Ni lini Tanzania itapata Rais, Makamu na Waziri Mkuu wenye mtizamo na mawazo ya kibiashara?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Tanzania inashindwa kuendelea kwa sababu ya kuweka madarakani viongozi wenye damu ya Utumishi wa umma na kushindwa kuweka mchanganyiko wa Watumishi wa umma na wafanyabiashara. Ntatoa mfano kwa awamu zote sita zilizowahi kuwepo kwenye utawala

Historia ya Mwalimu alikuwa Mtumishi wa Umma kwenda kwenye siasa na baada ya Urais, wasaidizi wake nao hivyohivyo. Akaja Mzee Mwinyi na safu yake nayo ikawa Watumishi wa umma

Mzee mkapa alipoingia akaja na Watumishi wa umma akina Mhe.Sumaye na Mhe Gharab Bilal, akakabidhi nchi kwa JK naye pure civil servant pamoja na Mzee Lowasa na Pinda.

JPM akaingia na safu accademician kila sekta na hivyo kila jambo kwao likawa linahitaji principles na urasimu mwingi wakiamini wanaibiwa. Hakuna mindset za kujua risk Ni sehemu ya mfumo wa uendeshaji nchi.

Mhe. Samia ameingia ukiangali safu yake yote Ni wanasiasa na wanataalumu hakuna wafanyabiashara. Na hakuna mtu anashtuka kwanini nivigumu sisi kusonga mbele.

Watumishi wa umma Ni watu wenye mindset za kimaskini (sory to say but that is reality). Watumishi wa umma Ni watu Wana mawazo yakuingia nakutoka ofisini kulingana na muda uliowekwa lakini siyo watu wakuingia kazini kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya mwajiri wake. Ni watu wanaoweza kukata kufanya Jambo flani bila sababu na hakuna wakuwalazimisha kufanya. Kauli mbiu ya Watumishi wa umma Duniani kote ni " HIZI KAZI ZIPO TU NA TUMEZIKUTA CHAKUFIA NINI?" Hii Ni kauli ambayo utolewa na viongozi wa kitaifa wanapokuwa faragha au wanapokaa na watendaji wao wa chini. Kauli namba mbili ya Watumishi wa umma ni USILIE KULIKO MFIWA, kwamba fanya usifanye almradi hakuna athari kwenye mshahara wako Basi nyamaza usipomhudumia atahudumiwa na wengine.

Kinyume chake wafanyabiashara ni watu wameumbwa kutafuta fursa mpya kila siku na kuchukua risk kama sehemu ya kazi yake. Mfanyabiashara anajitathimini amefanikiwa vipi na namna gani anaweza kuvuka hatua kwenda mbele

Sisi Tanzania kukosa wafanyabiashara kwenye mfumo wa uongozi madhara yake nikudumaa kwa akili. Mtu anastaafu katika nafasi kubw nchini lakini uoni mradi wake binafsi anaosimamia, anachoweza nikusubiri Mhe. Rais amteue mwenyekiti wa bodi au mkuu wa taasisi flani Basi. Tungekuwa na wafanyabiashara Leo hii wasingekaa nyumbani baada ya kustaafu wasubiri kuonewa huruma.

Tubadili mfumo tuchanganye wenye mawazo tegemezi (Watumishi) na wasio na mawazo tegemezi wenye uwezo wa kujisimamia (wafanyabiashara)
 
Mtizamo na mawazo ya kibiashara kwenye MFUMO wa mawazo ya kijamaa na wenye kuamini chama na serikali ndio kila kitu haitafurukuta.
 
Mtazamo wa serikali ya JK ulikuwa ni wa kibiashara zaidi,tatizo Tanzania bado tuna hangover ya Ujamaa.
 
Obama hakuwa mfanya biashara, akaiweka marekani pazuri tu, Trump alikuwa mfanyabiashara, akaharibu kabisa. Tanzania tuliwahi kuwa na Rais mchumi (JK), you know what happened, wengine wote naona ni wanakemia, na waalimu, sijui tumewakosea nini waalimu kila mara tunawapata wao tu na uchumi wetu wanaupeleka kiualimu alimu tu.

Kwa kifupi, watu wenye mawazo halisi ya kiuchumi na wenye uwezo kudrvie nchi kiuchumi ni watu wenye uwezo mkubwa sana kielimu na kiutendaji lakini wao huwa hawajikiti kwenye siasa, na kwasababu sio wanasiasa inakuwa ngumu kwao kushika dola, wataendelea kuongozwa na watu wenye uelewa wa chini yao kibiashra siku zote, na hata wakilipwa mshahara wawe washauri wao bado ushauri wao sio binding, unaweza kukalaliwa tu kama ilivyokuwa...., kazi iendelee.
 
Naomba kuuliza swali la kizushi hapa.Hivi Tanzania wafanyabiashara ni wapi au unaweza nipatia japo idadi kama utaweza? au unamanisha na machinga wawe introduced kwenye mfumo wa uongozi
 
Ni pale watanzania watakapo iondoa ccm madarakani iwe kwa nguvu au kwa hiari.
 
Upeo wako ni mdogo sana! CHADEMA kwa zaidi ya robo karne wamashindwa kujenga hata makao makuu ya Chama yenye hadhi! Ije kuwa kujenga Nchi!? Endelea kusugua matako kwenye benchi za Mahakama kufuatilia kesi ya Mbowe huku ukijua CCM is here to stay!
Nipale watanzania watakapo iondoa ccm madarakani iwe kwa nguvu au kwa hiari
 
Back
Top Bottom