Ni marufuku kufungua mtandao wa JF ukiwa katika ofisi za Serikali

Mugishagwe

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
300
58
Mnyetishaji amenipa habari hizi anasema kuna waraka na uamuzi umeptishwa kwa wakuu wote wa Idara Serikalini na mashirika ya Umma kwamba ukikamatwa uko kwenye mtandao wa JF ukiwa ofisini basi na kazi huna .Nina omba mwenye nyeti zaidi aje atupe ukweli zaidi na sababu ya Serikali kuogopa mtandao huu usitembelewe ila unaweza kutembelea hata mitandao ya ngono ila si JF .
 
Ni kweli nilisikia kuwa mkuu wa mk0a wa Iringa alipiga marufuku muda mrefu tuu kuwa hakuna ruhusa kufungua JF kwa kisingizio kuwa wafanyakazi wanakaa muda mrefu wakisoma nyeti za JF bila kufanya kazi.
 
Wote tuifanyie kazi taarifa hiyo.
Kumbukeni kwa Bongo hata salm Kikwete kisemwa vibaya, anaweza akamua hapo alipo kutia stop na ikaandikwa ni serikali.
 
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa yeye ni Mtaalam wa mambo ya compyuta (bila kukosea shahada yake ya uzamili ni katika mambo ya IT).
Kwa yeye kusema hivyo sio jambo geni kwa tunaomfahamu tangu alipokuwa mkuu wa Wilaya.
Na usishangae ukakuta kuwa naye ni mwana JF.
 
Wote tuifanyie kazi taarifa hiyo.
Kumbukeni kwa Bongo hata salm Kikwete kisemwa vibaya, anaweza akamua hapo alipo kutia stop na ikaandikwa ni serikali.

Mchunguzi .Akisema Mkuu wa Mkoa si Serikali hiyo ?Umesha ambiwa yeye kesha tamka lakini pia idara za Serikali zote na mashirika ya Umma wameambiwa ni marufuku maana wanajua siri za wakubwa wao .Ukikutwa kazi huna .
 
Mnyetishaji amenipa habari hizi anasema kuna waraka na uamuzi umeptishwa kwa wakuu wote wa Idara Serikalini na mashirika ya Umma kwamba ukikamatwa uko kwenye mtandao wa JF ukiwa ofisini basi na kazi huna .Nina omba mwenye nyeti zaidi aje atupe ukweli zaidi na sababu ya Serikali kuogopa mtandao huu usitembelewe ila unaweza kutembelea hata mitandao ya ngono ila si JF .

Kufungua mitandao yote hakuna matatizo! lakini ukifungua JF tu basi kitumbua kimeingia mchanga!!! JF inawatetemesha kweli mafisadi wanahaha huku na kule kufanya kila jinsi ili Watanzania wasijue uovu mkubwa uliojaa kwenye chama cha mafisadi na sirikali na pia kushiriki katika majadiliano ya hatima ya nchi yetu.

Kamwe hawatafanikiwa katika juhudi zao za kuinyamazisha JF na hata wale ambao walikuwa hawatembelei JF sasa watajiuliza kulikoni huku JF hebu na sisi tukajionee. Nawaonea huruma Mawaziri mbali mbali ambao huwa wanajifanya wako busy maofisini mwao kumbe wanapata dose yao ya JF ya kila siku., sasa ama watakuwa wanaondoka mapema ofisini au kuchelewa kuingia ili wapate hiyo dose ya JF. Idumu JF! Idumu.
 
Sizani kama hilo ni kosa hakuna muajiri popote pale duniani atakae kuruhusu ujivinjari mtandaoni muda wako wa kazi sio JF wala MTV , that is no no period!

Kwa hilo sizani kama serikali ina makosa, jamani tuweni makini kabla ya kutoa lawama
 
Mchelea nimekuhabarisha kwamba wanaweza kutembelea tovuti yeyote na si JF wakiwa katika ofisi za Serikali .Sasa hizo zingine ambazo hazijapigwa mkwara hawajaona muda wao wa kazi kwamba unatakiwa ?
 
Mchelea Mwana,
Mbona magazeti yanasomwa ndani ya ofisi za serikali? Tena kwa gharama za serikali. Au bado unaiona komputa kama UFO. internet ni maktaba mbadala na naamini inajenga afya ya kili za wafanyakazi kuliko gazeti la UHURU.

Watu wanasom hata sani na ijuma ofisini!
 
Mimi nafanya kazi serikalini hata hayo magazeti yanamuda wake, na hata hiyo internet sio kila mtu ana access nayo

jamani nyinyi wenzangu mnaishi nchi gani?
 
Mnyetishaji amenipa habari hizi anasema kuna waraka na uamuzi umeptishwa kwa wakuu wote wa Idara Serikalini na mashirika ya Umma kwamba ukikamatwa uko kwenye mtandao wa JF ukiwa ofisini basi na kazi huna .Nina omba mwenye nyeti zaidi aje atupe ukweli zaidi na sababu ya Serikali kuogopa mtandao huu usitembelewe ila unaweza kutembelea hata mitandao ya ngono ila si JF .
Sasa hapo kuna watu wamefunguliwa speed gavana........Siku hizi tunatumia simu kuingia JF na hizo wazikataze basi
 
Ninakumbuka niliupo kuwa shuleni (Sekondari ya kawaida), nilisoma kitabu kinaitwa KUSADIKIKA. Mhusika Mkuu Bw. Karama, alijitolea kwa uzalendo mkubwa ili kuziba pengo lililokuwepo katika jamii. Kwa muda wote alionekana kama ni mtu mwenye matatizo/msumbufu/asiyelipenda taifa lake/mchochezi nk mpaka alipelekwa mahakamani. alipokuwa mahakamani watu wengi wakawa wanamsikitikia kwamba kajitakia mwenyewe, mwishowe akashinda kesi, akaiwezesha Serikali katika masuala ya Sheria na wote (pamoja na Watawala) wakamfurahia.

Nimeikumbuka habari hii kwasababu mimi nimejiunga JF siyo kwa nia ya kuleta uasi dhidi ya Serikali bali kuisaidia Serikali kujadili na kupambanua mambo mbalimbali yanayotokea kwa lengo ya ustawi wa jamii yetu. Ninaamini kwamba, wanaoichukia JF wanakosea kwani sisi tupo wazi kusema na kueleza na kutoa maoni yetu. Tungebaki kimya bila kutoa mawazo yetu tungekuwa hatuna faida kwa taifa letu.

Sielewi msingi hasa wa JF kuchukiwa. Endapo watawala wanaichukia kwa kuwa imefichua siri za EPA, madudu ya ATCL, Richmond nk. basi huyo haitakii mema nchi yetu. Haiingii akilini pale watu wanapo isaidia Serikali kwamba wezi wale pale, na Serikali kugeuza kibao na kuwachukia wanaofichua wezi na kuwakumbatia wezi. Hapa ndipo ninapokosa imani na watawala wetu.
 
Sizani kama hilo ni kosa hakuna muajiri popote pale duniani atakae kuruhusu ujivinjari mtandaoni muda wako wa kazi sio JF wala MTV , that is no no period!

Kwa hilo sizani kama serikali ina makosa, jamani tuweni makini kabla ya kutoa lawama

Hebu soma tena hiyo habari, haikusema mtandao mwingine wowote bali JF. Sasa kama ni kweli wanaweza kuisoma hii thread wa wakerekebisha makosa yao na hivyo onyo likawa kwa mtandao wowote ule with exception ya ule wa chama cha mafisadi....:)
 
Kama wamesema JF pekee wamechemka na wanazidisha kuonyesha jinsi gani JF ni mwiba kwao.
 
Mimi nafanya kazi serikalini hata hayo magazeti yanamuda wake, na hata hiyo internet sio kila mtu ana access nayo

jamani nyinyi wenzangu mnaishi nchi gani?

Mtandao umeingia Tanzania miaka mingi tu, swali la kujiuliza ni kwanini wameamua kufanya hivyo sasa hivi na siyo miaka miwili au mitatu iliyopita na ni kwa nini wameitarget JF pekee (kama ni kweli)? na siyo mitandao mingine yote? Je, ni sawa kuingia mtandao wa CCM lakini ni makosa kuingia mtandao wa JF? Tusubiri hilo tangazo labda litatupa mwanga zaidi juu ya hii issue.
 
Hili jambo mbona lilianza tangu mwezi wa tatu... mlikuwa wapi wenzetu. Tulishalijadili hili na ukawepo mjadala mkubwa tu wa "internet usage policy"...
 
Hili jambo mbona lilianza tangu mwezi wa tatu... mlikuwa wapi wenzetu. Tulishalijadili hili na ukawepo mjadala mkubwa tu wa "internet usage policy"...

Mkuu MJJ,
Nafikiri Internet usage policy ni tofauti na kufungiwa kusoma JF. The later looks very specific. Nafikiri inawezekana ikawepo inter usage policy lakini sio specific kwa JF, o/w hiyo policy itakuwa inafurahisha.

Kama kuna aliye na hiyo policy aibandike ili tuhakiki.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom