Ni lini Vyeo vya Kijeshi (Collar Insignia) vimebadilishwa hapa nchini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni lini Vyeo vya Kijeshi (Collar Insignia) vimebadilishwa hapa nchini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mnyoofu, Jan 2, 2016.

 1. M

  Mnyoofu Senior Member

  #1
  Jan 2, 2016
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 155
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Wana JF

  Nimeona picha ya Meja General Gaudence Milanzi, aliyeteuliwa na kuapishwa na Rais hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, kwenye blog ya Mpekuzi Huru, ikanipa Maswali.

  Kwenye picha hiyo ( ambayo nimei copy na kupaste hapo chini tena), Major Generali Milanzi, anaonekana kuvaa mabegani COLLAR INSIGNIA yenye mkasi, nyota mbili na ile ngao ya bibi na bwana. Kwa uelewa wangu hicho cheo ni cha Generali Kamili, kama vile Mkuu wa Majeshi aliyepo. Japo kuwa nyota zake zimejipanga tofauti na zile za Generali kamili.

  Kwa ufahamu wangu, Ma- Major Generali wanakuwa na Mkasi na nembo ya Bibi na Bwana tu, je hii picha imechakachuliwa au vyeo vimebadilishwa? Naomba mwenye taarifa atujuze kama "Collar Insignia" za kijeshi zimebadilishwa hapa nchini.  [​IMG]
   
 2. babumapunda

  babumapunda JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2016
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 4,089
  Likes Received: 2,082
  Trophy Points: 280
  za jenerali nyota zake hazijipangi hivo
   
 3. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2016
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 13,050
  Likes Received: 6,804
  Trophy Points: 280
  @Kitulo kwa kuweka kumbukumbu sawa labda ungetoa ufafanuzi hapa ...
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2016
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,762
  Trophy Points: 280
  Ukiondoa cheo cha Private, na vyeo maalum, vyeo vingine vyote vya jeshi la polisi, magereza, uhamiaji, zimamoto na JWTZ, vimegawanyika mafungu matatu matatu ambao vinapisha kwa alama moja moja!.
  Kwa JWZ,


  Jeshi la Wananchi la Tanzania - JWTZ [​IMG]
  Koplo mdogo Koplo Sajenti
  lance corporal corporal sergeant
  [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  Sajenti Mtumishi Maafisa Wateule 2 Maafisa Wateule 1
  Staff Sergeant Warrant officer class 2 Warrant officer class 1
  [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  Luteni wa Pili Luteni wa Kwanza Kapteni
  Second Lieutenant First Lieutenant Captain
  [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  Meja Luteni Kanali Kanali Brigedia Jenerali
  major lieutenant colonel colonel brigadier general
  [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  Meja Jenerali Luteni Jenerali Jenerali
  major general lieutenant general general

  Happy New Year
  Pasco
   
 5. Kitulo

  Kitulo JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2016
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 2,355
  Likes Received: 2,606
  Trophy Points: 280
  vimebadilishwa mwaka 2015.

  hivyo vya Paco ni vya zamani.
   
 6. babumapunda

  babumapunda JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2016
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 4,089
  Likes Received: 2,082
  Trophy Points: 280
  tuwekee vipya mkuu
   
 7. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #7
  Jan 2, 2016
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,069
  Likes Received: 653
  Trophy Points: 280
 8. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2016
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,069
  Likes Received: 653
  Trophy Points: 280
  Tanzania inatumia mfumo huo
   
 9. General Mangi

  General Mangi JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2016
  Joined: Dec 21, 2013
  Messages: 8,571
  Likes Received: 9,532
  Trophy Points: 280
  Bado hujajibu hoja ya muuliza swali, kuhusu Meja jenerali Milanzi?
   
 10. b

  bantu.garage JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2016
  Joined: Oct 13, 2015
  Messages: 1,447
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Wamebadilisha uvaaji wa nyota mabegani uendane na nyota za kwenye magari.Hivyo basi lt.gen atavaa nyota tatu na gen atavaa nne
   
 11. Mtemi mpambalioto

  Mtemi mpambalioto JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2016
  Joined: Aug 23, 2015
  Messages: 808
  Likes Received: 1,026
  Trophy Points: 180
  vyeo vimebadilika wakat nyie mnajiandaa kuzungusha mikono! sasahv general mwamunyange anakuwa na NYOTA NNE mkasi na nembo
   
 12. General Mangi

  General Mangi JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2016
  Joined: Dec 21, 2013
  Messages: 8,571
  Likes Received: 9,532
  Trophy Points: 280
  Tupe mchanganuo wa vyeo vyote
   
 13. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2016
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,277
  Likes Received: 3,860
  Trophy Points: 280
  Mimi mwenye vimenichanganya,labda wameamua kufuata mfumo wa USA ambao Major General na two star general,Lutenant General ni three star general & full general four star general.
   
 14. N

  Nando JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2016
  Joined: Oct 5, 2014
  Messages: 4,894
  Likes Received: 1,543
  Trophy Points: 280
  wanafuata british army.
   
 15. Chakochangu

  Chakochangu JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2016
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 2,346
  Likes Received: 1,413
  Trophy Points: 280
  Wanatumia British system kuanzia chini mpaka Kanali. kuanzia Brigedia kwenda juu ni American.Kuanzia pale walipoanza Brigedia kumpa ujenerali kama miaka kumi iliyopita hivi.
   
 16. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #16
  Jan 2, 2016
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,049
  Likes Received: 2,567
  Trophy Points: 280
  Meja Jenerali James Mwakibolwa mara baada ya kuvishwa cheo kipya na Mkuu wa Majeshi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange hayupo pichani.
   

  Attached Files:

  • 5C.jpg
   5C.jpg
   File size:
   44.8 KB
   Views:
   1,025
 17. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #17
  Jan 2, 2016
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,049
  Likes Received: 2,567
  Trophy Points: 280
  General mwamunyange.
   

  Attached Files:

  • 4 (1).jpg
   4 (1).jpg
   File size:
   74.4 KB
   Views:
   413
  • 4.jpg
   4.jpg
   File size:
   55 KB
   Views:
   427
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Jan 2, 2016
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,762
  Trophy Points: 280
  Vyeo vyote vyote vya jeshi letu viko makundi matano , kila kundi lina maofisa wa ngazi tatu tatu isipokuwa kundi la majeali wao wako ngazi nne, Vyeo vyao katika kila kundi vinapishana kwa ngazi moja moja
  Kundi la Juu ni la maofisa wa Juu, wanaitwa Staff Oficers ambalo ni la majeneali na wako wanne.
  General Jenerali -Mkasi na nyota 4, pia gari yake ina nyota 4, anaitwa A Four-Star General.
  Lieutenant General Luteni Jenerali-Mkasi na nyota 3, pia gari yake ina nyota 3, anaitwa A Three-Star General.
  Major General Meja Jenerali-Mkasi na nyota 2, pia gari yake ina nyota 2, anaitwa A Two-Star General.
  Brigadier General Brigedia Jenerali-Mkasi na nyota 1, pia gari yake ina nyota 1, anaitwa A One-Star General.
  Kundi la Pili kutoka juu ni la maofisa wakuu, wanaitwa Senior Oficers ambalo wako watatu.
  Colonel
  Kanali-Ngao na nyota mbili
  Lieutenant Colonel Luteni Kanali-Ngao na nyota moja
  Major Meja -Ngao
  Kundi la tatu kutoka juu ni la maofisa wa chini, wanaitwa Junior Oficers ambalo wako watatu

  Captain Kapteni-Nyota tatu
  First Lieutenant Luteni-Nyota mbili
  Second Lieutenant Luteni Usu-Nyota moja
  Kundi la nne kutoka juu ni la askari ambao sio maofisa, wa juu, wanaitwa Senior NCOs (Non Commissioned Officers) ambalo wako watatu
  Warrant Officer Class I Afisa Mteule Daraja la Kwanza-Ngao mkononi kama saa
  Warrant Officer Class II Afisa Mteule Daraja la Pili-Mwenge mkononi kama saa
  Staff Sergeant Sajinitaji-Ngao na mbavu tatu
  Kundi la tano na la mwisho ni la askari ambao sio maofisa, wanaitwa Junior NCOs (Non Commissioned Officers) ambalo wako watatu

  Sergeant Sajenti-Mbavu tatu
  Corporal Koplo-Mbavu mbili
  Lance Corporal Koplo Usu-Mbavu moja
  Pasco.
  NB-Pasco baada ya kuhudumu JKT, alijiunga na JWTZ moja kwa moja lakini naomba nisiulizwe lolote kuhusu utumishi wangu jeshini, niliondokaje, na niliondoka na cheo gani, ila vita ikitangazwa leo, mimi ni miongoni mwa wana jf, tutakaokwenda mstari wa mbele!.
   
 19. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #19
  Jan 2, 2016
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,049
  Likes Received: 2,567
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  wacha upotoshaji Marekani genral anavaa Nyota TANO.
   
 20. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #20
  Jan 2, 2016
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,557
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Pasco, asante kwa maelezo. Ila tu kuhusu majina za vyeo>

  Mimi nimekuta orodha hii za vzeo ambazo ni tofauti kidogo upande wa Kiswahili>

  Officer ranks

  General Jenerali
  Lieutenant General Luteni Jenerali
  Major General Meja Jenerali
  Brigadier General Brigedia Jenerali
  Colonel Kanali
  Lieutenant Colonel Luteni Kanali
  Major Meja
  Captain Kapteni
  First Lieutenant Luteni
  Second Lieutenant Luteni Usu


  Enlisted Ranks


  Warrant Officer Class I Afisa Mteule Daraja la Kwanza
  Warrant Officer Class II Afisa Mteule Daraja la Pili
  Staff Sergeant Sajinitaji
  Sergeant Sajenti
  Corporal Koplo
  Lance Corporal Koplo Usu
   
  Last edited: Jan 2, 2016
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...