Ni lazima tugawanyike; Lazima tusiwe na umoja! -Yes I said it

Braza......u are missing something here! hujaelewa Philosophy nzima ya ''KUGAWANYIKA'' aliyoisema MM hapo juu mkuu!

Hivi, wamarekani walivyoamua kugawanyika na kuwa na camp mbili - Obama vs John M......kulimwagika damu? Umesema upo nje, umeona huko Ukraine kilichotokea juzi, wale jamaa wamemwaga damu kumpata Yonkovich? (sorry spelling)?

Mbali na camp za Obama na Mc Cain kulikuwa vile vile na camp ya Obama na Hillary Clinton pamoja kuwa wapo chama kimoja
 
Mwanakijiji, ingekuwa vema kama ungeelezea kidogo 'kugawanyika' ulikokukusudia na kwa nini hutoi suggestion bali unarule kwamba ni lazima tugawanyike.

Ama baada ya hapo, ueleze jinsi tutagavyogawanyika. Sio sahihi kusema tugawanyike bila kutoa muongozo wa huko kugawanyika, at least hata kwenye hitimisho.

Kwa independent thinker, inakuwa vigumu kuunga mkono au kuyakataa mawazo yako ya kulazimisha watu wagawanyike.

ndiyo maana ya kuzua mjadala; siyo kila kitu niseme mimi.. ndiyo maana wengine wananyambua zaidi, wengine wanapinga n.k
 
Kuna tofauti kati ya kugawanyika na kutofautiana. Tunatofautiana. Hatujagawanyika. Wala hatutagawanyika kamwe. Umoja na mshikamano ni urithi wa Chama kilichotukomboa.Tuuenzi na kuulinda umoja na utulivu. Kwa pamoja, Mwanakijiji, Mwanajiji, Mkulima, Mfanyakazi, Mfanyabiashara na Mwekezaji, tujenge Taifa letu changa.

Umoja ni Nguvu!

Companero
ni umoja gani unaosemea huu tuliouona juzi bungeni wa sakata la Richmond au mshikamano wa kuuza maliasili za nchi au ule wimbo wa majukwaani

ngoja nikuambie mshikamano unaoimbwa na CCM si wako wewe mlalahoi ni wa wanamtandao wewe ni kama chombo cha kuzolea taka zao wakishapata hawakutambui wanakusahau wanakutishia amani amani ili ukae kimya

Wazanzibari si wajinga wameliona hilo baada ya kuona wanafanywa mabwege kwa kisingizio cha mshikamano wakasema to hell with your mshikamano wakaanzisha wa kwao unaoitwa mseto wakaidharau CCM na mshikamano wake CCM wamebaki mdomo wazi habari ndiyo hiyo
 
Exactly!

Kutofautiana kwa mapato, mawazo, elimu, dini si kugawanyika hiyo ndio hazina ya maendeleo katika jamii..kwani sisi si kondoo!

Kugawanyika ni upotofu wa fikra na dalili za kukata tamaa kihoja

Si tabia njema ku-advocate kugawanyika badala yake tunatakiwa ku-advocate kutofautiana katika mambo na kuwa pamoja katika kuheshima mawazo ya wengi na wachache ata the time!

Usitake kudanganya watu eti kutofautiana kwa elimu na mapato ni hazina ya maendeleo shule gani ulisoma hayo na mwalimu gani alikufundisha kuwa tofauti ya mapato ni maendeleo this is nonsense thinking kwa nchi changa kama yetu
 
kuna kila dalli kuwa hapa jamvini kuna watu wana kazi ya kumpigia makofi mwanakijiji hata kama hawajaelewa ametoa mawazo gani!!!!!!!!!!!

jamani jaribuni kuthink critically, kama ni kutofautiana kimtazamo, matakwa, itikadi nk. mbona tayari tunatofautiana? tutofautiane mara mbili? au mara ngapi???

ishu ni "kugawanyika" nipeni mfano wa nchi kama yetu hususani ya kiafrika "iliyogawanyika" halafu hapakutokea mapigano/umwagaji damu na badala yake waka[pata maendeleo..............

nakubaliana na hoja za tumaini na companero..............

Yes, you agree with them because you are in the same boat and heading in the wrong direction
 
kwamba mbuzi na chui wakubaliane kutofautiana kuwa nani kati yao amle mwenzake; halafu wanatakiwa kuheshimu "tofauti hiyo".!

Hili ni jibu tosha kabisa kwa Akili kichwani Tumain na Campanero wanajua chui ni nani na mbuzi ni nani halafu eti tushikamane mshikamano wa kinafiki hatuutaki never on earth wazanzibari wameshituka bado sisi huku na si mbali
 
Samahani sana, kuhubiri uhasama wakati uko mbali na un owaambia wahasimiane ni sawa na na sungura kumdanganya nyani kuwa wote wakaue wazazi wao kisha sungura kwenda kuleta damu kutoka kwenye magome ya miti wakati mwenzanke nyani ameshamuua mama yake.MM ni mtaalamu wa lugjha na wengine wote hapa tunapaparuka tu. ukweli utabaki kwa historia humu kwamba VITA INAPIGANWA PALIPONA NA MGOGORO NA SI PENGINE. majirani walio mbali watakwambia tu mbinu na wakati mwingine watakukosoa.

Lugha za MM hapa jamvini zina utata. YAANI NI TUNGO TATA zenyee maana zaidi ya moja na yeye hajawahi kuwa mfafanuzi wanaofanya ufafanuzi ni wana JF. kwa imani huu ni mtego au ni ujanja wa kujua wengine wan fikiri nini. WIZI WA BUSARA NA HEKIMA.

MM anaushawishi mkubwa sana hapa jamvini lakini hajatupeleka hatua ya kupata elimu ya kweli. Tangu vyama vingi vikubaliwe sijawahi kuipigia CCM kura. Jee huku siyo kugawanyika? wewe hatujui kama unapiga kura! Kama mgawanyiko unouongelea ni wa amani kama ulivyojibu basi ungetshawishi tuliokopiga kura upinzani tuendelee.

Mimi ni mwana CCM lakini sikuwahi kuwaamini tangu enzi za Mwinyi..

Nafikiri inatosha , si vizuri kuweka busara yote hapa.
 
Sikubaliani na wewe kama MM ana ushawishi hapa JF watu walio JF nafikiri hawaangalii sana nani kasema wanaangalia nini kasema kama wapo wa aina hiyo basi wachache nakusema anahubiri uhasama wakati yeye yuko mbali si kweli siku hizi hapa duniani hakuna sehemu iliyo mbali na kuwa hero si lazima uwe mstari wa mbele umebeba bango au bunduki

naona wengi hawajamuelewa umoja ambao anasema hautaki nilivyomwelewa mimi ni kama ule wa wabunge juzi walipoungana kwa kitu kisicho na manufaa ilitakiwa wabunge wagawanyike kwa ile hoja angalau nusu kwa nusu 50/50 na si 90/10 kama ilivyoonekana hata mimi nauunga mkono mgawanyiko wa aina hiyo 50/50 ndipo tutakapoona maendeleo vinginevyo hakuna haja ya umoja wa kinafiki
 
Web,
Kama chui ni fisadi (kumbe hana makucha anakula majani kama tumain) then wako sawa kimaumbile tunaweza kuendelea na hoja

Tutafoutiana na huyo fisadi na tutamnyaganya anachokula ambacho si chake sisi kina tumain bila kugawanyika

kwa nini unamnyan'ganya tena? huoni kitendo cha wewe kuwaza kumnyang'anya kunadhihirisha kuwa mlishagawanyika tangu mwanzo? tena mna-conflict, atafurahi? , kwa nini hakuwaza mgawane sawa?
 
Usitake kudanganya watu eti kutofautiana kwa elimu na mapato ni hazina ya maendeleo shule gani ulisoma hayo na mwalimu gani alikufundisha kuwa tofauti ya mapato ni maendeleo this is nonsense thinking kwa nchi changa kama yetu

Hakuna taifa wala halitatokea taifa lemye watu walio sawa kielimu kwasababu watu wengine hawatapenda kusoma hataki kwa kupigwa hii ndio maana tuko tofauti wako watu lazima wawafanyie wengine kazi lakini wote ni binadamu kila moja anamheshimu mwingine kwa nafasi yake..hizo ni facts hakuna anayekudanganya ndugu..

Tofauti ya mapato ni facts ambayo hakuna binadamu anaweza kurekebisha kwasababu kupata ni matokeo ya juhudi binafsi, elimu na majaaliwa ya mwenye kugawa riziki..usiniulize mwalimu aliyenifundisha mimi mwenyewe mwalimu nasoma naona hali halisi pia (experience)

Kutofautiana kwa mapato, elimu, dini, rangi , mila etc ndio maendeleo yenyewe nimeseama hapo juu sisi si kondoo "kutofautiana na kuheshimiana bila kugawanya ndio msingi wa maendeleo ..rudi shuleni ndugu..kichwa ngumu
 
Hili ni jibu tosha kabisa kwa Akili kichwani Tumain na Campanero wanajua chui ni nani na mbuzi ni nani halafu eti tushikamane mshikamano wa kinafiki hatuutaki never on earth wazanzibari wameshituka bado sisi huku na si mbali

Acha emotions wewe, tunaongelea kutofautiana siyo kushikamana kinafiki hiyo inaonyesha hujui tofauti ya kutofautiana na kushikamana? kasome dictionary

Hypothesis ya chui na mbuzi ni null and void, hakuna chui wala mbuzi kuna either mbuzi tu au chui tu (binadamu kimaumbile) tukianzia hapo tutajadili mada kwa hoja zilizo sawa..lakini ikishaweka statement mfu (kama hii ya mwanakijiji) utatoa hoja mfu na supporters kama wewe wenye mawazo mfu vilevile

Tunaongelea taifa la watu ambao watatofautiana bila kugawanyika si mataifa mawili ya chui na mbuzi hapo hakuna mfano ili ni kuhalalisha vurugu na upuuzi
 
Mbuzi tu ama chui tu binadamu kimaumbile maana yake nini?Nani anazungumzia maumbile hapa?
 
Hakuna taifa wala halitatokea taifa lemye watu walio sawa kielimu kwasababu watu wengine hawatapenda kusoma hataki kwa kupigwa hii ndio maana tuko tofauti wako watu lazima wawafanyie wengine kazi lakini wote ni binadamu kila moja anamheshimu mwingine kwa nafasi yake..hizo ni facts hakuna anayekudanganya ndugu..

Tofauti ya mapato ni facts ambayo hakuna binadamu anaweza kurekebisha kwasababu kupata ni matokeo ya juhudi binafsi, elimu na majaaliwa ya mwenye kugawa riziki..usiniulize mwalimu aliyenifundisha mimi mwenyewe mwalimu nasoma naona hali halisi pia (experience)

Kutofautiana kwa mapato, elimu, dini, rangi , mila etc ndio maendeleo yenyewe nimeseama hapo juu sisi si kondoo "kutofautiana na kuheshimiana bila kugawanya ndio msingi wa maendeleo ..rudi shuleni ndugu..kichwa ngumu

Kama tofauti ya elimu inasababishwa na mtu mwenyewe kutopenda kusoma sawa lakini kama inasababishwa na umasikini hilo si sawa ni kosa

Hii tofauti ya mapato tanzania unaiona sawa basi utakuwa unamiss kitu fulani kichwani
 
Acha emotions wewe, tunaongelea kutofautiana siyo kushikamana kinafiki hiyo inaonyesha hujui tofauti ya kutofautiana na kushikamana? kasome dictionary

Hypothesis ya chui na mbuzi ni null and void, hakuna chui wala mbuzi kuna either mbuzi tu au chui tu (binadamu kimaumbile) tukianzia hapo tutajadili mada kwa hoja zilizo sawa..lakini ikishaweka statement mfu (kama hii ya mwanakijiji) utatoa hoja mfu na supporters kama wewe wenye mawazo mfu vilevile

Tunaongelea taifa la watu ambao watatofautiana bila kugawanyika si mataifa mawili ya chui na mbuzi hapo hakuna mfano ili ni kuhalalisha vurugu na upuuzi

Hakuna haja ya kusoma dictionary mbona maneno yenyewe yako tofauti kabisa

acheni hizo hypothesis zenu za mbuzi msitake kuchanganya watu hapa tunaongelea umoja fake wa wabunge wenu wa CCM mshikamano wa kufilisi nchi nyie mnatuletea hadithi za sungura na fisi hachanganywi mtu hapa
 
Mbuzi tu ama chui tu binadamu kimaumbile maana yake nini?Nani anazungumzia maumbile hapa?

Ndugu yangu jmushi1 hawa watu wanamalengo yao wanataka kupoteza madhumuni ya topic hii wanatuletea hadithi nyingi za kitoto mara mbuzi mara chui wapi na wapi tulishawagundua zamani
 
Moja ya matatizo yetu makubwa, ni kwamba tumezoea sana "groupthink" na collectivism. Pengine kwa sababu kujiamini ni kudogo na pia kuungaunga kwingi.Hizi falsafa za collectivism ndizo zinatufanya tuzunguke katika "vicious circle of poverty". Watu wenye kuuliza mambo provoking and critical wachache, kila mmoja anakuwa restricted na smallmindedness na kuogopa traditions ambazo mpaka leo hazijatusaidia that much.

Critical thinking mara zote huwa haiendi na blatant groupthink, paradigm shifts mara zote huwa haziendi na licensed groupthink, renaissances mara zote huwa haziendi na overt groupthink, why, hata Sarah Palin knows that "only ead fish go with the flow" and George Patton once said if you see people greeing too much that should be enough to show that there is a problem there, the Copernicuses, Galileos, Newtons and Einsteins of this world, just to take examples from science, did not change this world with groupthink.
 
Je wanaharakati wa ukombozi wa Afrika ya Kusini walikuwa wamoja na utawala wa makaburu - hapana; je wanamapinduzi walioongoza uasi dhidi ya utawala wa Mfalme George wa Uingereza kule Marekani walijaribu kuwa wamoja na ndugu zao ng'ambo ya atlantic? la hasha!

Kugawanyika tunakokupendekeza siyo kugowanyika kunakotokana na chuki binafsi, wivu, husuda au vitu ambavyo kimsingi havina uzito wa hoja. Kugawanyika tunakopendekeza kunatokana na kile wengi wameshakisema hapa yaani "tofauti". Wapo wale wanaotaka tuamini kwamba tofauti zetu zinatuunganisha badala ya kwamba zinatugawanisha.

Unapokuwa na kundi la watu ambao wameweka chama chao mbele kuliko taifa, mgawanyiko ni lazima!

Unapokuwa na kikundi cha watu ambao wanaamini wawekezaji wa kigeni ndio wataleta maendeleo ya taifa letu; mgawanyiko ni lazima!

Unapokuwa na watu wanaoamini kuwa katika taifa zima hakuna mtu mwingine mwenye uwezo wa kuongoza isipokuwa mmoja basi mgawanyiko ni lazima!

Unapokuwa na mfumo wenye kuzalisha utawala wa kifisadi ambapo kundi la watu wachache wamekuwa ni walaji wakuu wa ile keki ya taifa na wengine wakibakia kutamania toka mbali, basi mgawanyiko ni lazima!

Mgawanyiko ninauzungumzia ni kutenganga kiitikadi, kimkakati, kimtazamo, na kimwelekeo wa utatuaji wa matatizo yanayokabili taifa letu. Ni mgawanyiko ambao lengo lake ni kuhakikisha kuwa wanaotawala sasa hawapati nafasi hiyo tena na badala yake kutafuta watawala wengine ambao watakubalina na yale tunayoyapendekeza kama tiba ya matatizo yetu kama taifa. Ni mgawanyiko ambao hauna uwezekano wa upatano, umoja, urafiki, au kwa namna yoyote ile.

Kukubaliana na hilo yaweza kuwa ni group thinking, kutamani jambo hilo hilo laweza kuwa ni group thinking.. but well.. ninapokubaliana na ukweli ambao wengi nao wameukubali siwezi kuomba radhi kwamba tunakubaliana na ukweli huo.

Lakini uzuri wa demokrasia ni kuwa wale wanaopinga na wenyewe wanaweza na wanapaswa kusema kwanini tuungane na kwa nini tusigawanyike mbele ya uovu!.
 
Naona umeweka pointi nzuri sana mwanakijiji. Baadhi ya watu wanadhani kuwa kutofautiana ni kupigana. Sioni kama hilo ni kweli, kwa ujumla watanzania si watu wa vurumai, wala shari. watu wa shari ni wanasiasa ambao wanajaribu kutuchochea kwa manufaa yao binafsi. Tunatakiwa tuwe na true opposition, tunatakiwa tuwe na alternative government in waiting hawa jamaa wataacha kutuchezea.

Mkuu mmoja alaisema wazi kuwa hawatishiki hata kidogo, kwa kuwa nguvu yao iko ijijini wanaweza kufanya lolote wanalotaka na watashinda tu kwenye uchaguzi. So ni better tuwe na opposition inayoweza kufika vijijini kabisa, vyama vyetu vinatakiwa kufanya kazi zaidi huko tunakoibiwa zaidi au kwenye ngome ya walaghai.
 
Je wanaharakati wa ukombozi wa Afrika ya Kusini walikuwa wamoja na utawala wa makaburu - hapana; je wanamapinduzi walioongoza uasi dhidi ya utawala wa Mfalme George wa Uingereza kule Marekani walijaribu kuwa wamoja na ndugu zao ng'ambo ya atlantic? la hasha!

Kugawanyika tunakokupendekeza siyo kugowanyika kunakotokana na chuki binafsi, wivu, husuda au vitu ambavyo kimsingi havina uzito wa hoja. Kugawanyika tunakopendekeza kunatokana na kile wengi wameshakisema hapa yaani "tofauti". Wapo wale wanaotaka tuamini kwamba tofauti zetu zinatuunganisha badala ya kwamba zinatugawanisha.

Unapokuwa na kundi la watu ambao wameweka chama chao mbele kuliko taifa, mgawanyiko ni lazima!

Unapokuwa na kikundi cha watu ambao wanaamini wawekezaji wa kigeni ndio wataleta maendeleo ya taifa letu; mgawanyiko ni lazima!

Unapokuwa na watu wanaoamini kuwa katika taifa zima hakuna mtu mwingine mwenye uwezo wa kuongoza isipokuwa mmoja basi mgawanyiko ni lazima!

Unapokuwa na mfumo wenye kuzalisha utawala wa kifisadi ambapo kundi la watu wachache wamekuwa ni walaji wakuu wa ile keki ya taifa na wengine wakibakia kutamania toka mbali, basi mgawanyiko ni lazima!

Mgawanyiko ninauzungumzia ni kutenganga kiitikadi, kimkakati, kimtazamo, na kimwelekeo wa utatuaji wa matatizo yanayokabili taifa letu. Ni mgawanyiko ambao lengo lake ni kuhakikisha kuwa wanaotawala sasa hawapati nafasi hiyo tena na badala yake kutafuta watawala wengine ambao watakubalina na yale tunayoyapendekeza kama tiba ya matatizo yetu kama taifa. Ni mgawanyiko ambao hauna uwezekano wa upatano, umoja, urafiki, au kwa namna yoyote ile.

Kukubaliana na hilo yaweza kuwa ni group thinking, kutamani jambo hilo hilo laweza kuwa ni group thinking.. but well.. ninapokubaliana na ukweli ambao wengi nao wameukubali siwezi kuomba radhi kwamba tunakubaliana na ukweli huo.

Lakini uzuri wa demokrasia ni kuwa wale wanaopinga na wenyewe wanaweza na wanapaswa kusema kwanini tuungane na kwa nini tusigawanyike mbele ya uovu!.

Umeshaanza ku-qualify "kugawanyika kwend kwenye maana ya kutofautiana kwa mzunguko wa maneno"

Kutengana kiitikadi, kimtazamo, na mwelekeo tayari tunao hapa kwetu ndio maana kuna vyama vina amini serikali mbili nyingine serikali tatu, wengine tunaamini Uislam wewe unaamini ukristo, wengine wanamtazamo wa kipebari wengine ujamaaa..list goes on...wengine wanaamini wageni wengine wanaamini wazawa ni mtazamo na fikra...

Lakini huko si kutengana kama taifa au kama jamii huko ni kutofautiana ambayo hakuna mwenye shida na hayo ..inabidi yaboreshwe zaidi kitaasisi ifikie mahali tofauti za kimawazo na mtazamo iwe huru na malumbano yenye tija na kuibua fikra yafanyike kwa kila uamuzi wa kitaifa...
 
Back
Top Bottom