Ni lazima tugawanyike; Lazima tusiwe na umoja! -Yes I said it


Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,898
Likes
8,105
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,898 8,105 280
Mara kwa mara watawala wamekuwa wakituasa kuwa tofauti zetu zisisababishe mgawanyiko katika jamii na kuwa ni muhimu kuendeleza "umoja, utulivu na mshikamano".

Mimi nimeamua kukataa kuwa na umoja wa namna hii! Demokrasia ya kweli inatulazimisha kutofautiana kwa hoja, sera, na hata mitazamo; tofauti hizi zinatusababisha kushindwa kukaa pamoja na kukubaliana. Hivyo, kuna wakati ambapo mgawanyiko siyo tu ni muhimu lakini ni lazima vile vile.

Mgawanyiko tunaouona kula Iran
Mgawanyiko tuliouna kati ya mashabiki wa Bush na Obama
Mgawanyiko kati ya KANU na kina Mwai


Kama tunataka tupige kura inavyopaswa mwaka huu, ni lazima tugawanyike! CCM wanaelewa lugha ya mgawanyiko tu.. ndio maana leo wamekubali kukaa meza moja na CUF kwa sababu Wazanzibari wamegawanyika!!

Bara tunaogopa siasa za "kugawanyika" na hivyo tunalazimishwa kuwa katika umoja wa ulaghai na mshikamano wa uongo; haiwezekani kuwafunga ng'ombe na punda walime pamoja!

Wao wenyewe wanatugawanya sana karibu kila siku; tatizo kuwa tukianza kugawanyika wanashangaa mbona tunagawanyika! Ni kama mambo yale ya "Ukipanda nshale, ukishuka nshale, ukitingishika nshale, usiseme wala usimumunye!! "


Kwanini tunaogopa kugawanyika? je twapaswa kugawanyika? Je mgawanyiko huu ni lazima uwe wa vurugu na mapigano? Je ni ni lazime damu imwagike au tunaweza kugawanyika na kutafuta mwelekeo mpya wa taifa bila ya vurugu, umwagikaji wa damu au uhasama kama ilivyotokea kwenye mataifa mengine?

Je wanaharakati wa ukombozi wa Afrika ya Kusini walikuwa wamoja na utawala wa makaburu - hapana; je wanamapinduzi walioongoza uasi dhidi ya utawala wa Mfalme George wa Uingereza kule Marekani walijaribu kuwa wamoja na ndugu zao ng'ambo ya atlantic? la hasha!

Kugawanyika tunakokupendekeza siyo kugowanyika kunakotokana na chuki binafsi, wivu, husuda au vitu ambavyo kimsingi havina uzito wa hoja. Kugawanyika tunakopendekeza kunatokana na kile wengi wameshakisema hapa yaani "tofauti". Wapo wale wanaotaka tuamini kwamba tofauti zetu zinatuunganisha badala ya kwamba zinatugawanisha.

Unapokuwa na kundi la watu ambao wameweka chama chao mbele kuliko taifa, mgawanyiko ni lazima!

Unapokuwa na kikundi cha watu ambao wanaamini wawekezaji wa kigeni ndio wataleta maendeleo ya taifa letu; mgawanyiko ni lazima!

Unapokuwa na watu wanaoamini kuwa katika taifa zima hakuna mtu mwingine mwenye uwezo wa kuongoza isipokuwa mmoja basi mgawanyiko ni lazima!

Unapokuwa na mfumo wenye kuzalisha utawala wa kifisadi ambapo kundi la watu wachache wamekuwa ni walaji wakuu wa ile keki ya taifa na wengine wakibakia kutamania toka mbali, basi mgawanyiko ni lazima!

Mgawanyiko ninauzungumzia ni kutenganga kiitikadi, kimkakati, kimtazamo, na kimwelekeo wa utatuaji wa matatizo yanayokabili taifa letu. Ni mgawanyiko ambao lengo lake ni kuhakikisha kuwa wanaotawala sasa hawapati nafasi hiyo tena na badala yake kutafuta watawala wengine ambao watakubalina na yale tunayoyapendekeza kama tiba ya matatizo yetu kama taifa. Ni mgawanyiko ambao hauna uwezekano wa upatano, umoja, urafiki, au kwa namna yoyote ile.

Kukubaliana na hilo yaweza kuwa ni group thinking, kutamani jambo hilo hilo laweza kuwa ni group thinking.. but well.. ninapokubaliana na ukweli ambao wengi nao wameukubali siwezi kuomba radhi kwamba tunakubaliana na ukweli huo.

Lakini uzuri wa demokrasia ni kuwa wale wanaopinga na wenyewe wanaweza na wanapaswa kusema kwanini tuungane na kwa nini tusigawanyike mbele ya uovu!.
 
N

Nyauba

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2008
Messages
1,098
Likes
12
Points
135
N

Nyauba

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2008
1,098 12 135
Ni muhimu sana kugawanyika.. Strength in diversity!

Twahitaji sana Kugawanyika..Tunahitaji wapiganaji wanaopigania kugawanyika kwa ajili ya demokrasia yetu.

Kweli twahitaji kugawanyika na WAKATI NDIO HUU..
 
Pearl

Pearl

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2009
Messages
3,042
Likes
46
Points
135
Pearl

Pearl

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2009
3,042 46 135
Kugawanyika ni lazima maana hatuna viongozi waliotayari kututetee sisi kama wananchi wao tena tulio wachagua wneyewe.
kugawanyika lazima viuongozi hawajali maslahi ya nchi wala hawana uruma na wananchi
kugawanyika ni lazima wamezoea kutudanganya hawa,wanadhani bado tuko kule kwenye kutembea peku,na kupandwa na chawa mwili mzima.
Mimi siogopi kugawanyika najua tulishagawanyika kitambo
 
Next Level

Next Level

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2008
Messages
3,158
Likes
22
Points
135
Next Level

Next Level

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2008
3,158 22 135
Mkuu kugawanyika kupi huko unakokusemea hapa? Mbona tulishagawanyika sana mzee? Mshikamano, amani, utulivu unaoimbwa majukwaani ni wa kinadharia zaidi, practically.....hakuna amani hata huku bara!

Tatizo letu bara ni la kukosa sijui niseme political awareness tu! Ni kwambie kitu, wananchi walio wengi ambao huwa hawashiriki kupiga kura kwa mfano....wamejitenga na utawala dharimu, wamekata tamaa, wanamsubiri masihi aje awakomboe.....! kumbe hawa watu wangejua lile box la kupigia kura ndio haswa MASIHI wao, nakwambia wangefurika kwenye vituo vya kupigia kura na kvunja records! Hicho tu ndicho kilichokosekana mkuu!
 
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
198
Points
160
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 198 160
NAKUUNGA MKONO.
kwamba demokrasia yakukubalia kila jambo ili chama ama kundi letu lisiumbuke, ni demokrasia iliopitwa na wakati ambayo haiwezi kututoa hapa tulipo.
Lazima tuwe na mfumo makini wakupingana bila kuogopana, hii italeta msisimko katika uwajibikaji.
kilichopo leo ni kua, wanasiasa wengi wanakubaliana ktk kila jambo, hii inaleta shida sana.
nani alidhani wabunge wa CCM wangeungana na spika wao ktk kuuondo Richmond kwa hoja kwamba serikali imetekeleza baadhi ya maazimio ya bunge.
kulikua na haja gani swala lililoghalimu miaka miwili pesa na muda wetu kuishia juu juu kiasi hiki,. lazima ufumbuzi chanya ilikua upatikane kabla yakufunga rasmi mjadala huo.
sasa kama mpasuko ungekuwa dhahiri ndani ya CCM ndani ya watanzania kweli wasingetucheza shere kwa kiwango hiki.
 
A

Akili Kichwani

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2010
Messages
1,504
Likes
36
Points
145
A

Akili Kichwani

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2010
1,504 36 145
jamani tumechoka na amani?

tumekerwa na utulivu?

tunaomba mapambano?

tutnatamani vita?

huko zanzibar damu ilimwagika, wanofaidi sasa bado ni wanasiasa wachache sana matunda ya ile damu, nao ni mfano, hamadi rashid mohamedi maalim seif, sasa jusa ladhu nk

kenya damu ilimwagika, wanaofaidi matunda ya ile damu ni wachache kama raila, nk.

tunawezaje kuwatamani hawa? wanasiasa wanawatamani lakini watu wa kawaida hata huko walikogawanyika wanawatamani watanzania!!!!!!!!!! pamoja na umbumbumbu wetu.

mwanakijiji wewe unaishi marekani, nami pia kwa sasa naishi nje, kumbuka kuna wenzetu wengi sana huko nyumbani ambao kama tukigawanyika na baada ya kitambo kidogo tukaanza kutwangana basi watakufa hadi waishe!!!!!!!!!

katika lolote linalohusi amani, sitakubali tugawanyike

heri tuwe masikini na kuonekana nwajinga, kuliko kuwa matajiri wajanja wanaouana kwa kuchochewa na wanasiasa.............

Mungu ibariki tanzania
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,898
Likes
8,105
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,898 8,105 280
Ndilo tatizo.. nani kasema tukigawanyika lazima tupigane? Lakini kama kugawanyika ni lazima... yaani tunaogopa hata kupingana na watawala kwa sababu tunaogopa watatumwagia maji ya upupu.. that explains the docility of some people in the opposition camp! Kugawanyika si lazima kupigana!!!
 
C

Calipso

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2009
Messages
284
Likes
2
Points
35
C

Calipso

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2009
284 2 35
kugawanyika ni sababu kuu ya kuelekea ktk maendeleo,na ni changamoto kubwa watawala ktk kuchochea maendeleo,isiwe tumo ktk yaaale, fikra za....
 
N

Nyauba

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2008
Messages
1,098
Likes
12
Points
135
N

Nyauba

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2008
1,098 12 135
Ndilo tatizo.. nani kasema tukigawanyika lazima tupigane? Lakini kama kugawanyika ni lazima... yaani tunaogopa hata kupingana na watawala kwa sababu tunaogopa watatumwagia maji ya upupu.. that explains the docility of some people in the opposition camp! Kugawanyika si lazima kupigana!!!
mepesi mepesi yametuzidi..lol.
 
N

nyakyegi

Member
Joined
Jul 2, 2009
Messages
21
Likes
0
Points
3
N

nyakyegi

Member
Joined Jul 2, 2009
21 0 3
Ndilo tatizo.. nani kasema tukigawanyika lazima tupigane? Lakini kama kugawanyika ni lazima... yaani tunaogopa hata kupingana na watawala kwa sababu tunaogopa watatumwagia maji ya upupu.. that explains the docility of some people in the opposition camp! Kugawanyika si lazima kupigana!!!
yes kugawanyika si kupigana 100% correct. hata familia moja wana mitizamo tofauti na maono tofauti pia. ili kuleta changamoto lazima tugawanyike kwa hoja pia kwa matendo, hii itapelekea msukumo wa kiutendaji kwa serikali regardless nani yuko madarakani kwani atajua asipofanya vizuri lazima atang'oka maana mgawanyiko husababisha watu kutazama mbali zaidi na pia hata waliolala huamka na kujiuliza kuna nini?
 
M

Magezi

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2008
Messages
2,976
Likes
230
Points
160
M

Magezi

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2008
2,976 230 160
jamani tumechoka na amani?

tumekerwa na utulivu?

tunaomba mapambano?

tutnatamani vita?

huko zanzibar damu ilimwagika, wanofaidi sasa bado ni wanasiasa wachache sana matunda ya ile damu, nao ni mfano, hamadi rashid mohamedi maalim seif, sasa jusa ladhu nk

kenya damu ilimwagika, wanaofaidi matunda ya ile damu ni wachache kama raila, nk.

tunawezaje kuwatamani hawa? wanasiasa wanawatamani lakini watu wa kawaida hata huko walikogawanyika wanawatamani watanzania!!!!!!!!!! pamoja na umbumbumbu wetu.

mwanakijiji wewe unaishi marekani, nami pia kwa sasa naishi nje, kumbuka kuna wenzetu wengi sana huko nyumbani ambao kama tukigawanyika na baada ya kitambo kidogo tukaanza kutwangana basi watakufa hadi waishe!!!!!!!!!

katika lolote linalohusi amani, sitakubali tugawanyike

heri tuwe masikini na kuonekana nwajinga, kuliko kuwa matajiri wajanja wanaouana kwa kuchochewa na wanasiasa.............

Mungu ibariki tanzania
Wewe ni muongo hakuna anayetamani ufisadi wa CCM ya Tanzania. Kila binadau anapenda amani na utulivu lakini siyo amaniinayosemwa na CCM.

Haiingii akilini Adrew Chenge ana 1.3 Bilion TZS alafu useme tuko sawa, amani nautulivu,.....hiyo hakuna!!

Waziri Pinda anasimama jukwaani anasema anawashangaa viongozi wa serikali wanapenda magari ya anansa (Landcruiser VX) wakati huo huo yeye akimaliza mkutano anapanda gari la aina hiyo hiyo, huu ni uhuni na upuuzi mkubwa wa CCM.
 
Next Level

Next Level

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2008
Messages
3,158
Likes
22
Points
135
Next Level

Next Level

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2008
3,158 22 135
jamani tumechoka na amani?

tumekerwa na utulivu?

tunaomba mapambano?

tutnatamani vita?

huko zanzibar damu ilimwagika, wanofaidi sasa bado ni wanasiasa wachache sana matunda ya ile damu, nao ni mfano, hamadi rashid mohamedi maalim seif, sasa jusa ladhu nk

kenya damu ilimwagika, wanaofaidi matunda ya ile damu ni wachache kama raila, nk.

tunawezaje kuwatamani hawa? wanasiasa wanawatamani lakini watu wa kawaida hata huko walikogawanyika wanawatamani watanzania!!!!!!!!!! pamoja na umbumbumbu wetu.

mwanakijiji wewe unaishi marekani, nami pia kwa sasa naishi nje, kumbuka kuna wenzetu wengi sana huko nyumbani ambao kama tukigawanyika na baada ya kitambo kidogo tukaanza kutwangana basi watakufa hadi waishe!!!!!!!!!

katika lolote linalohusi amani, sitakubali tugawanyike

heri tuwe masikini na kuonekana nwajinga, kuliko kuwa matajiri wajanja wanaouana kwa kuchochewa na wanasiasa.............

Mungu ibariki tanzania
Braza......u are missing something here! hujaelewa Philosophy nzima ya ''KUGAWANYIKA'' aliyoisema MM hapo juu mkuu!

Hivi, wamarekani walivyoamua kugawanyika na kuwa na camp mbili - Obama vs John M......kulimwagika damu? Umesema upo nje, umeona huko Ukraine kilichotokea juzi, wale jamaa wamemwaga damu kumpata Yonkovich? (sorry spelling)?
 
N

Nyumbu-

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Messages
978
Likes
125
Points
60
N

Nyumbu-

JF-Expert Member
Joined May 26, 2009
978 125 60
Kugawanyika ni muhimu. Hata watawala wetu wanalijua na ndiyo maana wanapinga swala la mgombea binafsi, ili mtu akiwa na mawazo tofauti na yao wamtimue kwenye chama ili akose pa kuongelea.
Hivi kwanini wabunge wanashindwa kulijadili hili la mgombea binafsi? Wanaogopa nini hasa?
 
A

Akili Kichwani

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2010
Messages
1,504
Likes
36
Points
145
A

Akili Kichwani

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2010
1,504 36 145
ni makosa kulinganisha yalitotokea kwinginek duniani na huku kwetu, situation n tofauti sana.

jamani tujadili mambo kwa uhalisia wake,

nipeni mfano wa nchi ya dunia ya atatu huku afrika waliyogawanyika na bado ina amani, hapao tuttaelewana wazee....................
 
M

Magezi

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2008
Messages
2,976
Likes
230
Points
160
M

Magezi

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2008
2,976 230 160
ni makosa kulinganisha yalitotokea kwinginek duniani na huku kwetu, situation n tofauti sana.

jamani tujadili mambo kwa uhalisia wake,

nipeni mfano wa nchi ya dunia ya atatu huku afrika waliyogawanyika na bado ina amani, hapao tuttaelewana wazee....................
Kugawanyika siyo lazima kupigana lakini CCM mnalazimisha kupigana...kwa nini Botswana hawapigani na wanatendeanan haki??
 
M

Magezi

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2008
Messages
2,976
Likes
230
Points
160
M

Magezi

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2008
2,976 230 160
kwa mfano kama Mwanankijiji alivyo sema chanzo cha vurugu zote za zanzibar ni CCM sasa walivyo ona kuwa wazanzibari wanapinga kupigana CCM ikaanza kuona haina bao tena ndo wakaanza choko choko akina chiligati na makamba.
 
Next Level

Next Level

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2008
Messages
3,158
Likes
22
Points
135
Next Level

Next Level

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2008
3,158 22 135
ni makosa kulinganisha yalitotokea kwinginek duniani na huku kwetu, situation n tofauti sana.
Angalia maneno yako hapa chini.....wewe ndio ulioanza kutaja yaliyotokea sehemu nyingine duniani!

huko huko zanzibar damu ilimwagika, wanofaidi sasa bado ni wanasiasa wachache sana matunda ya ile damu, nao ni mfano, hamadi rashid mohamedi maalim seif, sasa jusa ladhu nk

kenya damu ilimwagika, wanaofaidi matunda ya ile damu ni wachache kama raila, zanzibar damu ilimwagika, wanofaidi sasa bado ni wanasiasa wachache sana matunda ya ile damu, nao ni mfano, hamadi rashid mohamedi maalim seif, sasa jusa ladhu nk

nipeni mfano wa nchi ya dunia ya atatu huku afrika waliyogawanyika na bado ina amani, hapao tuttaelewana wazee...................
....tatizo wewe definition ya amani na utulivu sijui unaichukuliaje, na pia Kugawanyika sijui unakuchukuliaje......kugawanyika tunafanya hivyo kifikra, kiitikadi, kisiasa, kimtazamo sio kimabavu mzee!

Wewe ukipigia kura CCM mimi nikapigia CUF, hapa tumegawanyika lakini hatujapigana na kumwaga damu......! I expected kwa kuwa wewe upo nchi za watu zilizoendelea zaidi kidemokrasia, ungekuwa na uelewa mpana zaidi wa dhana hii.....!
 
A

Aspirinminister

Member
Joined
Feb 22, 2009
Messages
15
Likes
0
Points
0
A

Aspirinminister

Member
Joined Feb 22, 2009
15 0 0
Dah! Hizo comments chache za kwanza zilinitisha kidogo...Nimefurahi kugundua kuwa kugawanyika kwa mitizamo ndiko kunakoongelewa hapa. Kama ni hivi, mi nasupport fully ila nafikiri kugawanyika huku kupo tayari tena hivi sasa kumekithiri hata zaidi.

Tuna mgawanyiko kwenye mitizamo ya aina mbali mbali, ukiangalia skendo zote zilizoibuka tangu JK apate urais, ni mengi sana tunayoyajadili tukipingana kimawazo. Nafikiri changamoto inayotukabili sasa ni kimatendo. Kwa sababu ni mengi tunayoongelea, tunayojadili na kupingana nayo tena kwa sana ila nani anasikia malalamiko yetu? Tunafanya nini kuhakikisha tunawawajibisha viongozi wetu?

Alafu kuhusu swala la kupiga kura, I have personally lost faith in the whole system. Leo hii tunaweza tukapigia kura vyama vingine ambavyo sio CCM ila utashangaa CCM bado itashinda, kura zinaibiwa hivi hivi. How do you solve such a problem. Mfumo mzima mbovu!!
 
Tangawizi

Tangawizi

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2009
Messages
2,999
Likes
1,035
Points
280
Tangawizi

Tangawizi

JF-Expert Member
Joined Jun 25, 2009
2,999 1,035 280
Well food of thought! Tulipofika sasa mwana siasa akianza kusema mambo ya umoja na mshikamano unamuangalia kama yuko serious maana wao wenyewe, wakidhani hawaonekani wanayoyafanya, wamesaliti huo umoja na mshikamano kwa kuwa tayari, kuiuza nchi kwa watu wasio wazalendo na wala rushwa wakubwa.
Imefika mahali sasa lazima tutofautiane katika fikra. Naamini sio watu wote wanaonufaika na upuuzi huu ambao wanasiasa wanaufanya. Kama spark ya mabadiliko ya kweli ikionekana, tutashuhudia jinsi watu wachache wanaoamini kuwa wanauwezo wa kututawala wote kwa hila hila watwkavyoshika vichwa kwa kushuhudia kushindwa kwao.
Tunaposhindwa sasa ni sehemu moja...bado hatuna chama wala wanasiasa wenye agenda serious ya kututoa huku kwenye shimo ambalo hawa wajanja wachache wametutumbukiza.Hawapo, na hata kwenye vyama vya upinzani pia hawapo!Kama wapo basi ni tone moja la maji ndani ya bahari.
 

Forum statistics

Threads 1,251,012
Members 481,556
Posts 29,754,132