Ni mara ngapi huwa unakumbuka kukagua filter hizi za gari yako?

EAPGS

JF-Expert Member
Jun 17, 2021
282
326
Wanajf , nawasalimu.

Leo tena ningependa tukumbushane mambo haya ya msingi kwenye magari yetu.

Ambazo huchangia kwa kiasi kikubwa matumizi makubwa ya mafuta au ya wastani.

Moja kati ya njia ambazo watengenezaji magari walitumia katika suala zima la kuifanya gari itumie mafuta kidogo ama wastani, ni kwa kuruhusu mtiririko bora wa hewa na uwiano wa juu wa hewa kwa mafuta kupitia.

Na moja ya key elements to that improved airflow ni air filter.

Matumizi ya kila siku ya gari yako, yanaweza kusababisha kuzibisha air filter ya gari yako na vumbi ama uchafu.

Inashauriwa, angalau once a month, uzifungue air filter na kuzikagia.

Ikiwa utaikuta na vumbi linaloonekana, unaweza kutumia mpira wenye pressure ( kama ule wa kujazia upepo )
kupulizia ili kuondoa vumbi/uchafu.

Itasaidia kutoa uchafu napia kuboresha mfumo mzima wa hewa.
Na ikiwa ni kubadilisha, baai hakikisha kwamba unabadilisha kulingana na muongozo uliotolewa na manufacture wa aina ya gari unayotumia.

Filter nyingine ya kubadili ama kuiangalia mara kwa mara kwenye gari lako, inayochangia utumiaji mzuri au m'baya wa mafuta ni fuel filter.

Haka ka filter , huzuia uchafu usiweze kufika kwenye Engine ya gari lako na mara nyingi huwa inaziba taratibu taratibu, na kadri kanavyoziba na matumizi ya mafuta kweli huwa yanapungua, na ni jambo jema, sindio mdau eeh!? 😃

Shubiri yake ni pale inapotokea kameziba kabisa. kanaweza kusababisha Engine kuzima ama uchafu kufika kwenye fuel injector za gari yako na mwisho kukusababishia gharama kubwa za matengenezo.

Je, ni mara ngapi huwa unakumbuka kuzikagua filter hizi za gari yako?!


EAPGS
MAFIATI AREA
MBEYA TANZANIA
WHATSAPP ONLY
+255 626 732 244
 
Wengine tuna baiskeli tueleze na sisi namna ya kutunza vyombo vyetu visitumie mafuta mengi.
 
Back
Top Bottom