Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Mara kwa mara watawala wamekuwa wakituasa kuwa tofauti zetu zisisababishe mgawanyiko katika jamii na kuwa ni muhimu kuendeleza "umoja, utulivu na mshikamano".
Mimi nimeamua kukataa kuwa na umoja wa namna hii! Demokrasia ya kweli inatulazimisha kutofautiana kwa hoja, sera, na hata mitazamo; tofauti hizi zinatusababisha kushindwa kukaa pamoja na kukubaliana. Hivyo, kuna wakati ambapo mgawanyiko siyo tu ni muhimu lakini ni lazima vile vile.
Mgawanyiko tunaouona kula Iran
Mgawanyiko tuliouna kati ya mashabiki wa Bush na Obama
Mgawanyiko kati ya KANU na kina Mwai
Kama tunataka tupige kura inavyopaswa mwaka huu, ni lazima tugawanyike! CCM wanaelewa lugha ya mgawanyiko tu.. ndio maana leo wamekubali kukaa meza moja na CUF kwa sababu Wazanzibari wamegawanyika!!
Bara tunaogopa siasa za "kugawanyika" na hivyo tunalazimishwa kuwa katika umoja wa ulaghai na mshikamano wa uongo; haiwezekani kuwafunga ng'ombe na punda walime pamoja!
Wao wenyewe wanatugawanya sana karibu kila siku; tatizo kuwa tukianza kugawanyika wanashangaa mbona tunagawanyika! Ni kama mambo yale ya "Ukipanda nshale, ukishuka nshale, ukitingishika nshale, usiseme wala usimumunye!! "
Kwanini tunaogopa kugawanyika? je twapaswa kugawanyika? Je mgawanyiko huu ni lazima uwe wa vurugu na mapigano? Je ni ni lazime damu imwagike au tunaweza kugawanyika na kutafuta mwelekeo mpya wa taifa bila ya vurugu, umwagikaji wa damu au uhasama kama ilivyotokea kwenye mataifa mengine?
Je wanaharakati wa ukombozi wa Afrika ya Kusini walikuwa wamoja na utawala wa makaburu - hapana; je wanamapinduzi walioongoza uasi dhidi ya utawala wa Mfalme George wa Uingereza kule Marekani walijaribu kuwa wamoja na ndugu zao ng'ambo ya atlantic? la hasha!
Kugawanyika tunakokupendekeza siyo kugowanyika kunakotokana na chuki binafsi, wivu, husuda au vitu ambavyo kimsingi havina uzito wa hoja. Kugawanyika tunakopendekeza kunatokana na kile wengi wameshakisema hapa yaani "tofauti". Wapo wale wanaotaka tuamini kwamba tofauti zetu zinatuunganisha badala ya kwamba zinatugawanisha.
Unapokuwa na kundi la watu ambao wameweka chama chao mbele kuliko taifa, mgawanyiko ni lazima!
Unapokuwa na kikundi cha watu ambao wanaamini wawekezaji wa kigeni ndio wataleta maendeleo ya taifa letu; mgawanyiko ni lazima!
Unapokuwa na watu wanaoamini kuwa katika taifa zima hakuna mtu mwingine mwenye uwezo wa kuongoza isipokuwa mmoja basi mgawanyiko ni lazima!
Unapokuwa na mfumo wenye kuzalisha utawala wa kifisadi ambapo kundi la watu wachache wamekuwa ni walaji wakuu wa ile keki ya taifa na wengine wakibakia kutamania toka mbali, basi mgawanyiko ni lazima!
Mgawanyiko ninauzungumzia ni kutenganga kiitikadi, kimkakati, kimtazamo, na kimwelekeo wa utatuaji wa matatizo yanayokabili taifa letu. Ni mgawanyiko ambao lengo lake ni kuhakikisha kuwa wanaotawala sasa hawapati nafasi hiyo tena na badala yake kutafuta watawala wengine ambao watakubalina na yale tunayoyapendekeza kama tiba ya matatizo yetu kama taifa. Ni mgawanyiko ambao hauna uwezekano wa upatano, umoja, urafiki, au kwa namna yoyote ile.
Kukubaliana na hilo yaweza kuwa ni group thinking, kutamani jambo hilo hilo laweza kuwa ni group thinking.. but well.. ninapokubaliana na ukweli ambao wengi nao wameukubali siwezi kuomba radhi kwamba tunakubaliana na ukweli huo.
Lakini uzuri wa demokrasia ni kuwa wale wanaopinga na wenyewe wanaweza na wanapaswa kusema kwanini tuungane na kwa nini tusigawanyike mbele ya uovu!.