Ni lini CCM ilibadilika na kuanza kuwa rafiki wa Waislamu Tanzania?

Status
Not open for further replies.
Ishu iko wazi,mamlaka iliyopo inatafuta njia za kifitina ile iendelee kujificha isionekane mbaya
Wanafanya kila linalowezekana kutumia watu,makundi ya kisiasa na kidini kusambaza fitina na kupotosha uhalisia
Tumeshaona vyama vya siasa vikitumika,tumeshaona UVCCM ikitumika,na tunaona Kundi la waislamu likitumika
Jambo la muhimu kutambua ni kwamba miongoni mwa hao wote hakuna atakayebaki salama na athari za njia wanazotumia,kutafuta suluhu ya kudumu ya matatizo yetu kama taifa kwa njia zinazokubalika ni muhimu sana zaidi ya kuganga njaa ya siku,mwezi au hata miaka michache.
 
Makamba machination.....just to hang on till death...no retirement
 
Wakati mwingine huwa tunafeli mitihani kirahisi kweli!! Maswali yako wazi kabisa na hayana utata lakini majibu mengine yanafanya tuulize kama huwa tunaelewa kinachoulizwa au tunaovershoot katika majibu!
 
1. Chama hakijabadilika, misingi iko the same, ni viongizi ndio wamebadilika. Majina mengi ndani ya chama ni yenye asili ya Arabuni.

2. Kuna uwezekano mkubwa sana wa hao viongozi, kutumia udhaifu, umbumbumbu na umaskini wa ndugu zetu ili kuficha madhambi Yao na kufinisha agenda zao.

3. CUF ambayo ilikuwa kipenzi cha Waislam back then, kimepoteza umaarufu, hence imani yao imepungua.

4. Kwa waislam no matters a lot, chadema chama chenye nguvu, hakina idadi kubwa ya viongozi waislamu

5. Wenzetu, hawana uvumilivu wa imani nyingine, pia wana ubinafsi sana (othering), ndio maana wana majina kama (kafir). Hii ipo pia kwa baadhi ya madhehebu ya kikristu (walokole na wasabato). Hii ni mbaya sana, kwani inatafuta makosa hata kama hayapo.

Hayo ndio maoni yangi
 
MZEE MWANAKIJIJI ME HUWA NAKUBALI SANA MAWAZO YAKO NATAMANI KICHWA CHAKO KINGEKUWA KWANGU. GIV ME SOME TECHNIQUES TO BE LIKE U. WE CAN CHAT THROUGH FACEBOOK VISIT TO mchaga mjanja profile.
 
Mzee mwanakijiji hapa wala hatutakiwi kupoteza muda kufikiria kama CCM imebadilika juu ya masuala ya waislam ama la! Wote tunajua kuwa CCM ni ile ile na iliongeza baya lingine kwa kuchakachua ahadi ya mahakama ya kadhi. Lakini chakujiuliza hapa ni kama hawa wote waopandikiza udini katika siasa zetu wanaelewa madhara yake uko mbele tuendapo?

Kama dini zitakuwa zimeishaingiliwa na ile kitu ya wanasiasa "nipe nikupe" sijui huu ushirika wanaotaka tuamini (Mufti na CCM) utazaa nini huko mbeleni?????

Watawala ni watu wakupita lakini Tanzania ni ya kudumu. Hivyo chonde chonde wanasiasa na nyie watu wa dini kumbukeni sie ni watanzania tunaoishi pamoja bila kuulizana dini zetu!
 
nadhani CDM hawajapenda ku invest kwa waislam

mfano mkubwa ni kuonyesha kuwa hawana interest yoyote na maeneo yenye waislamu wengi kama zanzibar na mikoa ya pwani km lindi na mtwara
labda ndiyo inayowapa wasiwasi waislamu leo kuona ni vizuri wawaunge mkono CCM ambao wanafahamiana vizuri tangu enzi hizo
 
NIKIYAAMINI maneno ya kina Njozi na Said na wengine juu ya udhalimu wa CCM najikuta sina uchaguzi isipokuwa kukubali kuwa matatizo ya Waislamu yamesababishwa na kuchangiwa na CCM.

Haya nijibu.

Mzee,
CCM ilizaliwa 1977 kabla ya hapo kulikuwa na TANU, Mkolononi, TAA nk. lakini wewe unakiri kuwa Waislamu wamedhulumiwa na CCM hivyo unamaana kuwa dhulma hii ilianza baada ya 1977? ok Swali hilo una uamuzi wa kujibu au kuacha!

Ila kuhusu Waislamu na CCM ni kuwa Waislamu wana 3 Options:Kuchagua CCM, CUF au CDM

Kuchagua CHADEMA haiwezekani kwa sababu CDM walimpitisha Padri aliyehusika na Mkataba haramu wa MOI 1992!
Viongozi wa Makanisa kumpigia mgombea wa CDM kampeni ndani ya Makanisa!
Makanisa kutangaza waziwazi kumuunga Mkono mgombea wa CDM na kudai madhambi yake ya ngono ni mambo ya Kibinafsi zaidi!
Chadema kutoweka wazi Sera zake kwa Waislamu nini watawafanyia!

Kuchagua CUF haiwezekani kwa sababu kungegawanya kura za Waislamu hivyo inabidi Waislamu waichague CCM!
Kuchagua CCM ni afadhali zaidi kuliko CDM kwa sababu Waislamu angalau wamepata afueni kipindi cha Kikwete na sera zake za kushugulikia kero za Waislamu wa Tanganyika na wale wa Zanzibar! kinyume na CDM ambayo inaonekana kuungwa mkono na Kanisa na huku wakiwa hawana sera yoyote ya kuwaondolea kero Waislamu!

Any way nimefurahi angalau kupokea maoni yako ya kukiri kuwa Waislamu Tanganyika wamekuwa daraja la pili chini ya CCM ingawaje hujakubali kuwa dhuluma hii ilianza tangu enzi za Ukoloni na kupata nguvu zaidi kipindi cha Nyerere ushahidi soma hapa: ISLAM AND POLITICS IN TANZANIA

Mwisho: kubadilika kwa chama cha siasa sijambo la kushangaza ndio maana tumeona vyama vilivyotawala nchi za Kikomunisti na kubadilisha siasa zao toka ujamaa wa kikomunisti na kujiunga na ubepari na hata CCM iliyokuwa ya Kijamaa tumeshuhudia kubadlika na kuwa ya Kibepari au kufuata siasa nyingine!
Hivyo sioni ajabu CCM kubadilisha Siasa zake dhidi ya Uislamu!!!!
 
Mkuu umelenga iko shida. Sina uhakika kama tumekujibu so far. Lakini na mimi natoa nionavyo mimi: hapa siyo sera wala mabadiliko ndani ya CCM. Waislam wanatumiwa na uongozi wa juu wa CCM ambao wamejikuta hawana hoja za kuujibu upinzani hivyo wanamshika chochote(MFA MAJI) ndiyo maana ukifuatilia mhamasishaji mkubwa wa agenda ya udini ni m.kiti CCM alifanya uzinduzu wa agenda hii ktk hotuba yake ya kuzindua bunge jipya. Sitashangaa baadae waislam wakazinduka na kuanza kuwabana CCM. Madai yao yako palepale sasa wanakatisha daraja na zimwi
 
Kwa bahati mbaya au nzuri wenzetu Waislamu wana sukumwa na hisia zaidi. Sisemi ni kitu kibaya ila ndiyo ukweli na ndicho kinacho sababishwa wenzetu hao kutumika. Leo ukimuambia tu Mwislamu kwamba fulani ni adui wa dini yake hata bila kuchambua atamfanya huyo mtu ni adui yake. Kweli wenzetu wana taka kutuaminisha Waislamu wote wanaendeshwa na Wakristo? Kweli na Waislamu wote waliopo serikali kuanzia ngazi cha chini mpaka juu kabisa (raisi) wana taka kutuaminisha kuwa serikali ina waonea na kuwa pendelea Wakristo? Basi kama ni hivyo ni wao wenyewe Waislamu wanaopendelea Wakristo.
 
nadhani CDM hawajapenda ku invest kwa waislam

mfano mkubwa ni kuonyesha kuwa hawana interest yoyote na maeneo yenye waislamu wengi kama zanzibar na mikoa ya pwani km lindi na mtwara
labda ndiyo inayowapa wasiwasi waislamu leo kuona ni vizuri wawaunge mkono CCM ambao wanafahamiana vizuri tangu enzi hizo
Hakuna sababu ya kuinvest kwa waislamu. Hakuna sababu ya kuinvest kwa wakristo. Kuna sababu ya kuinvest kwa watanzania.
 
Mwanakijiji, naona Kadogoo kishakupa jibu:

Kuchagua CCM ni afadhali zaidi kuliko CDM kwa sababu Waislamu angalau wamepata afueni kipindi cha Kikwete na sera zake za kushugulikia kero za Waislamu wa Tanganyika na wale wa Zanzibar! kinyume na CDM ambayo inaonekana kuungwa mkono na Kanisa na huku wakiwa hawana sera yoyote ya kuwaondolea kero Waislamu!
Tuendelee na mjadala.
 
Swali ni lini tuliacha kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwa Jamhuru wa Muungano wa Wakristo na Waislamu???
 
And when we have Christians,is there going to be any difference in our government or politics generally ? Religious leaders who ought to be preaching tolerance among Tanzanians are even the one creating more divide .Why do people or political parties turn religion for their own selfish interests

WHEN WILL WE AS A PEOPLE learn to judge people on their capacity for true leadership NOT the alliances whether Christian, Muslim.LETS MAKE 2015 A YEAR OF ELECTORAL ACCIDENTS for all the looters, pretenders, bigots, politicians who seek to make us dummies again

History shows that EVERYWHERE IN THE WORLD, religion is a tool used by those craving power to perpetuate themselves closely followed by ethnic bigotry. :embarassed2::embarassed2::embarassed2:

CCM has been Desperate of late to the extent that they use every means at their disposal to ensure that they continue to manipulate Tanzanians.It will not work.They have been in power for ages and still muslim community is backward,nani wa kulaumiwa?
 
Mzee,
CCM ilizaliwa 1977 kabla ya hapo kulikuwa na TANU, Mkolononi, TAA nk. lakini wewe unakiri kuwa Waislamu wamedhulumiwa na CCM hivyo unamaana kuwa dhulma hii ilianza baada ya 1977? ok Swali hilo una uamuzi wa kujibu au kuacha!

Ila kuhusu Waislamu na CCM ni kuwa Waislamu wana 3 Options:Kuchagua CCM, CUF au CDM

Kuchagua CHADEMA haiwezekani kwa sababu CDM walimpitisha Padri aliyehusika na Mkataba haramu wa MOI 1992!
Viongozi wa Makanisa kumpigia mgombea wa CDM kampeni ndani ya Makanisa!
Makanisa kutangaza waziwazi kumuunga Mkono mgombea wa CDM na kudai madhambi yake ya ngono ni mambo ya Kibinafsi zaidi!
Chadema kutoweka wazi Sera zake kwa Waislamu nini watawafanyia!

Kuchagua CUF haiwezekani kwa sababu kungegawanya kura za Waislamu hivyo inabidi Waislamu waichague CCM!
Kuchagua CCM ni afadhali zaidi kuliko CDM kwa sababu Waislamu angalau wamepata afueni kipindi cha Kikwete na sera zake za kushugulikia kero za Waislamu wa Tanganyika na wale wa Zanzibar! kinyume na CDM ambayo inaonekana kuungwa mkono na Kanisa na huku wakiwa hawana sera yoyote ya kuwaondolea kero Waislamu!

Any way nimefurahi angalau kupokea maoni yako ya kukiri kuwa Waislamu Tanganyika wamekuwa daraja la pili chini ya CCM ingawaje hujakubali kuwa dhuluma hii ilianza tangu enzi za Ukoloni na kupata nguvu zaidi kipindi cha Nyerere ushahidi soma hapa: ISLAM AND POLITICS IN TANZANIA

Mwisho: kubadilika kwa chama cha siasa sijambo la kushangaza ndio maana tumeona vyama vilivyotawala nchi za Kikomunisti na kubadilisha siasa zao toka ujamaa wa kikomunisti na kujiunga na ubepari na hata CCM iliyokuwa ya Kijamaa tumeshuhudia kubadlika na kuwa ya Kibepari au kufuata siasa nyingine!
Hivyo sioni ajabu CCM kubadilisha Siasa zake dhidi ya Uislamu!!!!

Yaleyale ya kutofanya utafiti...TANU ndio CCM....Halafu MOI 1992? What is this?....up to 1995 Dr Slaa was with CCM
 
Ndio maana nimesema huwa tunafeli mitihani kirahisi kweli; sijauliza kuhusu kuchaguliwa au kutochaguliwa, sikulinganisha CCM, CUF na Chadema; nimeuliza ni lini CCM ilibadilika na kuwa rafiki ya waislamu? Jibu lako inaonekana ni kuwa ni Kikwete ndiye aliyebadilika na siyo CCM na kuwa akiondoka waislamu wanaweza kurudi na kuwa kinyume na CCM tena? Maana hadi hivi sijaona mahali popote ambapo sera za CCM zimebadilika. Labda kama nakosa kitu.
 
Mimi binafsi huwa sipendi sana kuingia kwenye maswala ya majibishano ya dini, kwani nina ndugu wa dini zote. Lakini vyama vya siasa vimepoteza uzalendo kiasi cha kuacha kujenga utaifa, hata kuanza kutumia dini kwa maslahi binafsi. Mnatuchonanisha na ndugu zetu. kama kuna makosa ndani ya vyama basi kaeni navyo mvijenge katika itikadi ya uzalendo na upendo.

It is a bullship cheap politics kwa kiongozi wa dini kufungamana na chama fulani cha siasa.:gossip:

:angry:
 
Historia ya uislam na maendeleo imekuwapo tokea enzi na enzi. Ukiangalia kwa undani utaona kuwa historia hii inaenda nyuma tokea kabla ya uhuru. Mzee wangu alikuwa akinisimulia kuwa wakati wa Ukoloni shule nyingi zilikuwa zikimiliwa na christian missionaries, sharti moja wapo la kusoma shule hizi lilikuwa ni kushiriki katika misa za kikristo jambo amabalo liliwafanya wazazi wengi waliopo katika madhehbu ya kiislam kuogopa kuwapeleka watoto wao shule za kimisionari, japo evidence leo hii inaonesha kuwa wale waliopelekwa majority walibakia na dini yao ya uislam.

Kutokana na sababu hiyo Taifa baada ya kupata uhuru wasomi wengi waliokuwepo wakati huo ni wale waliohudhuria shule za kimisionari ambazo leo hii baadhi yake ambazo zimebadilishwa majina ni kama vile Tanga School, Mirambo, Tabora School, Minaki, Forodhani etc.

Baada ya uhuru serikali ya TANU ilitakiwa kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha inabadili mitazamo ya wazazi wa kiislam kupeleka watoto wao shule kwani hofu ile ya kubadilishwa dini haikuwepo tena ila TANU haikufanya hivyo(Kosa la kwanza la CCM dhidi ya waislam)

Kwa kutambua kabisa kuwa jamii ya waislam ilikuwa nyuma katika elimu kutokana na historia na kutochukua hatua yoyote ya kuiamsha, ilikuwa ni wazi kabisa kuwa serikali ya TANU/CCM ambayo ilikuwa ikiongozwa na wazomi wengi walio katika madhehbu ya kikristo, ilikuwa ni wazi kuwa CCM kwa makusudi haikutaka kuwainua waislam kwa kuhofia kuwa wanaweza kuja kuwazidi wakristo serikalini na kuigeuza nchi kuwa Taifa la kiislam, na hapo ndiyo dhana ya CCM na kanisa kuwa kitu kimoja ikazidi.(Kosa la pili la CCM dhidi ya waislam)

Katika mfumo wa elimu ilitokea kuwa katika wanafunzi mia wanaofaulu kuendelea kidato cha kwanza basi waislamu hawakuzidi 15, japo shule ya msingi walikuwa ni 50%-50%. Hii inawezekana kabisa ilisababishwa na wazazi wengi wa kiislam kutowasimamia vema vijana wao katika kusoma nyumbani na kuwasisitizia elimu ya madrasa kwa kuwa wao hakupata elimu na kujua umuhimu wake, lakini uvumi ulikuwa ni mkakati uliofanywa na serikali ya CCM wakishirikiana na kanisa kuhakikisha waislam hawavuki kwa wingi kwenda elimu ya juu. CCM ilitakiwa kufanya makusudi kuwahamasisha wazazi ambao wengi wao hawakuhudhuria shule umuhimu wa elimu dunia ila kwa makusudi hakawakufanya hivyo. Moja ya matunda haya tunayaona katika safu kuu ya uongozi wa BAKWATA ambapo sheikh mkuu ni mmoja kati ya wazamiaji wakuu wa elimu ya dini ila wana zero understanding of the world as it should be ndiyo maana wanakuja na matamko ya ahera zaidi ya kidunia katika mambo ya dunia.

CCM na serikali yake inaendelea kuwadhalilisha waislam mbele ya watanzania wengine kwa kutumia wale ambao hawakupata elimu ya kupambanua mbichi na mbivu, kutumia udhaifu wao wa kiuchumi ambao ulisababishwa na CCM yenyewe kwa kuwalubuni kwa hela ili watoe matamko yanayopingana na hali halisi ya maisha yao ili kuiwezesha CCM iendelee kupata ridhaa ya kuendelea kuwakandamiza wao, watoto na wajukuu zao bila wao kujijua?, Ni nani asiyekuwa na kumbukumbu kuwa waislam hawahawa walisakamwa kwa kutumia uhuru wao wa kikatiba kuchagua chama cha kisiasa na wengi wakafurahishwa na sera za CUF, ambapo CCM iliwazushia kila aina ya majina mabaya yakiwemo chama cha kigaidi kwa kuwa wao walikuwa wengi kwenye chama hicho?, ni nani asiyejua kuwa visu(majamvia) ni silaha zenye uhusiano na watu wenye utamaduni wa masharikiri ya kati ambao majority ni waislam, CCM ikawasingizia kuwa CUF chama cha kigaidi (Kwa kuwa walikuwa wanakisupport wengi walikuwa ni waislam) kuwa wameingiza kwa lengo la kufanyia ugaidi?

Kwa ujumla ukiangalia adui mkuu wa maendeleo ya waislam ni CCM na serikali yake ambazo ama kwa makusudi au kwa kutokujua ili wa-ignore waislam mara tu baada ya kupata uhuru na mpaka leo inaendelea kuwa ignore na hata kuwatungia sheria ya ugaidi mara baada ya mashambulizi ya WTC kwa shinikizo la wakubwa. Waislam hawana budi kukaa na kujiuliza maswali yafuatazo

1. Je ni serikali ya Chama gani iliyoua waislam wasiokuwa na hatia pale mwembechai mwaka tarehe 13/2/1998?

2. Je ni serikali ya Chama gani iliyoua waislam kule Zanzibar January 26 na 27 mwaka 2001?

3. Je tokea tupate uhuru ni chama gani kimekuwa madarakani?

Kama majibu ya maswali hayo ni CCM, basi waislam hawana haja ya kukilaumu chama chochote kwa maendeleo yao na uonevu dhidi yao zaidi ya CCM. Na leo hii Muislam kusimama na kuitetea CCM kifua mbele ni kukubali kuwa wale waliouwawa mwenyechai, Unguja na Pemba ambao ni waislam wenzao kuwa ni kweli walikuwa magaidi na walistahili hukumu ile, huu ni unafiki na adhabu ya mnafiki ni fi-nari jehanam
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom