Ni mapungufu gani ya mkeo/mumeo umeamua kuishi nayo?

Mhakiki

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
2,306
1,993
Wakuuu habari za usiku.

Moja kwa Moja twende kwenye maada. Mimi kwa upande wangu mapungu yafuatayo kutoka kwa mama watoto wangu nimekubali KUISHI NAYO.

1. Kutopokea simu.
Mke wa Mimi hapokei simu hata aione inaita hatashughulika NAYO Hadi amalize shughuli zake. Ukimpigia simu asipopokea usijisumbue kutuma sms, ukituma kuna siku utaisoma mwenyewe.

2. Dawa ya mswaki.
Kwenye matumizi ya hii KITU yeye huminya popote pale.

3. Hajichanganya na WATU.
Yeye ni kazini, nyumbani na kanisani. Haendi tofauti na maeneo hayo labda kwenye mambo ya jamii.

4. Ukimkosea hakuulizi na haoneshi kama amechukia ila utaulizwa siku nyingine na atawasilisha kwa njia ya utani.

5. Akikukosea ukiuliza atakuambia nisamehe baba......... hapo hata uongee vipi hatakujibu.

Hapendi kabisaa kijichanganya na WATU hasa ukitaka umuudhi fika nyumbani anza kumwongelea mtu, hapendi kabisaa na anachukia kwa dhati.

Haya ndio baadhi ya mambo ambayo nimeamua KUISHI NAYO na nimefamikiwa KUISHI NAYO kwa muda wa miaka 19 ya ndoa yetu.
 
Bora wewe unajibiwa asante baba, wengine ni wanabisha hawajakosea na wako sahihi.. 🤣😂

Ukishinda hoja utaambiwa basi yaishe.

Nina mwanangu ana majanga, wakati mwingine unaona hata aibu kumtembelea nyumbani kwake.

Mkewe ana kaujeri kakimya kimya, ukimuona ni mpole lakini ni mjeuri kinoooma, mwanangu anapata tabu saana, kuna muda anafikiria kumuacha.

Mie wangu ni kutaka kujua kila kitu in details, ananiboa saana, chochote kile atataka in details, hata apige simu mtu akuongeleshe atakuuliza nani huyo, ndio yupi. 😂🤣 Unamuliza utamjuaje sasa, hata nikikutajia fulani huwezi kumjua 😂, sijui ni kupenda kuongea na simu au vipi

Hata umpelekee zawadi atataka kujua yoote, kama umekopa, umemnunulia na sh ngapi, unajiuliza we unataka kujua nini, yaani ni shughuli pevu 😂

Kingine anapenda mnoo kuongea na simu, bora muwe karibu hii inasaidia, akiwa mbali anapiga simu ataongea mpaka stori zaitaisha, mie mvivu kubonga na FONI naishia kuweka loudspeaker tu.

Sometimes hana stori, anakupihia anakwambia mwanao anakuita, sasa mtoto Mwenyewe ndio bado hajatimiza mwaka vizuri, kuongea haongei, unajua tu hapa nimemisiwa.

Mengine madogo madogo, yanachangiwa na maisha yangu ya awali.

Elewa neno AWALI. lizingatie vema.
 
Back
Top Bottom