisoma kitabu kinaitwa KUSADIKIKA. Mhusika Mkuu Bw. Karama, alijitolea kwa uzalendo mkubwa ili kuziba pengo lililokuwepo katika jamii. Kwa muda wote alionekana kama ni mtu mwenye matatizo/msumbufu/asiyelipenda taifa lake/mchochezi nk mpaka alipelekwa mahakamani. alipokuwa mahakamani watu wengi wakawa wanamsikitikia kwamba kajitakia mwenyewe, mwishowe akashinda kesi, akaiwezesha Serikali katika masuala ya Sheria na wote (pamoja na Watawala) wakamfurahia.
Nimeikumbuka habari hii kwasababu mimi nimejiunga JF siyo kwa nia ya kuleta uasi dhidi ya Serikali bali kuisaidia Serikali kujadili na kupambanua mambo mbalimbali yanayotokea kwa lengo ya ustawi wa jamii yetu. Ninaamini kwamba, wanaoichukia JF wanakosea kwani sisi tupo wazi kusema na kueleza na kutoa maoni yetu. Tungebaki kimya bila kutoa mawazo yetu tungekuwa hatuna faida kwa taifa letu.
Sielewi msingi hasa wa JF kuchukiwa. Endapo watawala wanaichukia kwa kuwa imefichua siri za EPA, madudu ya ATCL, Richmond nk. basi huyo haitakii mema nchi yetu. Haiingii akilini pale watu wanapo isaidia Serikali kwamba wezi wale pale, na Serikali kugeuza kibao na kuwachukia wanaofichua wezi na kuwakumbatia wezi. Hapa ndipo ninapokosa imani na watawala wetu.